Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 371 to 380 of 515.

  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Mzazi anapojifungua mtoto ina maana ya kwamba mtoto yule ameanza maisha yake. Malengo ni kwamba mtoto yule atalewa na mwishowe atahitaji kazi. Tunajua vizuri namna nchi yetu ilivyo. Mheshimiwa aliyeuleta Mswada huu ametambua kwamba kuna dharura ya kuwapatia akina mama wanaofanya kazi muda wa kutosha wanapojifungua ili wajipange namna watakavyowaelekeza watoto hao. Naamini kwamba muda ambao wamepewa ni wa takribani miezi mitatu. Ningependa vilevile akina mama hao, baada ya kupewa miezi hiyo mitatu, kuwe na namna ambayo watakuwa wanasaidika kikamilifu katika kuliangazia suala hili la watoto. Hii ni kwa sababu, utotoni mwa kila mtu ni wakati muhimu sana katika malezi. view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Hivi sasa, vijana wengi wako katika hali ya sintofahamu; hawajitambui ama kujielewa. Vijana hao pengine wametupwa na mama zao ama hawajui wazazi wao. Siku hizi idadi ya vijana ambao hawana kazi imekuwa kubwa zaidi kwa sababu ya tatizo hili ambalo lilianza hapo awali, na kwa sababu ya makosa ambayo hufanyika wakati mtoto anapozaliwa. Kwa hivyo, kuna dharura katika nchi hii ya kuwepo kwa mwongozo kamili wa kujua idadi kamili ya vijana wanaozaliwa, wanaoinuka, wanaosoma na hata wale ambao hawana kazi. Sielewi ni kwa sababu gani nchi hii haina watu wengi. Tukiangazia idadi ya wanaoishi katika nchi hii, ambao wamefikia kiwango ... view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Ningependa kusema kwamba serikali zote za kaunti 47 ni vizuri ziwe na data ya kuonyesha ni vijana wangapi hawana kazi na wanaohitaji kazi na kiwango chao cha masomo, ili nchi hii iwe na mwongozo mwema. view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Itakuwa vyema wakati kila jambo linaanza liwe na utaratibu. Linapoanza na makosa basi hata huko mbele mambo mengi yataenda mrama. Ni dharura kubwa kwa nchi hii kuangazia mwelekeo na mwongozo wa wananchi wake hususan vijana hapa nchini kwa sababu namna inavyoenda ni kwamba wengi wamekosa imani kabisa na nchi yao. Unapata wengine wanafanya mambo ambayo hayastahili, wengine wanajiingiza katika mambo mabaya na tabia ambazo si njema katika jamii. Kwa hivyo, kuna dharura kubwa hapa nchini ya kuweza kuangazia na kuwa na mipangilio kamilifu katika suala hili kwa wananchi na jamii. view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu. Asante. view
  • 10 Sep 2019 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. Pursuant to the provisions of Standing Order No. 42A, I wish to ask the CS for Transport, Infrastructure, Housing, Urban Development and Public Works: view
  • 10 Sep 2019 in National Assembly: (i) What is the status of compensation to persons affected by the acquisition of land for the development of the Lamu Port – South Sudan – Ethiopia - Transport (LAPSSET) Corridor Project in Lamu? view
  • 10 Sep 2019 in National Assembly: (ii) What plans has the Ministry put in place to ensure that the affected persons in Kwasasi Area in Lamu East Constituency are compensated? view
  • 10 Sep 2019 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. view
  • 19 Jun 2019 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni “Lamu East”, na si “Amu”. Kwanza, ningependa kumpongeza Mhe. Osoro kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Kwa kweli suala la barabara ni suala nyeti sana. Tunazungumzia uchumi nzima wa nchi. Kwa masikitiko makubwa, barabara zetu za Kenya… Kwanza, kabla hatujaingia katika suala la namna tutakavyo fundisha vijana wetu wakiwa shule, barabara zetu ni tofauti na za nchi zingine. Kwa hivyo, hata unapomfundisha mtu kuhusu barabara, zile barabara anazofundishwa na zile anaenda kukumbana nazo ni tofauti. Kitu muhimu ni Serikali kupitia wizara ihakikishe kwamba barabara zetu zimejengwa kulingana na mwelekeo na mwongozo unaotakikakana. Utapata mambo ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus