3 Oct 2019 in National Assembly:
Mwisho, ninaamini kuwa kweli watu wengi wanapenda kuenda Saudi Arabia kufanya kazi kwa sababu ya hali ya kiuchumi nchini mwetu.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. Due to the time remaining and it looks like many Members are interested in speaking to this Motion, is it in order for the time to be limited to three minutes, instead of five per Member?
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Asante Naibu Spika wa Muda. Kwanza kabisa, ningependa kuungana na wenzangu kutoa rambirambi zangu za pole kwa familia waliopoteza wapendwa wao.Vile vile, ningependa kumpongeza Mhe. Mishi kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Naibu Spika wa Muda, Waheshimiwa wengi wamezungumza kwa masikitiko makubwa na kwa kuzingatia yaliyojiri kutokana na kisa hiki cha hivi majuzi cha kupoteza ndugu zetu Wakenya katika mkasa wa feri. Vile vile, ni masikitiko makuu kwa Wakenya. Ni majonzi makubwa kwamba, hata baada ya tukio hili, mpaka sasa, hakuna juhudi zozote ambazo zimefanywa kusawazisha hii mahali. Kwa kweli, ni masikitiko makubwa, na ni aibu kwa nchi hii kwa jumla. ...
view
25 Sep 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumpongeza Mheshimiwa kwa kuleta Hoja hii. Tunakubaliana sote kuwa ni Hoja muhimu sana na tunahitaji kuijadili kwa namna yake. Ukweli ni kwamba, mzazi yeyote anayepeleka mtoto shuleni huwa na malengo kwamba mtoto yule amalize shule na baadaye, awe kijana mwenye mwongozo katika ulimwengu wa leo. Lakini kwa masikitiko makubwa, suala hili limeonekana halina mwongozo na utaratibu. Sitaki niilaumu Serikali lakini nataka kuipa changamoto. Hii ni kwa sababu vijana wengi wanaomaliza shule wanapotea katika njia ambazo hazijulikani. Vijana wengi hawana kazi kwa sababu ya tatizo hilo. Kwa maana hiyo, kuna umuhimu mkubwa ...
view
25 Sep 2019 in National Assembly:
Inasikitisha kuona kwamba wengi wa vijana wetu hawana mwongozo katika hali hii. Hawana kazi wala ujuzi na hawajasomea taaluma nyingine. Sio kwa sababu vijana hawataki kufanya hivyo, ni kwa sababu ya utaratibu na mpangilio wa Serikali yetu. Hiyo ndiyo inafanya vijana wakose imani katika jambo hili. Nikizungumzia Eneo Bunge la Lamu, hivi sasa, watu wengi wanafahamu kwamba tuko na Lamu Port-South Sudan-Ethiopia-Transport Corridor Project (LAPSSET). Lakini kwa masikitiko makubwa, jambo ambalo Serikali haijafanya ni kuhakikisha kwamba mradi huu umewasaidia vijana. Zile nafasi 1,000 ambazo ziliahidiwa na Serikali kwa vijana katika LAPSSET, hadi sasa, hazijawekwa bayana. Jambo hili halijafanyika. Kutokana na ...
view
18 Sep 2019 in National Assembly:
Asante. Ningependa kuchukua fursa hii kuunga mkono Mswada huu na vilevile kumpongeza pakubwa Mbunge aliyeuleta hapa kwa sababu suala la ajira ni suala nyeti. Aliyeuleta Mswada huu amelenga masuala ya akina mama wanaofanya kazi, haswa wakati wanapojifungua na namna watakavyopata nafasi ya kupumzika watakapokuwa wakiwalea watoto wao.
view
18 Sep 2019 in National Assembly:
Ukweli ni kwamba Waheshimiwa wengi wanaposimama kuchangia Mswada huu wanazungumzia neno “ajira” kwa ujumla katika nchi hii. Ukweli ni kwamba ile hali ya ajira katika nchi hii ni hali ambayo inahitaji kupewa kipaumbele tunapojadili kuhusu suala hili.
view
18 Sep 2019 in National Assembly:
Mzazi anapojifungua mtoto ina maana ya kwamba mtoto yule ameanza maisha yake. Malengo ni kwamba mtoto yule atalewa na mwishowe atahitaji kazi. Tunajua vizuri namna nchi yetu ilivyo. Mheshimiwa aliyeuleta Mswada huu ametambua kwamba kuna dharura ya kuwapatia akina mama wanaofanya kazi muda wa kutosha wanapojifungua ili wajipange namna watakavyowaelekeza watoto hao. Naamini kwamba muda ambao wamepewa ni wa takribani miezi mitatu. Ningependa vilevile akina mama hao, baada ya kupewa miezi hiyo mitatu, kuwe na namna ambayo watakuwa wanasaidika kikamilifu katika kuliangazia suala hili la watoto. Hii ni kwa sababu, utotoni mwa kila mtu ni wakati muhimu sana katika malezi.
view
18 Sep 2019 in National Assembly:
Hivi sasa, vijana wengi wako katika hali ya sintofahamu; hawajitambui ama kujielewa. Vijana hao pengine wametupwa na mama zao ama hawajui wazazi wao. Siku hizi idadi ya vijana ambao hawana kazi imekuwa kubwa zaidi kwa sababu ya tatizo hili ambalo lilianza hapo awali, na kwa sababu ya makosa ambayo hufanyika wakati mtoto anapozaliwa. Kwa hivyo, kuna dharura katika nchi hii ya kuwepo kwa mwongozo kamili wa kujua idadi kamili ya vijana wanaozaliwa, wanaoinuka, wanaosoma na hata wale ambao hawana kazi. Sielewi ni kwa sababu gani nchi hii haina watu wengi. Tukiangazia idadi ya wanaoishi katika nchi hii, ambao wamefikia kiwango ...
view
18 Sep 2019 in National Assembly:
Ningependa kusema kwamba serikali zote za kaunti 47 ni vizuri ziwe na data ya kuonyesha ni vijana wangapi hawana kazi na wanaohitaji kazi na kiwango chao cha masomo, ili nchi hii iwe na mwongozo mwema.
view