7 Jun 2016 in National Assembly:
Kwa kweli, hatuwezi kukataa maendeleo yasifanyike, na tukiwa kama viongonzi tuna kila haki kuhakikisha kwamba tumesaidia nchi hii katika swala nzima la uchumi wetu. Lakini, mambo mengine kama haya yanahitaji maswala mengi kutoka kwetu sisi viongozi. Kwa mfano, tunasema kwamba tutachukua takribani miaka 34 kulipa deni hili na ilhali tuna uhakika KPA ni shirika moja katika nchi hii linaloingiza pesa nyingi sana. La ajabu ni kwamba leo Serikali inajiongezea madeni kama haya, na nina imani kwamba mzigo huu utakuwa wa wananchi. Hili linatendeka ilhali ushuru unaotozwa mizigo katika bandari ni wa juu. Baadaye wanaoleta bidhaa ama kufanya biashara katika nchi ...
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Kama viongozi tunahitaji kujadiliana pakubwa kabla hatujajiweka katika madeni kama haya ambayo mwisho wake kama ninavyosema, yatakuwa mzigo wa mwanachi wa Kenya wa kawaida. Mimi ningependa kusema kwamba kuna miradi mingi ambayo inahitaji kufanyika na ni bora zaidi. Kama hizi pesa zitatumika, zitafungua milango nchini na kuinua uchumi.
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Kama nilivyosema, tunahitaji maendeleo na uchumi uinuke katika nchi hii lakini ninaona Hoja hii ina maswala mengi ambayo tunahitaji kufahamu kupitia kwa Serikali ama kupitia wahusika. Hatuoni haja kama viongozi kupitisha pesa hizi halafu ziwe mzigo kwa wananchi ama kupitisha pesa hizi ilhali kuna sehemu zingine kama nilivyosema kama Lamu zinazohitaji pesa hizi ili miradi ambayo imekwama kama hii iendelee.
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Kwa hivyo, ningeomba Serikali ihakikishe kwamba tumefanya mambo ambayo yatawaridhisha wananchi na kuinua nchi hii ili tuweze kuimarisha chumi wetu. Tusifanye haya kwa sababu ya ubinafsi wa watu ama maslahi ya watu fulani katika nchi hii.
view
7 Jun 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
10 Mar 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii nikiwa mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Ardhi, kuzungumza kuhusu Mswada huu wa swala nzima la ardhi ambalo limeletwa hapa Bungeni. Ningependa kuipongeza Kamati kwa juhudi zake na yale ambayo wameweza kufanya mpaka kufikisha huu Mswada hapa. Utakubaliana nami ya kwamba swala la ardhi nchini ni nyeti na halihitaji kujadiliwa kiufupi ama kwa namna isio sawa. Hivi sasa Wakenya wengi wana hamu kubwa kujua swala hili limekuwa na mwelekeo upi katika nchi yetu ya Kenya. Tukiangazia pakubwa, Wakenya walipigia Katiba kura na wakaweka Tume ya Ardhi ili kutatua na ...
view
10 Mar 2016 in National Assembly:
Bunge linapopitisha masuala kama haya, linatatua matatizo ambayo yapo. Matatizo haya yapo na hayajatatuliwa hususan tukizungumzia Pwani. Mbali na hayo, walikuwa na imani kubwa katika Tume ya Kitaifa ya Ardhi. Mpaka wakati huu, Tume hii bado haijatatua matatizo kwa kisingizio kuwa Wizara ya Ardhi haijawapa mamlaka kamili au inawanyima haki yao ya kufanya kazi. Ikiwa kisingizio hicho kitaendelea kwa namna hii, ina maana kuwa yale malengo ya Wakenya kuipigia Katiba kura yatakuwa hayajapatikana. Tukizingatia muda ambao umepita tangu Wakenya waipigie Katiba kura mpaka leo ambapo Mswada huu umefika Bungeni ili tujadili jinsi tutawasaidia Wakenya kama viongozi na wawakilishi wa kila ...
view
9 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuandamana na wenzangu kuunga mkono huu Mswada ambao uko mbele yetu leo. Jambo muhimu ambalo nataka tujiulize ni kwamba umuhimu wa huu Mswada ni nini katika nchi yetu ya Kenya? Ni yapi ambayo tumeweza kuyafaidi ama tumeyaona katika nchi yetu ya Kenya kuhusiana na Mswada huu?
view
9 Mar 2016 in National Assembly:
Kwa kweli kumekuwa na tatizo kubwa katika suala la umeme katika nchi yetu. Tunajua vizuri kwamba kampuni ya Kenya Power and Lighting Company ndiyo iliyokuwa ikishughulika sana na suala hili na wao ndio washikadao katika suala la kusambaza umeme katika nchi yetu ya Kenya. Wachache ndio walikuwa wakipata huduma hii na wengi hawakuwa wakiipata. Kumekuwa na matatizo makubwa sana kwa sababu ukilinganisha na matumizi, utaona kwamba malipo ya huduma hiyo yako juu. Kutokana na hali hii, kumekuwa na utata mkubwa lakini nimeshukuru pakubwa kwamba jambo hili limeweza kusambazwa kwa njia nyingine kiasi kwamba kumekuwa na mashirika mengine ambayo yanasambaza umeme.
view
9 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuandamana na wenzangu kuunga mkono huu Mswada ambao uko mbele yetu leo. Jambo muhimu ambalo nataka tujiulize ni kwamba umuhimu wa huu Mswada ni nini katika nchi yetu ya Kenya? Ni yapi ambayo tumeweza kuyafaidi ama tumeyaona katika nchi yetu ya Kenya kuhusiana na Mswada huu?
view