21 Feb 2023 in National Assembly:
Kwa hivyo, nawasihi wenzangu hapa kuna kazi. Nilazima tufikirie kama viongozi ili tupate suluhisho. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda.
view
30 Nov 2022 in National Assembly:
Ahsante, Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia swala hili la janga la ukatili wa kijinsia. Kwa hakika, tunajua kuwa janga hili lipo na limekuwa donda sugu. Watu wengi wamepitia shida hizi na Serikali imetumia njia nyingi kujaribu kupigana na janga hili lakini bado hatujafikia pale tunapotakikana kuwa. Kila kituo cha polisi kinapaswa kiwe na kitengo ambacho kinahudumia mambo ya kijinsia lakini hadi sasa, vitengo hivi havijakuwa na nguvu za kusaidia zaidi. Wamejaribu lakini tunaomba wapewe nguvu zaidi ili tuwe na polisi wa kike watakaokuwa kwenye vitengo hivi ili wasaidie akina mama ambao wanakumbwa na shida hizi za ukatili ...
view
17 Nov 2022 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi. Moja kwa moja ningependa kupongeza wote tisa waliochaguliwa. Ninawapongeza sana Mhe. Shahbal, Omar na wengine wote. Hapa usawa umefanyika. Vyama vimewakilishwa vizuri, hata walemavu wamewakilishwa kwa hivyo sasa ni wakati wao wa kufanya kazi. Nilikuwa Mwenyekiti wa Regional Integration Committee Bunge lililopita. Nilikuwa nawaomba sana wale waliochaguliwa, ndugu zetu mliochaguliwa, wakienda wajue kuna kazi nyingi. Jumuiya hii iko na taasisi karibu kumi. Katika taasisi hizi kuna mambo mengi ambayo wanafaa kwenda kuyafanya. Taasisi ya kwanza ni Community Civil Aviation Safety and Security Oversight Agency (CASSOA), East African Community Competition Authority (EACA), East African ...
view
15 Nov 2022 in National Assembly:
Hon. Temporary Speaker, thank you for giving me this opportunity to ask the Cabinet Secretary for Roads, Transport and Public Works the following Question: (i) Could the Cabinet Secretary outline the Government policy measures being undertaken to develop marine transport in the country, and particularly in Lamu County? (ii) What immediate plans has the Ministry put in place to provide modern marine transport facilities such as ferries, among others, to Lamu residents and tourists? (iii) What policy measures are in place to facilitate private enterprises to develop marine transport facilities in the country, and in Lamu County in particular?
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Hon. Deputy Speaker, I already have the microphone.
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Asante Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia Mswada huu muhimu wa ukame kuwa janga la kitaifa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Mwanzo, ningependa kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kupata nafasi ya kuwa Naibu wa Spika. Tunajua wewe ni mtendakazi. Tunajua kazi yako ni nzuri na tayari ishaanza kuonekana. Kusema kweli, kiangazi kinawatatiza sana watu wetu; haswa, watu wangu wa Lamu Mashariki. Kiangazi kimewaathiri watu wa Kiunga na watu wa Eneo Wodi ya Faza. Ningeomba Wabunge ama viongozi wa taifa letu wasichukulie hili janga la kiangazi kama janga la watu fulani tu maana linaathiri watu kutoka nyanja zote. Mfugaji akipata hasara kwa minajili ya ng’ombe wake kufa, hatakuwa na kitu cha kuuza ili apate faida ili imuwezeshe kupata hela za kununua mazao. ...
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Nasi pia sasa tumekuwa kwa janga hilo la ukame ilhali tulikuwa tumejipanga. Kwa hivyo, nataka kuwaambia majirani zetu wa Garissa, Tana River na wale wote wanaoleta ng’ombe – hata wanaowabeba kwa malori wakiwaleta – wajue siku ile mimi napigania mabwawa na vitu vingine kupelekwa Lamu wao huwa wako mbele kupigania Lamu isipate mabwawa hayo ili wapate wao. Lakini saa hii tumeona kwamba yale mabwawa machache ya Lamu ndiyo wanayoyafuata. Kwa hivyo, Mhe. Naibu wa Spika, mimi ningeomba Serikali iweze kuangalia yale maeneo ambayo yatakuwa yakiwafaa wengine. Pesa zilitolewa yakajengwa mabwawa lakini mvua haikunyesha kule. Mvua imenyesha mahali kama Lamu, na ...
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Kwa hivyo, nyinyi mnaoniangalia vizuri, tena watu wangu majirani wa Garissa, mhakikishe, maanake nyinyi ndio wa kwanza, tukipata hivyo vidimbwi vinavuta Garissa zaidi kuliko Lamu. Na hivyo ndivyo vitu vinawafaa. Saa hii watu wangu wanatatizika. Changamoto za usalama zinaongezeka kwa sababu ng’ombe na wafugaji ni wengi kwenye misitu, na katika misitu kama Boni kuna matatizo. Kwa hivyo, mnanipatia kazi ngumu mno. Kwa sasa hivi ni wakati mgumu kwa watu wa Lamu, haswa watu wa Kiunga. Kule kwenyewe kuna shida za kiusalama ilhali watu na mifugo wanakuja kwa wingi kudhoofisha usalama zaidi. Kwa hivyo, wakati mwingine mnapopanga jambo lolote kama jambo ...
view
18 May 2022 in National Assembly:
Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naungana na wenzangu kupongeza Kamati husika kwa kuja na Ripoti hii. Kwa kweli, utakubaliana na mimi kwamba suala la afya ni nyeti na muhimu sana. Nawashukuru kwa kuwa wamelizingatia kikamilifu na kuliwekea mikakati. Mengi yamezungumzwa na wenzangu kuhusiana na suala hili. Masikitiko makubwa ni kwamba ni kweli sisi Waheshimiwa tuko na zile kadi za bima ya afya. Lakini, utapata kwamba unapopatikana na matatizo ukiwa hapa Bunge ama sehemu nyingineyo, huna budi kukimbilia hospitali kujiangalia afya. Kuna mambo mengine ambayo unapaswa kupitia hata kabla hujafika hospitali. Tukiwa hapa Bunge, Waheshimiwa huwa na kazi nyingi katika ...
view