16 Aug 2023 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. Tumeona vile pesa au rasilimali ya Tourism Promotion Fund (TPF) ilielekezwa sehemu mbalimbali. Nitakuwa na makosa nikisema Ministry of Tourism ndiyo imechangia pakubwa vita vya Al Shabaab - kwamba inasaidia Al Shabaab watupige kule Lamu na wapige Kenya nzima? Nyingi ya hizo pesa zimepelekwa kwingine. Ukiangalia barabara za Lamu Mashariki, kuna Dodori National Reserve, Kiunga Marine National Reserve na Boni National Reserve. Hizo zimechukua karibu Lamu Mashariki yote. Barabara ya mwisho kutengenezwa na KWS ni 1979. Nitakuwa ninakosea nikisema kwmba Ministry of Tourism inasaidia Al Shabaab ndio utovu wa usalama uendelee Lamu?
view
16 Aug 2023 in National Assembly:
Hon. Speaker, I am sure the Cabinet Secretary is out of order by insinuating that Lamu East is not a tourist destination. When we mentioned the swimming lions in Dodori National Reserve, we meant it. However, if you had maintained the road from 1979, by now many tourists wangekuwa wameenda huko !
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. Kama tunavyojua, dunia inabadilika na shetani ako juu zaidi. TikTok inatusaidia kuonyesha maendeleo yetu. Mimi nimekuwa nikionyesha mabarabara na maendeleo mengine lakini haijatrend kama siku nilipoimba tu Ngamia Wangu . Mambo ambayo si muhimu inatrend na kutuuza zaidi. Kwa hivyo TikTok isiende pahali. Kwa ajili ya uzuri wake, iwe papa hapa.
view
2 Aug 2023 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Swali langu kwa Waziri ni kuhusu huduma zinazotendeka katika ofisi yake kama mambo ya saratani. Lamu ni kisiwa. Mna mpangilio gani kwa sababu huu mpango wa wazee umeleta shida kwetu Lamu? Afisa anakaa Mji wa Lamu. Kutoka Mji wa Kiunga, gharama ya usafiri ya mzee hadi Mji wa Lamu ni Ksh4,100. Pesa anakuja kuchukua ni hiyo Ksh4,000. Inakuwa ni shida sana. Tafuta njia zingine. Inabidi wachange watafute mtu ndio aende awachukulie pesa. Ni shida kwetu. Mkitoa huduma yeyote, mfikirie watu wa Lamu ambao wanaishi kwa visiwa. Changamoto za usafiri ziko ghali sana. Asante, Mhe. ...
view
2 Aug 2023 in National Assembly:
Asante. Swali langu kwa Waziri ni kama lile tu. Sisi Lamu mipangilio yote inayotokea kwa Serikali tunasahaulika. Ningeomba nipewe utaratibu kama vile umepeana kwa Mbunge mwenzangu. Lamu Mashariki waliopata ni kina nani? Jiajiri Lamu Mashariki sioni. Uwezo Fund Lamu Mashariki kutoka nilipokua Mbunge Muwakilishi wa akina mama, nimeenda mbio mpaka sasa hakuna, haiendelei. Youth Enterprise Fund ni shida. Wale wote maafisa ambao wanafaa kukaa sub county ya Lamu Mashariki, wote wanakaa Lamu mjini. Waziri ninakuomba uje, ninasema hili kwa machungu. Kwa sababu mimi nikija hapa watu wananiambia tumeskia mashambulizi ya Al-Shabab. Inaweza kuwa sisi ndio tunasababisha hayo mashambulizi kwa sababu ...
view
2 Aug 2023 in National Assembly:
Bw. Spika wa Muda, mipangilio ya Serikali ni kuwacha Lamu nyuma au ana mipangilio gani ndio haya matatizo ya Al - Shabab yaishe? Kwa sababu kama vijana hawahusishwi katika mipangilio hii ndio inasababisha hayo mambo yanayotokea Lamu. Kisha mwakilisha wadi jana ameshambuliwa na mke wake amefariki. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
6 Jul 2023 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika. Nami naunga mkono hiyo Petition. Ahsante.
view
5 Jul 2023 in National Assembly:
On a point of order, Hon. Speaker.
view
5 Jul 2023 in National Assembly:
Itabidi Bi Waziri aangalie map vizuri.
view
5 Jul 2023 in National Assembly:
Nina hakika hakuna irrigation scheme yoyote Lamu Mashariki. Maji ya Mzima Springs hayawezi kupita Lamu. Hata ikibidi waipitishe kwa lazima, itakuwa gharama kubwa zaidi kuliko kuchukuwa maji kutoka Tana River. Kuna ya kupitisha kwenye bahari. Maji ya Mzima hayawezi kutusaidia kabisa. Weka The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view