Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 421 to 430 of 512.

  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia mjadala huu muhimu ambao unaangazia masuala ya afya ya Wakenya. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Naibu Spika wa Muda, kabla ya kuendelea, nilikuwa nimeomba hoja ya nidhamu kuhusiana na suala hili nzima. Hoja hii inaonekana imetia hamasa wengi na wangependa kuchangia lakini naona muda haupo nasi maana umetupa kisogo. Pengine kupitia utaratabu wa Bunge hili, Sheria za Bunge, Kifungu Nambari 97(4), ningeomba muda wa kuongea pengine upunguzwe kutoka dakika kumi hadi tano ili wenzetu wengine nao waweze kupata fursa ya kuchangia ikiwa itawezekana. Naibu Spika wa Muda, ningependa kumpongeza Mhe. Ali kwa fikira ya kuleta Hoja hii hapa.Vile vile, ningependa kumpongeza kwa ule utafiti ameweza kufanya kikamilifu kuhusiana na suala nzima la afya katika nchi ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: watasaidika namna gani. Kama nilivyosema, kuna umuhimu wa kuangalia suala hili na kuliangazia kwa undani kabisa. Tatizo ni nini na limesababishwa na nini? Naibu Spika wa Muda, Hospitali ya Mombasa kwa hivi sasa hakuna asiyejua kwamba inapokea wageni kupitia kila sehemu katika masuala ya matibabu. Iwe ni wageni kutoka Lamu, Kilifi ama sehemu tofauti, wote huenda Hospitali ya Mombasa. La kusikitisha ni kuwa Bunge hili likikaa kugawanya pesa za mashinani ama za kaunti ama kugawanya pesa katika Bajeti yake kila mwaka, sijaona mambo haya yakifikiriwa. Jambo ambalo ningependekeza tunaposubiri ujenzi ambao umependekezwa wa hospitali nyingine kule Mombasa, tayari hospitali hii ... view
  • 27 Feb 2018 in National Assembly: Asante Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati hii pamoja na kamati yake kwa kazi nzuri ambayo wameifanya. Tunalolizungumzia leo hapa ni Mswada muhimu sana katika nchi yetu. Unahusiana na barabara zetu, mipangilio ya Serikali na utaratibu wa kuinua hali ya barabara zetu nzuri. Kitu muhimu ambacho nataka tufahamu kwanza ni kujua umuhimu wa barabara katika nchi yetu na katika ulimwengu kwa ujumla. Vile vile, nataka tufahamu katika nchi yetu ya Kenya ni hatua gani tumepiga katika suala nzima la barabara. Kwa kweli, mbali kwamba tutaipongeza Serikali ilioko kwa juhudi zake bado kuna matatizo ambayo ... view
  • 27 Feb 2018 in National Assembly: yanaonekana kupitia kwa wanakandarasi wanaopewa kandarasi hizi ama kupitia wale wahusika wanaopewa kuendesha jambo hili. Mhe. Naibu Spika wa Muda, utakubaliana nami kwamba barabara ni muhimu sana katika nchi yetu ya Kenya kwa sababu inarahisisha usafiri na vile vile inainua uchumi wa sehemu yoyote ambayo kuna barabara nzuri. Tutaweza kufaidi vipi mambo kama haya katika hili suala nzima? Tatizo liko Serikalini au wahusika vile nilivyosema? Tatizo liko kwa wahusika na kandarasi. Mhe. Naibu Spika wa Muda, Serikali inatumia pesa nyingi sana katika sekta hii ya barabara. Bilioni za pesa zinatumika kila mwaka tunapopanga Bajeti ya nchi. Mbali kwamba bilioni za ... view
  • 27 Feb 2018 in National Assembly: Hii itasaidia kuokoa pesa ambazo Serikali inatumia kwa namna hiyo. Vile vile, itasaidia kwamba mwanakandarasi yeyote atakayepewa kazi ataifanya kulingana na vile vigezo vinayotakikana. Vile vile, katika suala hili la barabara, utapata kwamba mwanakandarasi mmoja anapewa kilomita 100. Thamani ya pesa ni Ksh10 bilioni had Ksh20 bilioni. Mwanakandarasi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 27 Feb 2018 in National Assembly: huyo anatumia miaka kumi ama miaka saba kutengeneza barabara ile ya kilomita mia moja. Kwa nini barabara ile isigawanywe miongoni mwa wanakandarasi watano, kwa mfano, ndiyo kila mwanakandarasi apewe kilomita 20? view
  • 27 Feb 2018 in National Assembly: Ikiwa mwanakandarasi yule atapewa kilomita 100 kuzijenga kwa miaka mitano, kazi hiyo ikigawanyiwa wanakandarasi watano, wataikamilisha kwa muda wa mwaka mmoja. Mikakati kama hiyo ndiyo itaifanya Serikali kuokoa pesa ambazo zitaiwezesha kufanya mambo mengine badala ya kutumia pesa kwa njia moja peke yake kwa njia ambazo sivyo. view
  • 27 Feb 2018 in National Assembly: Nataka kuipongeza Serikali kwa juhudi zake nikizungumzia Eneo Bunge la Lamu Mashariki na Kaunti ya Lamu kwa jumla. Kwa mara ya kwanza, wakazi katika Kaunti ya Lamu wameweza kupata barabara ya lami. Lakini kwa masikitiko makubwa, mwanakandarasi anayetengeneza barabara kutoka Garsen mpaka Lamu ana mwaka mmoja hivi sasa ameshapewa cheti. Mheshimiwa Rais ametia barabara wakfu lakini mwanakandarasi huyo hajatengeneza barabara hiyo, na haya ndiyo matatizo. Tuko na barabara ambayo inatoka Lamu kwenda Kiunga. Tunasikia mara kwa mara kuna magaidi na kadhalika. Barabara hiyo ikitengenezwa na iwekwe lami, itasaidia pakubwa katika masuala haya. Kwa hivyo, mimi naunga mkono lakini kama nilivyosema, ... view
  • 21 Feb 2018 in National Assembly: Asante Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii inayohusiana na maswala ya usalama katika nchi yetu hususan katika sehemu ya Wajir. Kwa kweli, swala la usalama ni swala nyeti sana. Limeweza kushuhudiwa mara kadhaa na limeweza kuleta madhara katika sehemu nyingi. Pia, limeweza kuleta madhara katika uchumi wetu, elimu ya watoto wetu na afya ya Wakenya. Si mara ya kwanza swala hili kujadiliwa Bungeni katika swala zima la usalama. Kule kutokana kwa mara kadhaa Bungeni inamaanisha kwamba limekuwa ni donda sugu. Kwa maana hii, linaonekana kwamba haijapatikana suluhisho katika swala zima. Ingawaje ningependa kushukuru Serikali ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus