11 Oct 2017 in National Assembly:
Ahsante na naunga mkono Hoja hii, Mhe. Spika wa Muda.
view
16 Mar 2017 in National Assembly:
On a point of order, Hon. Temporary Deputy Speaker.
view
16 Mar 2017 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. I think we are discussing a very important Motion today and yet we are only four members in this Chamber. I do not think we can proceed with this important Motion for our country while we are only four Members. The decision that will be made from this Motion will affect this country and it is wrong for only four members to make it. I do not think we have quorum under Standing Order No.35 to proceed with this Motion. Thank you.
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwa kweli, Hoja hii ni ya kushangaza. Kuzungumza kuhusu Bunge hili kupitisha mkopo wa Kshs27.3 bilioni ni jambo la kushangaza. Huu mradi ambao unafanyika Mombasa ni mradi ambao tukiwa watu wa Pwani na Wakenya, tungependa uwe kwa sababu ya kuinua uchumi wa nchi hii na uchumi wa Pwani. La kushangaza ni kwamba jambo hili limeletwa Bungeni ilhali mradi huu unaendelea. Ninashindwa pesa hizi zilikuwa zimepangiwa kulipwa namna gani ilhali huu ni mradi ambao tayari umeanza. Isitoshe, linalonishangaza ni kwamba mbali na kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuinua uchumi wetu, ni vipi tutaweza kusaidia sehemu ...
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Kwa kweli, hatuwezi kukataa maendeleo yasifanyike, na tukiwa kama viongonzi tuna kila haki kuhakikisha kwamba tumesaidia nchi hii katika swala nzima la uchumi wetu. Lakini, mambo mengine kama haya yanahitaji maswala mengi kutoka kwetu sisi viongozi. Kwa mfano, tunasema kwamba tutachukua takribani miaka 34 kulipa deni hili na ilhali tuna uhakika KPA ni shirika moja katika nchi hii linaloingiza pesa nyingi sana. La ajabu ni kwamba leo Serikali inajiongezea madeni kama haya, na nina imani kwamba mzigo huu utakuwa wa wananchi. Hili linatendeka ilhali ushuru unaotozwa mizigo katika bandari ni wa juu. Baadaye wanaoleta bidhaa ama kufanya biashara katika nchi ...
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Kama viongozi tunahitaji kujadiliana pakubwa kabla hatujajiweka katika madeni kama haya ambayo mwisho wake kama ninavyosema, yatakuwa mzigo wa mwanachi wa Kenya wa kawaida. Mimi ningependa kusema kwamba kuna miradi mingi ambayo inahitaji kufanyika na ni bora zaidi. Kama hizi pesa zitatumika, zitafungua milango nchini na kuinua uchumi.
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Kama nilivyosema, tunahitaji maendeleo na uchumi uinuke katika nchi hii lakini ninaona Hoja hii ina maswala mengi ambayo tunahitaji kufahamu kupitia kwa Serikali ama kupitia wahusika. Hatuoni haja kama viongozi kupitisha pesa hizi halafu ziwe mzigo kwa wananchi ama kupitisha pesa hizi ilhali kuna sehemu zingine kama nilivyosema kama Lamu zinazohitaji pesa hizi ili miradi ambayo imekwama kama hii iendelee.
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Kwa hivyo, ningeomba Serikali ihakikishe kwamba tumefanya mambo ambayo yatawaridhisha wananchi na kuinua nchi hii ili tuweze kuimarisha chumi wetu. Tusifanye haya kwa sababu ya ubinafsi wa watu ama maslahi ya watu fulani katika nchi hii.
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
10 Mar 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii nikiwa mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Ardhi, kuzungumza kuhusu Mswada huu wa swala nzima la ardhi ambalo limeletwa hapa Bungeni. Ningependa kuipongeza Kamati kwa juhudi zake na yale ambayo wameweza kufanya mpaka kufikisha huu Mswada hapa. Utakubaliana nami ya kwamba swala la ardhi nchini ni nyeti na halihitaji kujadiliwa kiufupi ama kwa namna isio sawa. Hivi sasa Wakenya wengi wana hamu kubwa kujua swala hili limekuwa na mwelekeo upi katika nchi yetu ya Kenya. Tukiangazia pakubwa, Wakenya walipigia Katiba kura na wakaweka Tume ya Ardhi ili kutatua na ...
view