Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 331 to 340 of 512.

  • 3 Aug 2021 in National Assembly: kwa namna isivyo. Mheshimiwa Mishi ametoa mfano kuwa kuna raslimali ambazo ziko Mombasa zinazotumiwa kwa njia isiyo ya haki. Kwa hivyo, kutokana na hali hii, tume hii ya waqf haiwezikufanya lolote isipokuwa kupitia Bunge hili na kuweza kuweka makaribisho haya kwa usaidizi wa Wabunge ili kuweza kurekebisha na kuendesha utaratibu huu kwa namna yake. Kama nilivyosema, tunao wengi ambao wako tayari kuyafanya haya – kuweka fedha zao na raslimali zao kwenye waqf ili zisaidie jamii. Lakini, inafaa kuwe na muongozo. Hakukuwa na utaratibu au sheria ya kisawasawa. Ndiposa watu wengi walikosa imani ya kufanya jambo kama hili. Ninaamini pakubwa kwamba ... view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii, kuungana na wenzangu kuunga mkono huu Mswada ambao uko mbele yetu kuhusiana na ugavi wa pesa ambazo zinaenda kwa serikali gatuzi. view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: Kwa kweli, Wakenya mwaka 2010 walisimama kidete kuhakikisha kuwa wamepitisha Katiba ambayo itakuwa na serikali gatuzi. Kutokana na hiyo, matarajio ya Wakenya yalikuwa ni mengi sana, miongoni mwao ni kuona kwamba, huduma zimeweza kuwafikia kule mashinani na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: kuhakikisha kwamba usawa umepatikana na wakaweze kufurahia zile huduma ambazo zilikuwa ziwafikie katika sehemu 47 zilizogawanywa nchini. view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: Vile vile, ni jambo muhimu sana na ni jambo linalohitaji kuzingatiwa, kwamba, zile fedha ambazo zinaenda katika serikali gatuzi, ni fedha ambazo zinahitaji kuwahudumia wananchi. Lakini kwa masikitiko makubwa, tumeweza kushuhudia kwa takriban hivi sasa awamu ya pili kuanzia serikali hizi zianze shughuli zake, kwamba kumekuwa na matatizo mengi sana, husasan katika zile hali za uongozi ambao unapatikana katika sehemu hizo. Mbali na maadhimiyo ya Wakenya kutaka serikali za kaunti ziwe zinafanya kazi katika sehemu 47 zilizopo, yale yanayoshuhudiwa hivi sasa yamekuwa ni matatizo mengi sana. Ukweli ni kwamba Wakenya wanahitaji huduma lakini zile shida na mateso yanayoonekana hivi sasa ... view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: ile na anayestahili kupewa kazi ambayo anaweza kuifanya katika sehemu ile haimaanishi kwamba awe ni mtu wako kisiasa. La msingi ni ikiwa anastahili kupata kazi ile, basi ni sawa wale wahusika waweze kuchukua fursa hii kufanya usawa katika kuendeleza mambo kama haya. Kwa hayo machache, ningependa kuhimiza Serikali ya kitaifa kuhakikisha kwamba matatizo haya hayapatikani kwa sababu yanapotokea, shida nyingi ambazo utaziona zinajitokeza katika kaunti, lawama inakuwa nyingi na ule uchumi unaaza kuleta shida katika sehemu zile kwa sababu zile fedha zinapokuwa hazijafika katika sehemu hiyo, ni wengi ambao wanapata matatizo na wanapata shida sana kutokana na hali hiyo. Kwa ... view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Spika. Nataka nichukue fursa hii kuungana na wenzangu ambao wametangulia kuzungumza kwa kupinga na kukataa marekebisho haya. Vile vile, nataka niseme kwamba nchi hii inawashukuru pakubwa Mhe. Raila Odinga na Mhe. Uhuru Kenyatta kwa kunyamazisha fujo iliyokuweko nchini. Miongoni mwa fujo hizo tulikuwa sisi viongozi. Leo hii nchi inashuhudia kwamba hakuna tena makelele na matusi. Tunalolijadili mbele yetu ni suala la uchumi na mazingira ama miundo msingi katika nchi yetu ya Kenya. Tunayajadili haya yote yaliyoko mbele yetu kama Wabunge tuliopewa fursa. Ni mambo mazuri tunapoyaona na kuyasoma lakini yote yanahitaji kutekelezwa baada ya kupitishwa na Bunge. The ... view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Kwa mtazamo wangu, nikiwa kama Mkenya na kiongozi anayeishi katika hii nchi, haya yote yatahitaji fedha ili kuendelezwa. Kwa mfano, iwapo twapanga kuongeza maeneo bunge sabini, ni lazima kuwe na fedha zitakazoendesha maeneo bunge hayo. Vile vile, sote twajua na kufahamu namna uchumi wa nchi hii ulivyo. Mwisho wa haya yote, mimi na wengine tutalazimika kutoa ushuru wa ziada ilhali tunauelewa uchumi ambao tuko nao. Hakuna kiongozi atakayekataa mazuri yaliyoko katika marekebisho haya. Hofu yangu kubwa ninayotaka wakenya waifahamu ni utekelezaji wa haya mazuri tunayoyajadili yatakapopitishwa. Tunavyojua sasa ni kwamba nchi imekumbwa na madeni chungu nzima. Lazima hatua za ziada ... view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Hon. Sharif Athman Ali, MP for Lamu East. On my behalf and my people, I vote no. view
  • 6 May 2021 in National Assembly: I vote No. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus