15 Mar 2023 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nipate kuchangia. Moja kwa moja, nataka nimpongeze ndugu yetu, Mhe. Mohammed Ali, kwa kuleta Hoja hii. Hoja hii imeambatana na Katiba, maanake kama kitu kinakatazwa na Katiba, basi Katiba hiyo hiyo inafaa ikataze kusambazwa kwake. Ikiwa wewe ni muuzaji wa bhangi na bhangi inakatazwa kwenye Katiba, huwezi kuruhusiwa kuenda kuisambaza ile habari na uuze ile bhangi. Kwa hivyo, ni sawa sawa na Hoja hii inavyosema tukataze na tupinge hizi mbinu zozote ambazo wanatumia ili kusambaza maneno haya ya usagaji na ushoga. Mimi nataka niende kwa dhamira. Dhamira ya mwanadamu ...
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
mtu huyo awe na kasoro ili kuikubali. Hakuna utamaduni wetu wa Waafrika ama wa Kenya ambao unakubali jambo hili. Ni wazi kuwa inafaa haya mambo ya kuchapisha vitabu au kusambaza vitu hivi vikatazwe. Nataka pia nizungumze kuhusu muktadha. Sisi kama Waafrika hatuliungi mkono jambo hili. Halikuwa linazungumziwa zamani. Saa hii, tumelizungumzia. Limeletwa na hao watu wanaotuletea msaada kwa sababu ya umaskini wetu. Afadhali tukufe na njaa. Umaskini ni wetu. Tumeishi hivyo na tutaendelea kuishi bila wao.
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Misingi ya pamoja, common ground, na misimamo ya dini zote za Kenya haziungi mkono jambo hili. Tumeambiwa kwa Quran na Bibilia aya ambazo zinapinga jambo hili. Sasa hakuna haja tuunge mkono kitu ambacho kinapingwa na dini zote. Dini ikipinga kitu, kuna sababu. Qowmu Lut waliadhibiwa vikali. Je, twataka tujiunge na wao na tuadhibiwe vikali? Zile adhabu ambazo saa hizi Mwenyezi Mungu anatupatia, bado hatujatosheka. Mara kuna jua, kiangazi na ukame. Ikiwa ni mvua, ni mafuriko.
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika wa Muda. Jambo hili la usagaji na ushoga ni la kuchukiza. Mwanaume anabadilishwa anakuwa mboga. Ukimwona analegeza mikono yaani utashangaa amekuwa kabichi. Amelainika namna ile na si maumbile alioumbwa na Mwenyezi Mungu. Tena anajilegeza zaidi kushinda hata wanawake. Ata amekosesha wanawake wengine market .
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Siku moja nikiwa katika safari zangu nikiwa rubani, tuliingia katika hoteli fulani ambayo sitaki kutaja jina. Tukipumzika hapo ndio tuendelee na safari katika mbuga za wanyama, nilifika nikaona akina mama wengi. Sasa ikawa mwanaume ni mmoja ambaye ni nahodha wangu. Nilikuwa mdogo wake. Kuuliza hapo, tuliambiwa walikuwa wanaume na wanawake ambao wameoana. Wamechoka na stress za wanaume. Yaani, tunaelekea wapi sisi? Usagaji na ushoga ni njia kubwa ya kusambaza maradhi. Tunajua hivyo. Sasa tunataka nini sisi? Jambo hili linachangia sana katika kuvunjika ndoa. Ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya mambo kama haya. Sasa ukimpata mwanamke anafanya mambo haya au atumie ...
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
alivyosema Mbunge mwenzangu, ukionja leo, basi inakuwa kama ni mdudu sasa utabidi uonje siku zote. Wanawake ni wengi duniani na ni maumbile ya Mwenyezi Mungu. Alituumba na akapanga hivyo. Sasa, tukiwa tuko wengi na wanaume waende wakafanye ushoga, kweli hawa wanawake wataolewa na nani? Tunaomba ndugu zangu hapa, Wabunge wenzangu, tafadhali, tufanye lolote... Nimeshangazwa na Mbunge ambaye amesema hili jambo haliko kwa Katiba. Iko kwa Katiba sahihi. Hili jambo ni haramu na limekatazwa na Katiba kwa sababu haiwezi kuchangia zaidi kwa sababu ya pesa. Wacha zikae kwa sababu sio kila kitu. Tunataka utulivu wa roho na rehema za Mwenyezi Mungu. ...
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Hon. Temporary Speaker, I want to inform
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
that there are Cabinet Secretaries who were rejected by Committees and were approved by this House.
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja hii. Ripoti hii imezungumzia stakabadhi za Umra, ambazo zote zilikuwa sahihi na halali. Hii ni kwa sababu Umra alipitishwa na IEBC mwezi wa Mei, na stakabadhi zake zote zilikuwa sawa. Haikuwa imepita mwaka, kwani alikuwa amepigania kiti cha ugavana kule Lamu. IEBC ni shirika la Serikali. Itakuwaje IEBC wampitishe halafu Bunge liseme halimpitishi?
view
15 Mar 2023 in National Assembly:
Who gave him the permission to inform
view