2 May 2023 in National Assembly:
Mashariki haujafanyiwa. Imekuwa shida kwetu kwani Lamu Mashariki imekuwa nyuma sana kwa miaka mingi kwa sababu hawa wakaguzi wakienda wanaambiwa kule kuna Al Shabaab, bahari chafu na huwa hakuna bahari chafu wala Al Shabaab. Huwa ni kigezo tu cha kuwafanya wasiende kukagua. Na wakiendelea hivyo huwa wanaleta shida. Shida ni kama sasa hivi mimi nimeingia nikifika kwangu kazi ni nyingi za kufanywa na pesa nayo iko lakini nikiangalia zile kazi nilizonazo kama zingefanywa nyuma ingekuwa rahisi kwangu. Kwa mfano, saa hii wanaambiwa upande wa NG-CDF wapande miti. Miti hiyo itapandwa vipi na sasa shule zote za Lamu Mashariki hazina kuta, ...
view
2 May 2023 in National Assembly:
wakaribishwe kule wakague. Lakini pia matatizo yale pia yasionekane ni ya sasa hivi. Uzuri utajulikana ni akina nani ndio waliofanya makosa katika miaka iliyopita. Hao wakija kule watasaidia maanake kuna matatizo ambapo saa zingine bursary inatumika kisiasa, saa zingine bursary haiendi kwa watarajiwa, na saa zingine kuna shule ambazo kuna wakora ambapo inakubidi ukague pesa ya bursary moja kwa moja mpaka ukosane na walimu. Kama hufanyi hivyo, imekuwa ni kama biashara. Ninataka huyo Auditor-General kwa hii Ripoti yake pia ahakikishe amekagua vizuri hizi shule. Shule pia zina matatizo mengi. Kwa hii NG-CDF, tulipoingia, wale walio na wadi tatu wamepunguziwa. Ni ...
view
2 May 2023 in National Assembly:
visiwa, inakuwa ngumu kutengeneza kwa sababu gharama ziko juu sana. Wengine pia hutumia gharama kama hizo kuiba na inakuwa juu kushinda huku. Shukran, Mhe. Spika wa Muda.
view
26 Apr 2023 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Mswada huu. Mwanzo, ningependa kumpongeza ndugu yangu, Mhe. Barasa. Ninaiunga mkono sheria hii. Ninaomba sheria hii iwe rahisi kutumika, na isiwe sheria ngumu ya kuwatatiza The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
26 Apr 2023 in National Assembly:
wagonjwa. Ukitengeneza sheria, huwa inapelekwa kwa Kamati, mnajadiliana, Wabunge wanahusishwa, na hata sisi tukitaka, tunaweza kuja huko kama marafiki wa hiyo Kamati maanake haya ni mambo yanayotuhusu na yanatutatiza kila wakati. Ningependa wagonjwa wapewe uhuru wa kwenda popote wanapotaka kutibiwa katika sheria hiyo. Kumekuwa na mtindo ambapo mgonjwa anapotaka kwenda matibabu India, anazungushwa tu. Madaktari wanamwambia aende kwa Kenya Medical PractitionersPharmacists and Dentists Union (KMPDU) ili ombi lake litiliwe sahihi. Akifika kule, wanamwambia hawawezi kutia sahihi na atafute daktari amtilie sahihi. Akienda kwa daktari, daktari anamwambia kuwa hawezi kutia sahihi kwa sababu huduma hiyo inafanyika Kenya. Hata kama huduma hiyo ...
view
26 Apr 2023 in National Assembly:
Itabidi sisi kama Bunge tujipange, na pia Ministry ijipange, kuwe na hospitali za rufaa katika kila eneo. Maanake hapa Kenya, kuna hospitali sita kubwa za Level 6. Lakini hizi Level6 hospitals zinapatikana katika eneo moja. Coast nzima hakuna Level 6 hospital hata moja. Kisha bado watu huku wanazungumzia ‘ one man, one vote, one shilling’ . Hospitali hizi zinafaa ziwe karibu na wagonjwa. Mtu anatoka Lamu kuja KNH kwa sababu hiyo ndiyo Level 6 hospital ambayo iko karibu naye. Kutoka Kiunga kufika Nairobi ni gharama ya juu. Watu wanakufa kwa sababu ya kukosa uwezo wa kufika KNH. Hospitali yetu ya ...
view
26 Apr 2023 in National Assembly:
Pia, kuna rufaa nyingine ya lazima, ambayo ni kifo. Msiisahau hiyo. Hilo ni tatizo maanake kifo kinasikitisha. Executive Order ilitolewa kusema kuwa mgonjwa akifariki hospitalini, maiti isizuiliwe. Lakini utaona tunaitwa kama Wabunge kuchangia mambo haya. Inakuwa procedure ndefu mpaka watu wanaambiwa watafute title deeds na vitu vingine. Mgonjwa anapofariki, ashapata rufaa ya lazima. Hakuna haja ya kuweka maiti pale. Hospitali ni ya umma kisha unazuilia maiti hiyo mpaka watu wao wafanye Harambee na michango ili walipe. Mtilie maanani rufaa hiyo ya lazima katika sheria hiyo.
view
26 Apr 2023 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, nina mengi ya kuzungumza lakini naona wenzangu pia wako na hamu ya kuzungumza. Kwa hivyo, nitawachia hapo. Ahsante.
view
16 Mar 2023 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi kuwakaribisha watoto wangu wa Tchundwa Primary School kutoka Lamu East, Faza Ward. Wametoka mbali. Walitoka saa tisa asubuhi ili wapate boti, maji iwaruhusu wafike Mokowe. Ili wafike Nairobi, wameondoka huko saa tatu na kufika saa tisa usiku. Nachukua nafasi hii niwaombe watoto wangu wasome. Tumewaleta hapa musome na muangalie dunia ilivyo Nairobi. Watu wamesoma. Kusoma ni muhimu. Musome ili kule kwetu kujengwe kuwe kama Nairobi. Sisi tumesoma na tunaambiwa tujipange ama tutapangwa. Masomo ndio
view
16 Mar 2023 in National Assembly:
Mmeingia Kenyatta International Convention Centre (KICC), mumeenda Nairobi School, na pia kule tumeambiwa tujihadhari kabla ya hatari. Kwa hivyo, sisi tuna mambo mengi. Hatari iko karibu na sisi. Kwa hivyo, naona mutakayoyasoma hapa muende mukafanye bidii ili pia nyinyi mchukue nafasi hizi. Muje mfanye kazi Nairobi. Sio kwamba wengine waandikwe kazi lakini sisi Wabajuni tuwachwe nyuma. Karibuni sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view