Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 351 to 360 of 458.

  • 13 Feb 2019 in National Assembly: Magavana tunawajua. Sifa za wengi wao zinajulikana. Siyo wote wenye sifa za kupendeza. Udhaifu upo ndani ya baadhi ya ndugu zetu. Kutokana na hali hii ambayo tunajadili sasa hivi, ni vyema kuhakikisha kwamba mwongozo huu umewekwa vikwazo vya kisheria namna inavyotakikana. Hivyo, tutahakikisha kwamba yeyote ambaye ni mhusika katika kaunti ni mhusika wa kuendeleza kaunti. Masuala ya fedha yatadhibitiwa kwa njia ya furaha kubwa. Serikali ya kitaifa yafaa kuhakikisha kwamba imepeana mwongozo kwa serikali za kaunti kuhusu matumizi ya fedha. Tumeshuhudia mara kadhaa matatizo katika kaunti tofauti tofauti. Mimi naona yamesababishwa na hali ambayo haikuwa hapo mbeleni ya kuweka utaratibu ... view
  • 13 Feb 2019 in National Assembly: Ahsante. view
  • 5 Dec 2018 in National Assembly: Athman (Lamu East, JP): Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumpongeza ndugu yetu ambaye ameleta Hoja hii Bungeni. Vile vile, niwapongeze Wabunge ambao wameweza kuchangia Hoja hii. La muhimu kwanza ni lazima kufahamu kama viongozi malengo na umuhimu wa Hoja hii ni nini. Tunaweza kuzungumza na kujadili lakini mwishowe ikawa umuhimu wake usipatikane kwa jamii. view
  • 5 Dec 2018 in National Assembly: Kama tunavyofahamu, ulimwengu wa leo umebadilika kwa namna nyingi sana, ndiposa fikira hii imefika mahali pa kwamba ni muhimu sana kwa Serikali kuhakikisha kwamba wameweza kulitekeleza jambo hili punde tu tutakapolipitisha hapa Bungeni. Leo hii mambo mengi yanavyoendeshwa ulimwenguni kwa ujumla yanatumia mitandao katika kupata zile habari ama kutuma habari zozote zinazohusiana na mambo ya kileo. Lakini kwa masikitiko makubwa katika sehemu nyingi sana katika nchi hii, utapata kwamba mambo kama haya hayapatikani. Utapata sehemu nyingi sana wanatumia zile teknolojia za zamani katika kuwasiliana na mambo mengi sana ama kuweza kufanya zile shughuli zao za kileo. Ukweli ni kwamba sio ... view
  • 5 Dec 2018 in National Assembly: Ningependa kuunga mkono na kuhimiza ya kuwa lifanyiwe haraka jambo hili na litekelezwe kikamilifu. Jambo ambalo singependa lipatikane ni kwamba watashirikishwa waezekaji wa kibinafsi. Kama tutafanya hivyo, basi, itakuwa bado hatujasonga mbele. Leo hii waekezaji wa kibinafsi wanaweza kufanya huduma hii katika sehemu ambazo hamna, lakini tunapolijadili hapa, huwa tunapendekeza Serikali ichukue majukumu haya kwa sababu matatizo yale ambayo tunayahofia sasa hivi, walioko mashinani hawapati huduma hizi. Hata kesho zikifika huduma hizi na ikiwa wameshirikishwa hawa waekezaji wa kibinafsi gharama zitakuwa vile vile. Kwa hivyo, ningependa Serikali iingilie kikamilifu na kuhakikisha wametekeleza huduma hii kwa Wakenya wengi. Asante. view
  • 4 Dec 2018 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka nikubaliane na Kiongozi Wa Wengi Bungeni kwamba hili jambo tayari liko kwenye Katiba yetu. Vile nakubaliana na yule aliyeleta kutaka kurekebisha haya. Ukweli ni kwamba, matatizo juu ya maswala haya yapo. Pesa zinatengwa na Bunge; zina kwenda kwa wizara; kandarasi inatangazwa; anayefanya kandarasi ile inatia sahihi makubaliano ya kandarasi. Lakini ajabu ni kwamba, ikifika wakati wa malipo, linakuja swala lile kwamba hakuna pesa. Si serikali ya kaunti, ama Serikali ya uma. Kuna mkandarasi anadai pesa. Amefanya kazi takriban miaka miwili na alitia sahihi maafikiano na hajalipwa pesa: Anaambiwa hakuna pesa. view
  • 4 Dec 2018 in National Assembly: Kuna mwongozo wa kwamba wakati mkandarasi amefeli kufanya kazi yake, kuna utaratibu wa kujadili swala hili ili kuliweka sawa. Ningependa hata ikiwa ni Serikali kuu ama ile ya kaunti, wakati mkandarasi amefanya kazi ayke, amepeana lile cheti la malipo na ikiwa umepita muda fulani na hajalipwa pesa yake, kuwe na njia ya kuhakikisha kwamba mkandarasi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 4 Dec 2018 in National Assembly: huyu amepewa uwezo wa kulipwa fidia katika swala hilo ama iandaliwe namna ya kuhifadhi kandarasi hiyo. Tatizo hilo lipo na ni lazima Bunge hili liangazie vizuri tatizo hilo kwa sababu wanakandarasi wengi wanateseka kwa kufanya kazi katika kaunti zetu na Serikali kuu. Tunajua kwamba pesa hizi ziko kwenye bajeti na zimepelekwa kwenywe wizara lakini sijui ni njia gani wanaotumia hawa kuhakikisha wamewadhalilisha wanakandarasi hawa. Mwishowe yafaa tutafute mbinu ya kuwasaidia hawa wakandarasi. view
  • 31 Jul 2018 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kulaani kitendo ambacho kilifanyika cha ukosefu wa nidhamu kwa dini zetu ambazo zimetambulika ulimwenguni huu. Ingawaje pengine Mheshimiwa na watu wake wa Garissa watalisamehe jambo hili, nataka ukubaliane na mimi kwamba mhusika mkuu ndiye anapaswa kuchukue nafasi hii ya kuomba msamaha hata si kwa jamii ya Garissa, bali kwa mwenyezi Mungu. Dini zote hizi si za binadamu ni za Mwenyezi Mungu. Hajamkosea binadamu, amemkosea Mwenyezi Mungu. Dini zote zinazotambulika, hususan zile dini ambazo zimepewa vile vitabu ambavyo vinatambulika katika ulimwengu huu, ni za Mwenyezi Mungu. Waislamu ni watu wa amani. ... view
  • 4 Jul 2018 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kuunga mkono Mswada huu ambao uko mbele yetu hapa leo. Nikiamini pakubwa, ni Mswada ambao wakenya wamekuwa wakiusubiri kwa siku nyingi sana. Hakukua na mwongozo kamili katika swala hili nzima ya maswala ya ardhi. Ingawaje mwaka wa 2010 Wakenya walipitisha Katiba, miongoni mwao yalikua ni haya ya kuweka Tume ya Ardhi ili kusawazisha tatizo hili la ardhi. Leo hii tutapata kwamba, Kenya nzima, sana sana Pwani ambako nimetoka kumekua na tatizo kubwa katika swala la ardhi. Matatizo haya yamesababishwa na kutokuwa na mwongozo kamili katika swala hili, kwa namna watu ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus