Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 311 to 320 of 458.

  • 25 Sep 2019 in National Assembly: Inasikitisha kuona kwamba wengi wa vijana wetu hawana mwongozo katika hali hii. Hawana kazi wala ujuzi na hawajasomea taaluma nyingine. Sio kwa sababu vijana hawataki kufanya hivyo, ni kwa sababu ya utaratibu na mpangilio wa Serikali yetu. Hiyo ndiyo inafanya vijana wakose imani katika jambo hili. Nikizungumzia Eneo Bunge la Lamu, hivi sasa, watu wengi wanafahamu kwamba tuko na Lamu Port-South Sudan-Ethiopia-Transport Corridor Project (LAPSSET). Lakini kwa masikitiko makubwa, jambo ambalo Serikali haijafanya ni kuhakikisha kwamba mradi huu umewasaidia vijana. Zile nafasi 1,000 ambazo ziliahidiwa na Serikali kwa vijana katika LAPSSET, hadi sasa, hazijawekwa bayana. Jambo hili halijafanyika. Kutokana na ... view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Asante. Ningependa kuchukua fursa hii kuunga mkono Mswada huu na vilevile kumpongeza pakubwa Mbunge aliyeuleta hapa kwa sababu suala la ajira ni suala nyeti. Aliyeuleta Mswada huu amelenga masuala ya akina mama wanaofanya kazi, haswa wakati wanapojifungua na namna watakavyopata nafasi ya kupumzika watakapokuwa wakiwalea watoto wao. view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Ukweli ni kwamba Waheshimiwa wengi wanaposimama kuchangia Mswada huu wanazungumzia neno “ajira” kwa ujumla katika nchi hii. Ukweli ni kwamba ile hali ya ajira katika nchi hii ni hali ambayo inahitaji kupewa kipaumbele tunapojadili kuhusu suala hili. view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Mzazi anapojifungua mtoto ina maana ya kwamba mtoto yule ameanza maisha yake. Malengo ni kwamba mtoto yule atalewa na mwishowe atahitaji kazi. Tunajua vizuri namna nchi yetu ilivyo. Mheshimiwa aliyeuleta Mswada huu ametambua kwamba kuna dharura ya kuwapatia akina mama wanaofanya kazi muda wa kutosha wanapojifungua ili wajipange namna watakavyowaelekeza watoto hao. Naamini kwamba muda ambao wamepewa ni wa takribani miezi mitatu. Ningependa vilevile akina mama hao, baada ya kupewa miezi hiyo mitatu, kuwe na namna ambayo watakuwa wanasaidika kikamilifu katika kuliangazia suala hili la watoto. Hii ni kwa sababu, utotoni mwa kila mtu ni wakati muhimu sana katika malezi. view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Hivi sasa, vijana wengi wako katika hali ya sintofahamu; hawajitambui ama kujielewa. Vijana hao pengine wametupwa na mama zao ama hawajui wazazi wao. Siku hizi idadi ya vijana ambao hawana kazi imekuwa kubwa zaidi kwa sababu ya tatizo hili ambalo lilianza hapo awali, na kwa sababu ya makosa ambayo hufanyika wakati mtoto anapozaliwa. Kwa hivyo, kuna dharura katika nchi hii ya kuwepo kwa mwongozo kamili wa kujua idadi kamili ya vijana wanaozaliwa, wanaoinuka, wanaosoma na hata wale ambao hawana kazi. Sielewi ni kwa sababu gani nchi hii haina watu wengi. Tukiangazia idadi ya wanaoishi katika nchi hii, ambao wamefikia kiwango ... view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Ningependa kusema kwamba serikali zote za kaunti 47 ni vizuri ziwe na data ya kuonyesha ni vijana wangapi hawana kazi na wanaohitaji kazi na kiwango chao cha masomo, ili nchi hii iwe na mwongozo mwema. view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Itakuwa vyema wakati kila jambo linaanza liwe na utaratibu. Linapoanza na makosa basi hata huko mbele mambo mengi yataenda mrama. Ni dharura kubwa kwa nchi hii kuangazia mwelekeo na mwongozo wa wananchi wake hususan vijana hapa nchini kwa sababu namna inavyoenda ni kwamba wengi wamekosa imani kabisa na nchi yao. Unapata wengine wanafanya mambo ambayo hayastahili, wengine wanajiingiza katika mambo mabaya na tabia ambazo si njema katika jamii. Kwa hivyo, kuna dharura kubwa hapa nchini ya kuweza kuangazia na kuwa na mipangilio kamilifu katika suala hili kwa wananchi na jamii. view
  • 18 Sep 2019 in National Assembly: Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu. Asante. view
  • 10 Sep 2019 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. Pursuant to the provisions of Standing Order No. 42A, I wish to ask the CS for Transport, Infrastructure, Housing, Urban Development and Public Works: view
  • 10 Sep 2019 in National Assembly: (i) What is the status of compensation to persons affected by the acquisition of land for the development of the Lamu Port – South Sudan – Ethiopia - Transport (LAPSSET) Corridor Project in Lamu? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus