Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 231 to 240 of 458.

  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Ahsante Bi. Naibu Speaker. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu wa Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Kusema kweli, hii kupimiwa kwa barabara, inaleta adhari nyingi sana. Sisi tunayapitia mambo haya Lamu. Imekuwa ni kama ya kawaida. Nimeshangaa kwa sababu nilifikiri ni Lamu peke yake ambayo inapata shida kama hizi. Ikifika saa kumi na mbili Lamu, barabara na Kaunti nzima inafungwa na hakuna ruhusa ya kutoka nje. Kukiwa na mambo ya dharura, ni gari la wagonjwa pekee ambalo linatoka. Katika sehemu zingine nilipatana na Special Force wakanisomea kama mtoto mdogo. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Katika barabara ya kwenda Kiunga, hakuna gari linapita. Kukiwa na jambo la dharura Kiunga, lazima utumie bahari, ambayo saa zingine ina mawimbi makali. Watu wengi wamepata ajali nyingi. Naunga mkono huyu Mheshimiwa. Maombi yake yafuatiliziwe na pia katika sehemu zingine. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Ilipotokea COVID-19, Wakenya walipata amri za kutotoka nje. Sisi tulikuwa tumezoea kwetu. Kwetu Lamu, mara kuna amri ya kutotoka ya wavuvi ama barabara ambayo haipitwi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Hii inatuadhiri sana kiuchumi. Naomba maombi haya yaangaliwe na Kamati vizuri, na ihakikishe jambo hili limerekebishwa. Pia, hizo baraka zisonge kwetu. view
  • 16 Mar 2023 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu wa Spika view
  • 15 Mar 2023 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nipate kuchangia. Moja kwa moja, nataka nimpongeze ndugu yetu, Mhe. Mohammed Ali, kwa kuleta Hoja hii. Hoja hii imeambatana na Katiba, maanake kama kitu kinakatazwa na Katiba, basi Katiba hiyo hiyo inafaa ikataze kusambazwa kwake. Ikiwa wewe ni muuzaji wa bhangi na bhangi inakatazwa kwenye Katiba, huwezi kuruhusiwa kuenda kuisambaza ile habari na uuze ile bhangi. Kwa hivyo, ni sawa sawa na Hoja hii inavyosema tukataze na tupinge hizi mbinu zozote ambazo wanatumia ili kusambaza maneno haya ya usagaji na ushoga. Mimi nataka niende kwa dhamira. Dhamira ya mwanadamu ... view
  • 15 Mar 2023 in National Assembly: mtu huyo awe na kasoro ili kuikubali. Hakuna utamaduni wetu wa Waafrika ama wa Kenya ambao unakubali jambo hili. Ni wazi kuwa inafaa haya mambo ya kuchapisha vitabu au kusambaza vitu hivi vikatazwe. Nataka pia nizungumze kuhusu muktadha. Sisi kama Waafrika hatuliungi mkono jambo hili. Halikuwa linazungumziwa zamani. Saa hii, tumelizungumzia. Limeletwa na hao watu wanaotuletea msaada kwa sababu ya umaskini wetu. Afadhali tukufe na njaa. Umaskini ni wetu. Tumeishi hivyo na tutaendelea kuishi bila wao. view
  • 15 Mar 2023 in National Assembly: Misingi ya pamoja, common ground, na misimamo ya dini zote za Kenya haziungi mkono jambo hili. Tumeambiwa kwa Quran na Bibilia aya ambazo zinapinga jambo hili. Sasa hakuna haja tuunge mkono kitu ambacho kinapingwa na dini zote. Dini ikipinga kitu, kuna sababu. Qowmu Lut waliadhibiwa vikali. Je, twataka tujiunge na wao na tuadhibiwe vikali? Zile adhabu ambazo saa hizi Mwenyezi Mungu anatupatia, bado hatujatosheka. Mara kuna jua, kiangazi na ukame. Ikiwa ni mvua, ni mafuriko. view
  • 15 Mar 2023 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika wa Muda. Jambo hili la usagaji na ushoga ni la kuchukiza. Mwanaume anabadilishwa anakuwa mboga. Ukimwona analegeza mikono yaani utashangaa amekuwa kabichi. Amelainika namna ile na si maumbile alioumbwa na Mwenyezi Mungu. Tena anajilegeza zaidi kushinda hata wanawake. Ata amekosesha wanawake wengine market . view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus