Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 401 to 410 of 512.

  • 13 Feb 2019 in National Assembly: Vile vile, tumeshuhudia mara nyingi sana nchi hii ikilalamika kuhusiana na masuala ya uchumi na matatizo mengineo. Naamini pakubwa haya yanasababishwa na hali ya kutodhibiti kile tunachopata kwa uangalifu. Asilimia 25 ambayo inaenda kwa kaunti sio pesa kidogo. Lakini utapata ya kwamba pesa hizi zinazoenda kwa kaunti, kaunti nyingi bado zinalalamika kuhusiana na miradi na maendeleo. Naamini pakubwa kwamba kama utaratibu huu ambao tuaujadili hapa utaweza kutumika kiusawa, nina imani kwamba matatizo kama haya hayatashuhudiwa mbeleni. Ukweli ni kwamba nchi hii ina umuhimu mkubwa wa kuhakikisha ya kwamba fedha za umma zimedhibitiwa na zimetumika kiusawa na kiuangalifu. view
  • 13 Feb 2019 in National Assembly: Utakubaliana nami kwamba matatizo haya yanapatikana kwa wahusika wakuu wanaoendesha mwongozo kama huu ambao tunaujadili hapa Bungeni. Ni matumaini yangu makubwa na nina imani kwamba kama mwongozo huu utafuatwa kikamilifu na vile unavyotakikana, basi fedha za umma zitadhibitika na matarajio makubwa ya wananchi yatapatikana. view
  • 13 Feb 2019 in National Assembly: Vile vile, mbali ya kwamba tunayazungumzia haya leo ama tunayajadili marekebisho haya, ni lazima tukubali matatizo yako na ni sisi tunayasababisha kupitia serikali za kaunti ama Serikali Kuu. Utapata kwamba utaratibu huu ambao tunaujadili hapa, wengine wanautumia kama sababu kwa mambo yao ya kibinafsi. Mfano ni namna serikali za kaunti zinavyotaka kutumia pesa zao. Lakini hapa katikati, hofu ni kwamba kuna baaadhi ya Wakenya ambao ni wahusika katika kutumia utaratibu huu. Wanatumia mbinu za kusikitisha badala ya kufanya mambo kiutaratibu hasa kwa kuzingatia mwongozo huu ambao tunazungumzia. Kuna miradi ambayo inahitaji kufanywa kila mwaka lakini hucheleweshwa kwa sababu ya mwongozo ... view
  • 13 Feb 2019 in National Assembly: kwamba tumetembea na mwongozo huu kikamilifu. Tusilete mvutano kati ya wahusika na kaunti. Kuna wakati pengine mkandarasi amefanya kazi yake kwa utaratibu lakini inapofika wakati wa kulipwa, kwa sababu ya vigezo hivyo ambavyo tumeweka hapa, serikali ya kaunti inasema kwamba utaratibu ndio una matatizo. Hivyo basi, mkandarasi anachelewa kupewa pesa zake kwa sababu kama hiyo. Ninaamini kwamba ni mwongozo mzuri. Wakenya wanahitaji huduma bora. Mbali na hayo, ninaamini pakubwa huduma hizi zitapakitana ikiwa kutakuwa na mwongozo kamilifu na viongozi husika wataweza kumakinika na kuhakikisha wamekubali kufuata utaratibu na sharia zilizowekwa. view
  • 13 Feb 2019 in National Assembly: Magavana tunawajua. Sifa za wengi wao zinajulikana. Siyo wote wenye sifa za kupendeza. Udhaifu upo ndani ya baadhi ya ndugu zetu. Kutokana na hali hii ambayo tunajadili sasa hivi, ni vyema kuhakikisha kwamba mwongozo huu umewekwa vikwazo vya kisheria namna inavyotakikana. Hivyo, tutahakikisha kwamba yeyote ambaye ni mhusika katika kaunti ni mhusika wa kuendeleza kaunti. Masuala ya fedha yatadhibitiwa kwa njia ya furaha kubwa. Serikali ya kitaifa yafaa kuhakikisha kwamba imepeana mwongozo kwa serikali za kaunti kuhusu matumizi ya fedha. Tumeshuhudia mara kadhaa matatizo katika kaunti tofauti tofauti. Mimi naona yamesababishwa na hali ambayo haikuwa hapo mbeleni ya kuweka utaratibu ... view
  • 13 Feb 2019 in National Assembly: Ahsante. view
  • 5 Dec 2018 in National Assembly: Athman (Lamu East, JP): Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumpongeza ndugu yetu ambaye ameleta Hoja hii Bungeni. Vile vile, niwapongeze Wabunge ambao wameweza kuchangia Hoja hii. La muhimu kwanza ni lazima kufahamu kama viongozi malengo na umuhimu wa Hoja hii ni nini. Tunaweza kuzungumza na kujadili lakini mwishowe ikawa umuhimu wake usipatikane kwa jamii. view
  • 5 Dec 2018 in National Assembly: Kama tunavyofahamu, ulimwengu wa leo umebadilika kwa namna nyingi sana, ndiposa fikira hii imefika mahali pa kwamba ni muhimu sana kwa Serikali kuhakikisha kwamba wameweza kulitekeleza jambo hili punde tu tutakapolipitisha hapa Bungeni. Leo hii mambo mengi yanavyoendeshwa ulimwenguni kwa ujumla yanatumia mitandao katika kupata zile habari ama kutuma habari zozote zinazohusiana na mambo ya kileo. Lakini kwa masikitiko makubwa katika sehemu nyingi sana katika nchi hii, utapata kwamba mambo kama haya hayapatikani. Utapata sehemu nyingi sana wanatumia zile teknolojia za zamani katika kuwasiliana na mambo mengi sana ama kuweza kufanya zile shughuli zao za kileo. Ukweli ni kwamba sio ... view
  • 5 Dec 2018 in National Assembly: Ningependa kuunga mkono na kuhimiza ya kuwa lifanyiwe haraka jambo hili na litekelezwe kikamilifu. Jambo ambalo singependa lipatikane ni kwamba watashirikishwa waezekaji wa kibinafsi. Kama tutafanya hivyo, basi, itakuwa bado hatujasonga mbele. Leo hii waekezaji wa kibinafsi wanaweza kufanya huduma hii katika sehemu ambazo hamna, lakini tunapolijadili hapa, huwa tunapendekeza Serikali ichukue majukumu haya kwa sababu matatizo yale ambayo tunayahofia sasa hivi, walioko mashinani hawapati huduma hizi. Hata kesho zikifika huduma hizi na ikiwa wameshirikishwa hawa waekezaji wa kibinafsi gharama zitakuwa vile vile. Kwa hivyo, ningependa Serikali iingilie kikamilifu na kuhakikisha wametekeleza huduma hii kwa Wakenya wengi. Asante. view
  • 4 Dec 2018 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka nikubaliane na Kiongozi Wa Wengi Bungeni kwamba hili jambo tayari liko kwenye Katiba yetu. Vile nakubaliana na yule aliyeleta kutaka kurekebisha haya. Ukweli ni kwamba, matatizo juu ya maswala haya yapo. Pesa zinatengwa na Bunge; zina kwenda kwa wizara; kandarasi inatangazwa; anayefanya kandarasi ile inatia sahihi makubaliano ya kandarasi. Lakini ajabu ni kwamba, ikifika wakati wa malipo, linakuja swala lile kwamba hakuna pesa. Si serikali ya kaunti, ama Serikali ya uma. Kuna mkandarasi anadai pesa. Amefanya kazi takriban miaka miwili na alitia sahihi maafikiano na hajalipwa pesa: Anaambiwa hakuna pesa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus