Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 281 to 290 of 512.

  • 26 Apr 2023 in National Assembly: Pia, kuna rufaa nyingine ya lazima, ambayo ni kifo. Msiisahau hiyo. Hilo ni tatizo maanake kifo kinasikitisha. Executive Order ilitolewa kusema kuwa mgonjwa akifariki hospitalini, maiti isizuiliwe. Lakini utaona tunaitwa kama Wabunge kuchangia mambo haya. Inakuwa procedure ndefu mpaka watu wanaambiwa watafute title deeds na vitu vingine. Mgonjwa anapofariki, ashapata rufaa ya lazima. Hakuna haja ya kuweka maiti pale. Hospitali ni ya umma kisha unazuilia maiti hiyo mpaka watu wao wafanye Harambee na michango ili walipe. Mtilie maanani rufaa hiyo ya lazima katika sheria hiyo. view
  • 26 Apr 2023 in National Assembly: Mhe. Spika wa Muda, nina mengi ya kuzungumza lakini naona wenzangu pia wako na hamu ya kuzungumza. Kwa hivyo, nitawachia hapo. Ahsante. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi kuwakaribisha watoto wangu wa Tchundwa Primary School kutoka Lamu East, Faza Ward. Wametoka mbali. Walitoka saa tisa asubuhi ili wapate boti, maji iwaruhusu wafike Mokowe. Ili wafike Nairobi, wameondoka huko saa tatu na kufika saa tisa usiku. Nachukua nafasi hii niwaombe watoto wangu wasome. Tumewaleta hapa musome na muangalie dunia ilivyo Nairobi. Watu wamesoma. Kusoma ni muhimu. Musome ili kule kwetu kujengwe kuwe kama Nairobi. Sisi tumesoma na tunaambiwa tujipange ama tutapangwa. Masomo ndio view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Mmeingia Kenyatta International Convention Centre (KICC), mumeenda Nairobi School, na pia kule tumeambiwa tujihadhari kabla ya hatari. Kwa hivyo, sisi tuna mambo mengi. Hatari iko karibu na sisi. Kwa hivyo, naona mutakayoyasoma hapa muende mukafanye bidii ili pia nyinyi mchukue nafasi hizi. Muje mfanye kazi Nairobi. Sio kwamba wengine waandikwe kazi lakini sisi Wabajuni tuwachwe nyuma. Karibuni sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Ahsante Bi. Naibu Speaker. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu wa Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Kusema kweli, hii kupimiwa kwa barabara, inaleta adhari nyingi sana. Sisi tunayapitia mambo haya Lamu. Imekuwa ni kama ya kawaida. Nimeshangaa kwa sababu nilifikiri ni Lamu peke yake ambayo inapata shida kama hizi. Ikifika saa kumi na mbili Lamu, barabara na Kaunti nzima inafungwa na hakuna ruhusa ya kutoka nje. Kukiwa na mambo ya dharura, ni gari la wagonjwa pekee ambalo linatoka. Katika sehemu zingine nilipatana na Special Force wakanisomea kama mtoto mdogo. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Katika barabara ya kwenda Kiunga, hakuna gari linapita. Kukiwa na jambo la dharura Kiunga, lazima utumie bahari, ambayo saa zingine ina mawimbi makali. Watu wengi wamepata ajali nyingi. Naunga mkono huyu Mheshimiwa. Maombi yake yafuatiliziwe na pia katika sehemu zingine. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Ilipotokea COVID-19, Wakenya walipata amri za kutotoka nje. Sisi tulikuwa tumezoea kwetu. Kwetu Lamu, mara kuna amri ya kutotoka ya wavuvi ama barabara ambayo haipitwi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Hii inatuadhiri sana kiuchumi. Naomba maombi haya yaangaliwe na Kamati vizuri, na ihakikishe jambo hili limerekebishwa. Pia, hizo baraka zisonge kwetu. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu wa Spika view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus