Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 251 to 260 of 458.

  • 15 Mar 2023 in National Assembly: ya Umrah. Nawaambia, Umrah ndiye expert kwa mambo haya. Umrah amevuta pesa nyingi kutoka serikali za nje kuleta huku Kenya, mpaka akapewa tuzo ya UN. Itakuwaje apewe tuzo ya UN kisha hapa sisi tunamkataa? Hiyo ni dhuluma kwa Wabajuni, na haifai. Si sawa. Sisi pia ni Wakenya na tunalipa tax . Mtu mmoja wa Kibajuni katika hawa appointees ndio nyinyi hamumtaki? Imewaingia jichoni. It is not fair! view
  • 14 Mar 2023 in National Assembly: Asante Bwana Spika, kwa kunipa nafasi ya kutoa rambirambi zangu kwa niaba yangu, watu wangu wa Lamu East, na familia yangu, kwa familia ya Grace Onyango. Kwa kweli, Bi. Grace alikuwa mfano mwema. Mwanzo, ningependa kumpongeza Mbunge wa kiume ambaye ni rafiki wa wanawake. Inaonyesha kuwa kuna wanaume ambao ni marafiki wa wanawake. Lakini kuna wale ambao ni maadui wa wanawake ilhali hawawezi kukaa bila wanawake. Wakija hapa, wanaanza kutupiga. Hawawezi kukaa bila wanawake lakini wanapinga affirmative action . Tunavyo hivi viti 47 mkononi. Wanaume, msijisumbue kuvitoa. Hatuwezi kuwachilia kile tunacho ili tutafute kingine. Tumeona umuhimu wa affirmative action seats ... view
  • 7 Mar 2023 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia ombi lililotumwa kuhusu watu kupotea kiholela. Sisi, katika Lamu Kaunti, tumeathirika sana. Tukitaja watu wetu waliopotea na hatujui wako wapi mpaka sasa, orodha ni ndefu. Tulifikiria ni masuala ya Al Shabaab kwa vile tuko mpakani lakini la kusikitisha na kuchanganya watu zaidi ni kuwa hivi karibuni tuliambiwa mauaji ya Lamu Kaunti hayahusiani na Al Shabaab bali ni mambo ya mashamba. Watu ninaowasimamia sasa wanatatizika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 7 Mar 2023 in National Assembly: Hawajui wanaowaua ni nani? Kwa nini watu wetu wakimbie na wateswe kwa sababu ya AlShabaab na kumbe kuna kiongozi anayejua wanavyouawa? Nimefurahia hili ombi. Hata mimi itabidi niifanye iwe kauli au dua ili Serikali ituambie ni nani anawaua watu Lamu. Hilo ni jambo ambalo limetatiza watu sana. Siku nyingi tumekuwa tukifikiri ni Al Shabaab kumbe siyo wao bali ni mambo ya ardhi. Aliyoyasema Kiongozi wa Wengi Bungeni, inamaanisha anawajua wanaowaua watu huko Lamu Kaunti. Na itakuwa vizuri kuwataja kwa sababu imetutatiza sana. Kule, tunategemea utalii. Watalii sasa hawakuji maana kuna askari wengi na msafara wa magari mengi. Wakikuja kama watalii ... view
  • 7 Mar 2023 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu Spika. Swali hili limengojewa sana, mpaka wenyewe wamekuja hapa. Dadangu ambaye ni rafiki yangu, Thweba, amekuja kuona vile nitauliza Swali hili kwa sababu wao wanaathiriwa sana. view
  • 7 Mar 2023 in National Assembly: Hon. Deputy Speaker, I rise to ask the Cabinet Secretary for Information, Communication and the Digital Economy the following Question: (a) Could the Cabinet Secretary explain why the people of Siu, Shanga and Mkokoni in Lamu East Constituency are suffering from digital exclusion by not being connected to the mobile phone network? (b) Could the Cabinet Secretary further explain why the entire Lamu East Constituency is still served by 2G Network when the rest of the country is on 4G Network and is soon transitioning to 5G Network? (c) What plans does the Ministry have to ensure that Siu, Shanga ... view
  • 7 Mar 2023 in National Assembly: Thank you, Hon. Deputy Speaker. view
  • 21 Feb 2023 in National Assembly: Asante, Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi nichangie jambo hili la masomo ya CBC . Jambo lolote jipya hupata upinzani. Kwa hakika, CBC iko na mapungufu mengi – mapungufu ya upande wa walimu, upande wa wazazi, na kwa majengo kwenye junior secondary school. Tena mapungufu yamezidi kwenye maeneo Bunge mengine. Maeneo Bunge kama Lamu ni visiwa. Hata kama kina wanafunzi wachache, kisiwa ni lazima kiwe na shule na walimu. Ukisema unawatoa wanafunzi kwa kisiwa kizima uwapeleke kwingine, ni shida kwa sababu usafiri ni taabu. Walioanzisha CBC hawakuzifikiria sehemu nyingine. Hatusemi CBC ni mbaya, lakini kuna sehemu haiwezekani. CBC ina uzuri ... view
  • 21 Feb 2023 in National Assembly: Haya mahangaiko tuliyonayo sasa pia yatarudi vile vile. Ikiwa itawezekana, tushirikiane tuweke Bajeti tuongezee walimu wapatikane zaidi. Kama alivyosema Mbunge The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 21 Feb 2023 in National Assembly: mwenzangu, Mhe. Nyikal, saa zingine utaona hapa hata hizi sheria zinawekwa hazifanyi kwingine. Hizo sheria ziliwekwa ni nyingi. Sheria ingine inasema eti ni lazima walimu wawe na gredi ya C+ ambayo ni masikitiko katika Eneo Bunge langu. Hata tunaweza kuisema kama ni janga la kitaifa, kwa sababu sisi tulipata alama ya B- moja katika Eneo Bunge nzima. Tuna alama za C plain mbili. Nilipata shule hazina mikakati ya watoto kusoma. Sasa sheria zikitungwa hivyo na CBC iwekwe na haijaangalia mtu wa Lamu Mashariki, atafanya vipi? Atapata walimu kutoka wapi? Huwa ni changamoto. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus