Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 321 to 330 of 512.

  • 12 Oct 2022 in National Assembly: Mwanzo, ningependa kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kupata nafasi ya kuwa Naibu wa Spika. Tunajua wewe ni mtendakazi. Tunajua kazi yako ni nzuri na tayari ishaanza kuonekana. Kusema kweli, kiangazi kinawatatiza sana watu wetu; haswa, watu wangu wa Lamu Mashariki. Kiangazi kimewaathiri watu wa Kiunga na watu wa Eneo Wodi ya Faza. Ningeomba Wabunge ama viongozi wa taifa letu wasichukulie hili janga la kiangazi kama janga la watu fulani tu maana linaathiri watu kutoka nyanja zote. Mfugaji akipata hasara kwa minajili ya ng’ombe wake kufa, hatakuwa na kitu cha kuuza ili apate faida ili imuwezeshe kupata hela za kununua mazao. ... view
  • 12 Oct 2022 in National Assembly: Nasi pia sasa tumekuwa kwa janga hilo la ukame ilhali tulikuwa tumejipanga. Kwa hivyo, nataka kuwaambia majirani zetu wa Garissa, Tana River na wale wote wanaoleta ng’ombe – hata wanaowabeba kwa malori wakiwaleta – wajue siku ile mimi napigania mabwawa na vitu vingine kupelekwa Lamu wao huwa wako mbele kupigania Lamu isipate mabwawa hayo ili wapate wao. Lakini saa hii tumeona kwamba yale mabwawa machache ya Lamu ndiyo wanayoyafuata. Kwa hivyo, Mhe. Naibu wa Spika, mimi ningeomba Serikali iweze kuangalia yale maeneo ambayo yatakuwa yakiwafaa wengine. Pesa zilitolewa yakajengwa mabwawa lakini mvua haikunyesha kule. Mvua imenyesha mahali kama Lamu, na ... view
  • 12 Oct 2022 in National Assembly: Kwa hivyo, nyinyi mnaoniangalia vizuri, tena watu wangu majirani wa Garissa, mhakikishe, maanake nyinyi ndio wa kwanza, tukipata hivyo vidimbwi vinavuta Garissa zaidi kuliko Lamu. Na hivyo ndivyo vitu vinawafaa. Saa hii watu wangu wanatatizika. Changamoto za usalama zinaongezeka kwa sababu ng’ombe na wafugaji ni wengi kwenye misitu, na katika misitu kama Boni kuna matatizo. Kwa hivyo, mnanipatia kazi ngumu mno. Kwa sasa hivi ni wakati mgumu kwa watu wa Lamu, haswa watu wa Kiunga. Kule kwenyewe kuna shida za kiusalama ilhali watu na mifugo wanakuja kwa wingi kudhoofisha usalama zaidi. Kwa hivyo, wakati mwingine mnapopanga jambo lolote kama jambo ... view
  • 18 May 2022 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naungana na wenzangu kupongeza Kamati husika kwa kuja na Ripoti hii. Kwa kweli, utakubaliana na mimi kwamba suala la afya ni nyeti na muhimu sana. Nawashukuru kwa kuwa wamelizingatia kikamilifu na kuliwekea mikakati. Mengi yamezungumzwa na wenzangu kuhusiana na suala hili. Masikitiko makubwa ni kwamba ni kweli sisi Waheshimiwa tuko na zile kadi za bima ya afya. Lakini, utapata kwamba unapopatikana na matatizo ukiwa hapa Bunge ama sehemu nyingineyo, huna budi kukimbilia hospitali kujiangalia afya. Kuna mambo mengine ambayo unapaswa kupitia hata kabla hujafika hospitali. Tukiwa hapa Bunge, Waheshimiwa huwa na kazi nyingi katika ... view
  • 18 May 2022 in National Assembly: Katika sehemu nyingi za nchi hii na kaunti zetu, utapata watu ni wagonjwa lakini hawawezi kufikia zile huduma za kujua magonjwa yao. Ndiposa utapata mtu amekaa na mara presha imepanda ila hajui alikuwa nayo; mtu amekaa, amepatikana na matatizo haya na hajui. Kwa hivyo, itakuwa vyema ikiwa Kamati itaangalia haya mambo zaidi na kuhakikisha kuwa kaunti zetu ziko na huduma za madaktari wa kutembea kama wale wanaopeana chanjo kwa watoto wadogo. Ukifanya utafiti wako, nchi hii yetu iko na watu wengi wanaoathirika na madhara ya afya ilhali hawajui. Itakuwa bora tukipata serikali yenye mipangilio ya kuenda mashinani kuangalia afya za ... view
  • 1 Dec 2021 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika. Ningependa kuchukua fursa hii kuungana na wenzangu kumshukuru Mhe. Rais na kumpongeza pakubwa kwa Hotuba yake hapo jana katika Bunge hili. Ni dhahiri shahiri kuwa mengi yaliyozungumzwa na Mhe. Rais ni mambo ambayo yameonekana na Wakenya. Jambo moja kubwa ambalo lilishuhudiwa na Wakenya katika Bunge lililopita nikikumbuka vyema ni kuwa katika shughuli kama hii ya Hotuba ya Rais, Bunge lilikuwa na taharuki kubwa na bughudha nyingi sana kutokana na hali za kisiasa. Ukweli ni kwamba, jana kulishuhudiwa utulivu uliotokana na ushirikiano mwema kati ya Mhe. Rais Uhuru Kenyatta na wapinzani wake. Hata hivyo, ningependa kumwambia Mhe. Rais ... view
  • 1 Dec 2021 in National Assembly: Ningependa kumwambia Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta kuwa, mbali na kuona miradi mingi ya barabara ikifanyika, katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki, hakuna hata kilomita moja ya lami. Nimeweza kulileta jambo hili mara kadhaa katika Bunge hili na kuliwasilisha kwa wahusika wakuu. Kama viongozi kutoka Lamu, tumeshuhudia ujenzi wa LAPSSET. Ni matarajio makubwa kuwa kutokana na malengo ya ujenzi wa poti ile, Serikali hii na Rais watawapea kipao mbele vijana wetu wa Lamu katika nafasi zitakazopatikana mahali pale. Hayo ndiyo mambo ambayo yanafaa kuwa na mwongozo mwema katika Serikali hii tunayo. Tatizo kubwa ambalo liko na yafaa tulizingatie ni kuwa katika ... view
  • 24 Nov 2021 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nami naungana na wenzangu kuchangia marekebisho haya huku nikimpongeza Mhe. Barasa kwa kuleta haya Bungeni. Nataka kwanza tujiulize ikiwa haya tunayojadili hapa Bungeni leo ni ya sheria ambayo tayari iko katika nchi hii ama haiko. Ukweli ni kwamba hii ni sheria tayari ipo lakini imemlazimu Mhe. Barasa kuiregesha Bungeni kwa sababu ya marekebisho. Nataka tujiulize kwa nini imelazimu irudi Bungeni kwa sababu ya marekebisho. Hali halisi ni kwamba sheria hii inawagandamiza na kuwadhulumu Wakenya sana. Wengi wameenda mbele za haki bila kupata hizi haki zao. Unapokuwa mfanyikazi na kila mwisho wa mwezi unakatiwa pesa ... view
  • 24 Nov 2021 in National Assembly: nyumbani, wafaa kuambiwa pesa zako ziko benki uende ukachukue. Ndiyo ujue utazifanyia nini. Sioni sababu hata moja ya pesa hizi kukaa katika sehemu ambazo zipo kwa muda wote huo, kama miaka mitano au sita au saba, baada ya mtu kustaafu. Baada ya hizo siku zote, pesa hizo zinazalisha riba katika benki. Lakini mtu yule hapewi! Wanaochukua riba ni watu wenngine Serikalini. Ndiposa utapata matatizo makubwa katika idara hizi. Kuna masuala mengi. Wengi wanapatikana na makossa ya ulaghai na ufisadi katika idara hizi kwa sababu wamezuia haki za watu wakidhania labda ni haki zao. Kwa hivyo, la usawa katika kurekebisha haya ... view
  • 3 Aug 2021 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kupata fursa hii kuchangia Mswada huu wa waqf. Wengi wamezungumzia suala hili la waqf . Ningependa kueleza kwamba ni vyema kwanza tufahamu maana ya waqf ndiposa tupate yale maelezo kamili, ingawaje Mhe. Duale ametueleza. Waqf imekuweko katika nchi hii na imekuwa ikitambulika na nchi hii. Ni muongozo umekuwa ukitembea ama ukiendelezwa na Waislamu. Hivi sasa Mswada huu umefika hapa bungeni kwa marekebisho zaidi. Hii ni dalili kuonyesha kwamba umechukua mkondo wa sheria ya nchi hii inavyotakikana. Lakini, ni vyema vilevile tufahamu ya kwamba utaratibu na muongozo ambao unatakikana hususan katika suala hili, tukiwa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus