15 Mar 2023 in National Assembly:
that there are Cabinet Secretaries who were rejected by Committees and were approved by this House.
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja hii. Ripoti hii imezungumzia stakabadhi za Umra, ambazo zote zilikuwa sahihi na halali. Hii ni kwa sababu Umra alipitishwa na IEBC mwezi wa Mei, na stakabadhi zake zote zilikuwa sawa. Haikuwa imepita mwaka, kwani alikuwa amepigania kiti cha ugavana kule Lamu. IEBC ni shirika la Serikali. Itakuwaje IEBC wampitishe halafu Bunge liseme halimpitishi?
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Who gave him the permission to inform
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, Umrah ana tajriba ya mambo ya mazingira. Hayo ndiyo mambo yake. Ana shirika linaloitwa Safari Doctor, shirika ambalo limekuwa Lamu na limetusaidia sana mpaka likapewa tuzo na United Nations (UN) katika mambo haya. Leo, nashangaa ninapoambiwa kwamba Umrah hana tajriba. Umrah ndiye mtu anayeweza kututetea tupate fedha kutoka kwa donors ili zitusaidie kwa mambo ya mazingira. Rekodi zinaonyesha Umrah alishindana na nchi nyingine kwa mambo haya, akashinda kama Mkenya, na akapewa tuzo ya UN. Inasikitisha sana. Au ni kwa sababu yeye ni Mbajuni? Hizi shida ambazo tunapata ni nyingi. Mambo haya yamefanywa kana kwamba hawakuwa wanataka ...
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Hivi juzi tu, wamefanya mambo ya forest rangers . Sisi watu wa Lamu East tukapewa
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
watano na watu wengine wamepewa arobaini. Ni mambo haya yanatumika kukandamiza Mbajuni. Kwani sisi hatuna haki? Huyu Umrah ni mmoja tu! Tumepitisha watu wangapi hapa? Mbajuni mmoja ndio mmeona lazima mumkandamize? Si haki! Kamati haiko sawa. Haifai inavyofanya. Nionyesheni document moja ya Umrah ambayo haiko sawa. Mwanzo, alipokwenda Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) aliambiwa hizi
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
ndio zinafaa; apeleke hili na lile. Hii ndio maana alitoa mfano kuwa ukienda kuomba passport, utaambiwa uandike reason . Ukiandika sababu ni kuwa unaenda Tanzania, kisha uende huko na uitwe uende taifa lingine, utatumia passport hiyo hiyo. Kama alipitishwa na IEBC, kwa nini hawezi kupitishwa na Bunge na mwaka haujaisha? Documents zote ambazo sisi tulipeana kama wagombea viti bado hazija expire . Wana sababu zao hawa! Hawamtaki tu Umrah. Ninawaambia wanafanya makosa. Waangalie shirika la Safari Doctor na waulize
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
ya Umrah. Nawaambia, Umrah ndiye expert kwa mambo haya. Umrah amevuta pesa nyingi kutoka serikali za nje kuleta huku Kenya, mpaka akapewa tuzo ya UN. Itakuwaje apewe tuzo ya UN kisha hapa sisi tunamkataa? Hiyo ni dhuluma kwa Wabajuni, na haifai. Si sawa. Sisi pia ni Wakenya na tunalipa tax . Mtu mmoja wa Kibajuni katika hawa appointees ndio nyinyi hamumtaki? Imewaingia jichoni. It is not fair!
view
14 Mar 2023 in National Assembly:
Asante Bwana Spika, kwa kunipa nafasi ya kutoa rambirambi zangu kwa niaba yangu, watu wangu wa Lamu East, na familia yangu, kwa familia ya Grace Onyango. Kwa kweli, Bi. Grace alikuwa mfano mwema. Mwanzo, ningependa kumpongeza Mbunge wa kiume ambaye ni rafiki wa wanawake. Inaonyesha kuwa kuna wanaume ambao ni marafiki wa wanawake. Lakini kuna wale ambao ni maadui wa wanawake ilhali hawawezi kukaa bila wanawake. Wakija hapa, wanaanza kutupiga. Hawawezi kukaa bila wanawake lakini wanapinga affirmative action . Tunavyo hivi viti 47 mkononi. Wanaume, msijisumbue kuvitoa. Hatuwezi kuwachilia kile tunacho ili tutafute kingine. Tumeona umuhimu wa affirmative action seats ...
view
7 Mar 2023 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia ombi lililotumwa kuhusu watu kupotea kiholela. Sisi, katika Lamu Kaunti, tumeathirika sana. Tukitaja watu wetu waliopotea na hatujui wako wapi mpaka sasa, orodha ni ndefu. Tulifikiria ni masuala ya Al Shabaab kwa vile tuko mpakani lakini la kusikitisha na kuchanganya watu zaidi ni kuwa hivi karibuni tuliambiwa mauaji ya Lamu Kaunti hayahusiani na Al Shabaab bali ni mambo ya mashamba. Watu ninaowasimamia sasa wanatatizika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view