Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 381 to 390 of 458.

  • 11 Oct 2017 in National Assembly: Katika nchi yetu ya Kenya, sehemu zote ziko na ardhi ya kutosha ya kufanya ukulima. Ni jambo la kushangaza kuona nchi yetu ya Kenya leo inaagiza bidhaa kama sukari kutoka nchi za nje, na ilhali tuko na viwanda na wakulima ambao wako tayari kuifanya biashara hii. Leo ni bidhaa moja ambayo imeletwa hapa na Mhe. mwenzetu. Tatizo moja ni kwamba wakulima hawalipwi pesa yao kwa wakati unaofaa. Na kutokana na haya, inasababisha wakulima hawa kupata hasara, kufa moyo ama pengine inasababisha hali hii ya bidhaa hizi kutoweko katika nchi yetu kwa sababu ya udhaifu kama huu. Sasa tujiulize tatizo hili ... view
  • 11 Oct 2017 in National Assembly: Leo tunazungumzia masuala ya wakulima wa miwa lakini tatizo hili si la wakulima wa miwa peke yao. Tatizo hili liko kwa kila nyanja kama ilivyogusiwa na wenzangu hapa. Tatizo liko kila nyanja. Leo sisi kama nchi hatupaswi kuomba mambo fulani katika nchi za inje, ama kama nilivyosema, tunaleta bidhaa kutoka nchi za inje, na ilhali sisi tunazo kila sababu na kila kitu cha kuweza kufanya mambo haya. view
  • 11 Oct 2017 in National Assembly: Suala hili la miwa tunafaa kuliangazia. Kwa mfano, kuna viwanda ambavyo hivi sasa vimekufa, vimetupilia mbali kazi ama vimeweza kutoweza kufanya biashara hii. Kuna Kiwanda cha Ramisi, Pwani. Hakuna sababu hata moja ya viwanda hivi kufungwa. Ikiwa nchi hii itasimama na idhamini ukulima, sioni sababu ya matatizo kama haya. Leo, sioni sababu Serikali itumie pesa kununua vyakula vya kupea watu katika sehemu ambazo zina ukame. Pesa hizi zinazotumiwa kununua bidhaa hizi za kugawia watu wenye njaa na sehemu kame, kama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be ... view
  • 11 Oct 2017 in National Assembly: zingeelekezwa katika masuala haya ya ukulima, zipewe wakulima, nafikiri kila mahala ama sehemu katika nchi hii, watu wangeweza kufanya ukulima. view
  • 11 Oct 2017 in National Assembly: Mimi ningependa kuwaambia ndugu zangu Waheshimiwa kwamba mambo kama haya ni muhimu tuyajadili kwa namna inayotakikana. Tunafaa tujadili ni vipi mkulima atalipwa pesa wakati ameleta bidhaa yake. Ni vipi tutaweza kulizungumzia suala la miwa peke yake kwa sababu uchumi wetu ni ukulima na matatizo yako kila mahali. Leo, Bunge hili litapitisha suala hili la wakulima wa miwa wasaidike kwa namna hii, lakini je, kesho tutarudia tena tuanze kuzungumza na wengine? Naomba ile kamati ambayo itaundwa iweze kuzingatia zile nyanja husika na kuweza kulisuluhisha suala hili la kuhakikisha kwamba nchi hii haiko tena katika ile taswira ya kuonekana kwamba watu wako ... view
  • 11 Oct 2017 in National Assembly: Ni muhimu sana Serikali izingatie wakulima na ihakikishe kwamba imeweza kusaidia viwanda vyote na wakulima wote. Nina imani kubwa litakapofanyika hivyo, basi tutasahau masuala ya matatizo ya vyakula na kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi hii. Leo, kilo moja ya sukari ni mia tatu ama mia nne. Kuna watu wameacha kunywa chai kwa sababu hawawezi kununua sukari. Leo tunajadili vipi mkulima atalipwa pesa yake wakati ameleta bidhaa. Tunamjadili vipi yule anainunua hii sukari ili bei ipungue? Njia ya kuweza kumsaidia yule mwenye kununua bidhaa hii ni kuhakikisha ya kwamba wakulima wamesaidika na tumeweka mambo ya ukulima kisawasawa. Bidhaa zile zinapofika ... view
  • 11 Oct 2017 in National Assembly: Ahsante na naunga mkono Hoja hii, Mhe. Spika wa Muda. view
  • 16 Mar 2017 in National Assembly: On a point of order, Hon. Temporary Deputy Speaker. view
  • 16 Mar 2017 in National Assembly: Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. I think we are discussing a very important Motion today and yet we are only four members in this Chamber. I do not think we can proceed with this important Motion for our country while we are only four Members. The decision that will be made from this Motion will affect this country and it is wrong for only four members to make it. I do not think we have quorum under Standing Order No.35 to proceed with this Motion. Thank you. view
  • 7 Jun 2016 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwa kweli, Hoja hii ni ya kushangaza. Kuzungumza kuhusu Bunge hili kupitisha mkopo wa Kshs27.3 bilioni ni jambo la kushangaza. Huu mradi ambao unafanyika Mombasa ni mradi ambao tukiwa watu wa Pwani na Wakenya, tungependa uwe kwa sababu ya kuinua uchumi wa nchi hii na uchumi wa Pwani. La kushangaza ni kwamba jambo hili limeletwa Bungeni ilhali mradi huu unaendelea. Ninashindwa pesa hizi zilikuwa zimepangiwa kulipwa namna gani ilhali huu ni mradi ambao tayari umeanza. Isitoshe, linalonishangaza ni kwamba mbali na kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuinua uchumi wetu, ni vipi tutaweza kusaidia sehemu ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus