5 Jul 2023 in National Assembly:
Inaitwa Mkokoni mji wa wangwana.
view
21 Jun 2023 in National Assembly:
Asante Bw. Spika wa Muda. Hii pesa ya usawazishaji, kutoka kwa jina lenyewe, inaonyesha ni kusawazisha. Lakini vile mambo yashatokea, afadhali nusu shari kuliko shari kamili.
view
21 Jun 2023 in National Assembly:
Ni muhimu hii pesa ije hata kama ni kidogo. Bora tuipate itumike vizuri. Hii pesa muda wake usije ukaisha kabla haijatumika. Sisi miradi yetu ikija kule iwe ni miradi itakumbukwa na hata vizazi vijavyo. Kuna sehemu nyingine kama vile Lamu Mashariki ambayo ilipata pesa hii ya usawazishaji. Pesa ilikuwa ya kujenga barabara lakini hiyo barabara tukiitafuta leo haiko. Zaidi ya Ksh1 milioni zilitumika. Tunaomba pesa hii itumike vizuri. Haki pia itendeke. Kila Wadi ipate haki yake. Isiwe wadi nyingine kama Basuba Ward inaambiwa kuna mambo ya usalama basi siku zote haifanyiwi miradi kwa sababu ya mambo ya usalama. Ikiwa hivyo, ...
view
2 May 2023 in National Assembly:
Asante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili nichangie hii Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha. Katika hii Ripoti, nimeona Lamu Mashariki haiko lakini Lamu Magharibi iko. Nina masikitiko kwani naona kuna matatizo mengi na fedha hizi huwa ni za kusaidia wanyonge kule. Wale ambao hawajiwezi hata haziwasaidii. Fedha hizi zikiwa haziangaliwi vizuri, wale wanyonge wanazidi kuwa wanyonge. Mimi naunga mkono hii Ripoti kama Mkaguzi Mkuu alivyosema. Nimeshangazwa sana kama Kaunti ya Lamu. Upande wa Lamu Magharibi umefanyiwa ukaguzi na Lamu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of ...
view
2 May 2023 in National Assembly:
Mashariki haujafanyiwa. Imekuwa shida kwetu kwani Lamu Mashariki imekuwa nyuma sana kwa miaka mingi kwa sababu hawa wakaguzi wakienda wanaambiwa kule kuna Al Shabaab, bahari chafu na huwa hakuna bahari chafu wala Al Shabaab. Huwa ni kigezo tu cha kuwafanya wasiende kukagua. Na wakiendelea hivyo huwa wanaleta shida. Shida ni kama sasa hivi mimi nimeingia nikifika kwangu kazi ni nyingi za kufanywa na pesa nayo iko lakini nikiangalia zile kazi nilizonazo kama zingefanywa nyuma ingekuwa rahisi kwangu. Kwa mfano, saa hii wanaambiwa upande wa NG-CDF wapande miti. Miti hiyo itapandwa vipi na sasa shule zote za Lamu Mashariki hazina kuta, ...
view
2 May 2023 in National Assembly:
wakaribishwe kule wakague. Lakini pia matatizo yale pia yasionekane ni ya sasa hivi. Uzuri utajulikana ni akina nani ndio waliofanya makosa katika miaka iliyopita. Hao wakija kule watasaidia maanake kuna matatizo ambapo saa zingine bursary inatumika kisiasa, saa zingine bursary haiendi kwa watarajiwa, na saa zingine kuna shule ambazo kuna wakora ambapo inakubidi ukague pesa ya bursary moja kwa moja mpaka ukosane na walimu. Kama hufanyi hivyo, imekuwa ni kama biashara. Ninataka huyo Auditor-General kwa hii Ripoti yake pia ahakikishe amekagua vizuri hizi shule. Shule pia zina matatizo mengi. Kwa hii NG-CDF, tulipoingia, wale walio na wadi tatu wamepunguziwa. Ni ...
view
2 May 2023 in National Assembly:
visiwa, inakuwa ngumu kutengeneza kwa sababu gharama ziko juu sana. Wengine pia hutumia gharama kama hizo kuiba na inakuwa juu kushinda huku. Shukran, Mhe. Spika wa Muda.
view
26 Apr 2023 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Mswada huu. Mwanzo, ningependa kumpongeza ndugu yangu, Mhe. Barasa. Ninaiunga mkono sheria hii. Ninaomba sheria hii iwe rahisi kutumika, na isiwe sheria ngumu ya kuwatatiza The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
26 Apr 2023 in National Assembly:
wagonjwa. Ukitengeneza sheria, huwa inapelekwa kwa Kamati, mnajadiliana, Wabunge wanahusishwa, na hata sisi tukitaka, tunaweza kuja huko kama marafiki wa hiyo Kamati maanake haya ni mambo yanayotuhusu na yanatutatiza kila wakati. Ningependa wagonjwa wapewe uhuru wa kwenda popote wanapotaka kutibiwa katika sheria hiyo. Kumekuwa na mtindo ambapo mgonjwa anapotaka kwenda matibabu India, anazungushwa tu. Madaktari wanamwambia aende kwa Kenya Medical PractitionersPharmacists and Dentists Union (KMPDU) ili ombi lake litiliwe sahihi. Akifika kule, wanamwambia hawawezi kutia sahihi na atafute daktari amtilie sahihi. Akienda kwa daktari, daktari anamwambia kuwa hawezi kutia sahihi kwa sababu huduma hiyo inafanyika Kenya. Hata kama huduma hiyo ...
view
26 Apr 2023 in National Assembly:
Itabidi sisi kama Bunge tujipange, na pia Ministry ijipange, kuwe na hospitali za rufaa katika kila eneo. Maanake hapa Kenya, kuna hospitali sita kubwa za Level 6. Lakini hizi Level6 hospitals zinapatikana katika eneo moja. Coast nzima hakuna Level 6 hospital hata moja. Kisha bado watu huku wanazungumzia ‘ one man, one vote, one shilling’ . Hospitali hizi zinafaa ziwe karibu na wagonjwa. Mtu anatoka Lamu kuja KNH kwa sababu hiyo ndiyo Level 6 hospital ambayo iko karibu naye. Kutoka Kiunga kufika Nairobi ni gharama ya juu. Watu wanakufa kwa sababu ya kukosa uwezo wa kufika KNH. Hospitali yetu ya ...
view