27 Feb 2018 in National Assembly:
Ikiwa mwanakandarasi yule atapewa kilomita 100 kuzijenga kwa miaka mitano, kazi hiyo ikigawanyiwa wanakandarasi watano, wataikamilisha kwa muda wa mwaka mmoja. Mikakati kama hiyo ndiyo itaifanya Serikali kuokoa pesa ambazo zitaiwezesha kufanya mambo mengine badala ya kutumia pesa kwa njia moja peke yake kwa njia ambazo sivyo.
view
27 Feb 2018 in National Assembly:
Nataka kuipongeza Serikali kwa juhudi zake nikizungumzia Eneo Bunge la Lamu Mashariki na Kaunti ya Lamu kwa jumla. Kwa mara ya kwanza, wakazi katika Kaunti ya Lamu wameweza kupata barabara ya lami. Lakini kwa masikitiko makubwa, mwanakandarasi anayetengeneza barabara kutoka Garsen mpaka Lamu ana mwaka mmoja hivi sasa ameshapewa cheti. Mheshimiwa Rais ametia barabara wakfu lakini mwanakandarasi huyo hajatengeneza barabara hiyo, na haya ndiyo matatizo. Tuko na barabara ambayo inatoka Lamu kwenda Kiunga. Tunasikia mara kwa mara kuna magaidi na kadhalika. Barabara hiyo ikitengenezwa na iwekwe lami, itasaidia pakubwa katika masuala haya. Kwa hivyo, mimi naunga mkono lakini kama nilivyosema, ...
view
21 Feb 2018 in National Assembly:
Asante Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii inayohusiana na maswala ya usalama katika nchi yetu hususan katika sehemu ya Wajir. Kwa kweli, swala la usalama ni swala nyeti sana. Limeweza kushuhudiwa mara kadhaa na limeweza kuleta madhara katika sehemu nyingi. Pia, limeweza kuleta madhara katika uchumi wetu, elimu ya watoto wetu na afya ya Wakenya. Si mara ya kwanza swala hili kujadiliwa Bungeni katika swala zima la usalama. Kule kutokana kwa mara kadhaa Bungeni inamaanisha kwamba limekuwa ni donda sugu. Kwa maana hii, linaonekana kwamba haijapatikana suluhisho katika swala zima. Ingawaje ningependa kushukuru Serikali ...
view
21 Feb 2018 in National Assembly:
rasilmali zake na nguvu nyingi kupambana na mambo ambayo hayastahili. Utapata majeshi yetu na walinda usalama wetu wanapelekwa katika sehemu nyingine kupambana na wananchi wa kawaida. Yote haya ni mifano mibaya katika nchi yetu na nchi za nje. Kwa hivyo, tunapojadili swala hili na kuliangalia, ni lazima tuangalie pande zote katika hili swala zima ili tupate suluhisho juu ya maswala kama haya. Ikiwa sisi wenyewe kama nchi ndio mara nyingine tunasababisha matatizo haya, je yule mwingine ambaye ni adui atafanya nini? Naibu Spika wa Muda, kwa kweli adhari ni nyingi kama nilivyosema hususan nikuzungumzia maswala ya Eneo Bunge ninalotoka ama ...
view
21 Feb 2018 in National Assembly:
Nikizungumza kwamba kuna nyumba imepigwa alama ya “X” na kuvunjwa, haijavunjwa, wala hakuna ilani yoyote. Ninataka kuhakikishia watu wa Lamu Mashariki wasiwe na hofu yoyote . Hakuna nyumba inavunjwa na Serikali iko pamoja na wao. Sidhani kama kutakuwa na maswala kama hayo. Maendeleo yapo na tumeyaona.
view
11 Oct 2017 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza kabisa, nataka nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye aliniwezesha kurudi katika Bunge hili la Kumi na Mbili. Vile vile, nawashukuru wananchi wa Eneo Bunge la Lamu Mashariki kwa kuwa na imani na mimi tena na kuniregesha kuwahudumia kwa miaka mitano ijayo. Bunge hili lajadili Hoja muhimu sana, ni Hoja nyeti na inahusiana na uchumi wetu wa Kenya. Kama tunavyofahamu, ukulima ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu wa Kenya. Lakini, ni masikitiko makubwa kuona, la kwanza, Wabunge wengi hawako kujadili suala hili ambalo ni muhimu katika nchi yetu ya Kenya.
view
11 Oct 2017 in National Assembly:
Suala la ukulima katika nchi yetu ya Kenya, Mhe. Spika wa Muda, limekuwa ni doda sugu. Kwa maana hiyo, utapata ile hali iliyoko kwa wakulima wetu leo kama Waheshimiwa wanavyoizungumzia, hakuna mkulima yeyote ako na furaha kwa sababu ya kufanya kazi hii. Sababu ambazo zinasababisha haya yote yamezumgumzwa ni tofauti za hapa na pale. Pengine ni wahusika wakuu wanaosimamia suala hili kuwasaidia wakulima, ama utaratibu unaotumika kuwatumia na kuwasaidia wakulima. Sababu ni nyingi zinazofanya wakulima hawa kufa moyo na kutokuwa na hamu ya kufanya ukulima.
view
11 Oct 2017 in National Assembly:
Katika nchi yetu ya Kenya, sehemu zote ziko na ardhi ya kutosha ya kufanya ukulima. Ni jambo la kushangaza kuona nchi yetu ya Kenya leo inaagiza bidhaa kama sukari kutoka nchi za nje, na ilhali tuko na viwanda na wakulima ambao wako tayari kuifanya biashara hii. Leo ni bidhaa moja ambayo imeletwa hapa na Mhe. mwenzetu. Tatizo moja ni kwamba wakulima hawalipwi pesa yao kwa wakati unaofaa. Na kutokana na haya, inasababisha wakulima hawa kupata hasara, kufa moyo ama pengine inasababisha hali hii ya bidhaa hizi kutoweko katika nchi yetu kwa sababu ya udhaifu kama huu. Sasa tujiulize tatizo hili ...
view
11 Oct 2017 in National Assembly:
Leo tunazungumzia masuala ya wakulima wa miwa lakini tatizo hili si la wakulima wa miwa peke yao. Tatizo hili liko kwa kila nyanja kama ilivyogusiwa na wenzangu hapa. Tatizo liko kila nyanja. Leo sisi kama nchi hatupaswi kuomba mambo fulani katika nchi za inje, ama kama nilivyosema, tunaleta bidhaa kutoka nchi za inje, na ilhali sisi tunazo kila sababu na kila kitu cha kuweza kufanya mambo haya.
view
11 Oct 2017 in National Assembly:
Suala hili la miwa tunafaa kuliangazia. Kwa mfano, kuna viwanda ambavyo hivi sasa vimekufa, vimetupilia mbali kazi ama vimeweza kutoweza kufanya biashara hii. Kuna Kiwanda cha Ramisi, Pwani. Hakuna sababu hata moja ya viwanda hivi kufungwa. Ikiwa nchi hii itasimama na idhamini ukulima, sioni sababu ya matatizo kama haya. Leo, sioni sababu Serikali itumie pesa kununua vyakula vya kupea watu katika sehemu ambazo zina ukame. Pesa hizi zinazotumiwa kununua bidhaa hizi za kugawia watu wenye njaa na sehemu kame, kama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be ...
view