15 Mar 2023 in National Assembly:
Siku moja nikiwa katika safari zangu nikiwa rubani, tuliingia katika hoteli fulani ambayo sitaki kutaja jina. Tukipumzika hapo ndio tuendelee na safari katika mbuga za wanyama, nilifika nikaona akina mama wengi. Sasa ikawa mwanaume ni mmoja ambaye ni nahodha wangu. Nilikuwa mdogo wake. Kuuliza hapo, tuliambiwa walikuwa wanaume na wanawake ambao wameoana. Wamechoka na stress za wanaume. Yaani, tunaelekea wapi sisi? Usagaji na ushoga ni njia kubwa ya kusambaza maradhi. Tunajua hivyo. Sasa tunataka nini sisi? Jambo hili linachangia sana katika kuvunjika ndoa. Ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya mambo kama haya. Sasa ukimpata mwanamke anafanya mambo haya au atumie ...
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
alivyosema Mbunge mwenzangu, ukionja leo, basi inakuwa kama ni mdudu sasa utabidi uonje siku zote. Wanawake ni wengi duniani na ni maumbile ya Mwenyezi Mungu. Alituumba na akapanga hivyo. Sasa, tukiwa tuko wengi na wanaume waende wakafanye ushoga, kweli hawa wanawake wataolewa na nani? Tunaomba ndugu zangu hapa, Wabunge wenzangu, tafadhali, tufanye lolote... Nimeshangazwa na Mbunge ambaye amesema hili jambo haliko kwa Katiba. Iko kwa Katiba sahihi. Hili jambo ni haramu na limekatazwa na Katiba kwa sababu haiwezi kuchangia zaidi kwa sababu ya pesa. Wacha zikae kwa sababu sio kila kitu. Tunataka utulivu wa roho na rehema za Mwenyezi Mungu. ...
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Hon. Temporary Speaker, I want to inform
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
that there are Cabinet Secretaries who were rejected by Committees and were approved by this House.
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja hii. Ripoti hii imezungumzia stakabadhi za Umra, ambazo zote zilikuwa sahihi na halali. Hii ni kwa sababu Umra alipitishwa na IEBC mwezi wa Mei, na stakabadhi zake zote zilikuwa sawa. Haikuwa imepita mwaka, kwani alikuwa amepigania kiti cha ugavana kule Lamu. IEBC ni shirika la Serikali. Itakuwaje IEBC wampitishe halafu Bunge liseme halimpitishi?
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Who gave him the permission to inform
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, Umrah ana tajriba ya mambo ya mazingira. Hayo ndiyo mambo yake. Ana shirika linaloitwa Safari Doctor, shirika ambalo limekuwa Lamu na limetusaidia sana mpaka likapewa tuzo na United Nations (UN) katika mambo haya. Leo, nashangaa ninapoambiwa kwamba Umrah hana tajriba. Umrah ndiye mtu anayeweza kututetea tupate fedha kutoka kwa donors ili zitusaidie kwa mambo ya mazingira. Rekodi zinaonyesha Umrah alishindana na nchi nyingine kwa mambo haya, akashinda kama Mkenya, na akapewa tuzo ya UN. Inasikitisha sana. Au ni kwa sababu yeye ni Mbajuni? Hizi shida ambazo tunapata ni nyingi. Mambo haya yamefanywa kana kwamba hawakuwa wanataka ...
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Hivi juzi tu, wamefanya mambo ya forest rangers . Sisi watu wa Lamu East tukapewa
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
watano na watu wengine wamepewa arobaini. Ni mambo haya yanatumika kukandamiza Mbajuni. Kwani sisi hatuna haki? Huyu Umrah ni mmoja tu! Tumepitisha watu wangapi hapa? Mbajuni mmoja ndio mmeona lazima mumkandamize? Si haki! Kamati haiko sawa. Haifai inavyofanya. Nionyesheni document moja ya Umrah ambayo haiko sawa. Mwanzo, alipokwenda Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) aliambiwa hizi
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
ndio zinafaa; apeleke hili na lile. Hii ndio maana alitoa mfano kuwa ukienda kuomba passport, utaambiwa uandike reason . Ukiandika sababu ni kuwa unaenda Tanzania, kisha uende huko na uitwe uende taifa lingine, utatumia passport hiyo hiyo. Kama alipitishwa na IEBC, kwa nini hawezi kupitishwa na Bunge na mwaka haujaisha? Documents zote ambazo sisi tulipeana kama wagombea viti bado hazija expire . Wana sababu zao hawa! Hawamtaki tu Umrah. Ninawaambia wanafanya makosa. Waangalie shirika la Safari Doctor na waulize
view