4 Dec 2018 in National Assembly:
Kuna mwongozo wa kwamba wakati mkandarasi amefeli kufanya kazi yake, kuna utaratibu wa kujadili swala hili ili kuliweka sawa. Ningependa hata ikiwa ni Serikali kuu ama ile ya kaunti, wakati mkandarasi amefanya kazi ayke, amepeana lile cheti la malipo na ikiwa umepita muda fulani na hajalipwa pesa yake, kuwe na njia ya kuhakikisha kwamba mkandarasi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
4 Dec 2018 in National Assembly:
huyu amepewa uwezo wa kulipwa fidia katika swala hilo ama iandaliwe namna ya kuhifadhi kandarasi hiyo. Tatizo hilo lipo na ni lazima Bunge hili liangazie vizuri tatizo hilo kwa sababu wanakandarasi wengi wanateseka kwa kufanya kazi katika kaunti zetu na Serikali kuu. Tunajua kwamba pesa hizi ziko kwenye bajeti na zimepelekwa kwenywe wizara lakini sijui ni njia gani wanaotumia hawa kuhakikisha wamewadhalilisha wanakandarasi hawa. Mwishowe yafaa tutafute mbinu ya kuwasaidia hawa wakandarasi.
view
31 Jul 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kulaani kitendo ambacho kilifanyika cha ukosefu wa nidhamu kwa dini zetu ambazo zimetambulika ulimwenguni huu. Ingawaje pengine Mheshimiwa na watu wake wa Garissa watalisamehe jambo hili, nataka ukubaliane na mimi kwamba mhusika mkuu ndiye anapaswa kuchukue nafasi hii ya kuomba msamaha hata si kwa jamii ya Garissa, bali kwa mwenyezi Mungu. Dini zote hizi si za binadamu ni za Mwenyezi Mungu. Hajamkosea binadamu, amemkosea Mwenyezi Mungu. Dini zote zinazotambulika, hususan zile dini ambazo zimepewa vile vitabu ambavyo vinatambulika katika ulimwengu huu, ni za Mwenyezi Mungu. Waislamu ni watu wa amani. ...
view
4 Jul 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kuunga mkono Mswada huu ambao uko mbele yetu hapa leo. Nikiamini pakubwa, ni Mswada ambao wakenya wamekuwa wakiusubiri kwa siku nyingi sana. Hakukua na mwongozo kamili katika swala hili nzima ya maswala ya ardhi. Ingawaje mwaka wa 2010 Wakenya walipitisha Katiba, miongoni mwao yalikua ni haya ya kuweka Tume ya Ardhi ili kusawazisha tatizo hili la ardhi. Leo hii tutapata kwamba, Kenya nzima, sana sana Pwani ambako nimetoka kumekua na tatizo kubwa katika swala la ardhi. Matatizo haya yamesababishwa na kutokuwa na mwongozo kamili katika swala hili, kwa namna watu ...
view
4 Jul 2018 in National Assembly:
Ningependa kuunga mkono wenzangu na ningeomba Serikali ihakikishe kwamba utaratibu huu umefuatwa kikamilifu na wale wote ambao wataathirika na swala hili wazingatiwe kikamilifu na kupewa haki zao. Ili amani kupatikana na mwongozo ama uchumi kuendelea kisawasawa katika nchi hii, ni lazima haki ya kila Mkenya ipatikane. Kama nilivyosema, ni tatizo ambalo limekuwa kwa siku nyingi sana, hasa katika sehemu ya Pwani. Tumeona mara kwa mara watu wamepokonywa sehemu zao na Serikali kwa njia za mabavu ama za kulazimishwa na hakuna lolote ambalo linafidiwa. Hufika wakati mtu anapokonywa haki yake akiwa ameshika hati miliki mkononi. Haya tumeyashuhudia na ni mambo ambayo ...
view
4 Jul 2018 in National Assembly:
Ndio, Mhe. Spika wa Muda, nimekubali anifahamishe mahali ambapo ameona kwamba nahitaji kufahamika.
view
4 Jul 2018 in National Assembly:
Asante Mhe. Spika wa Muda. Ningependa nifahamishe mwenzangu aangalie vizuri vile Mswada unasema. Hakuna mahali ambapo unasema kwamba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
4 Jul 2018 in National Assembly:
mtu atalazimika, lakini Mswada haujawekwa wazi. Hofu yangu ni kwamba kumewekwa utaratibu wa kusema kwamba ni maswala ya pesa, ardhi, bondi na kadhalika. Moja ya hizi. Ningeomba kwamba, katika hizi kuwe na kufahamika kwamba kutakuwa na maridhiano. Ndilo neno ambalo nataka liwepo hapa, kwa sababu tunapowacha wazi ni kuonyesha kwamba ni mtu atachagua mwenyewe. Lakini inafika wakati kulingana na hali tunavyoiona, wale wahusika wakuu wenye mamlaka au majukumu ya kuendesha haya inafika wakati wanakwenda na maamuzi yale wanayotaka wao. Haya tumeyaona yakifanyika katika nchi yetu. Mtu anakwenda na maamuzi, anasema ni hivi, ilhali kuna namna nyingine ya kusuluhisha swala lile. ...
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Hoja ya nidhamu, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwa kuwa Kiswahili ni lugha ya kitaifa, naomba kisitumike kwa njia isiyo. Ni makosa kutumia lugha ya Kiswahili kwa namna ambayo sivyo na kuiharibu. Asante.
view