Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 2266.

  • 6 May 2025 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza ninataka kutoa rambirambi zangu kwa familia, jamii, marafiki na wale wote waliokuwa karibu na familia ya Mhe. Charles Ong’ondo Were. Kama tunavyoelewa ni kwamba hivi sasa familia wanalia kwa sababu wamempoteza mzee wao. Familia ya Mhe. Were iko katika huzuni wakati huu. Sio kwamba wakati wa Mwenyezi Mungu kwake wa kufa ulikuwa umefika lakini ni mambo ambayo yaliyotendwa na majambazi. Jambo la kusikitisha kabisa ni kwamba baadhi ya hao majambazi wengine wao ni polisi. Hili ni jambo la kusikitisha sana ikiwa sisi sote tunalindwa na askari halafu hao askari wanatuendea kinyume. view
  • 6 May 2025 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate. view
  • 6 May 2025 in Senate: Tunataka uchunguzi ufanywe kisawa sawa. Wale watakaopatikana na hatia, hukumu iweze kupeanwa vile vile kisawa sawa, kwa sababu jambo waliotenda ni la kusikitisha. Bw. Spika, wakati huu waheshimiwa wengi wako katika hali ya sintofahamu ya kuogopa; kutojua ni nani mwingine ambaye ataangushwa na risasi. Kutokana na hicho kitendo kilichofanyika kwa mheshimiwa, tunaomba waheshimiwa wengine wajue ya kwamba kama uko na askari na hawezi kukutetea, ikakuwa ni jambo la kusikitisha. Kwa wale ambao wamefiwa na mpendwa wao, ninaomba tuwaweke mbele ya Mwenyezi Mungu, tuwaombee na tujue ya kwamba hilo ni kosa ambalo lilifanyika. Ni mauti ya Mhe. Ong’ondo Were ambayo ilifanyika ... view
  • 9 Apr 2025 in Senate: Asante, Bw, Spika wa Muda. Kiwanja hiki cha ndege cha Isiolo kina wale mahandisi na maafisa husika ambao waliweza kutayarisha ripoti juu yake. Tukiangalia, kwanza, hawa wataalam waliweza kutayarisha ripoti yao na kusema kwamba hiki kiwanja kitakuwa tayari ikiwa kitatumia shilingi 1.5 bilioni. Bw. Waziri, ningependa kujua majina ya hawa mahandisi ambao waliweza kutengeneza kiwanja hiki cha ndege na wakaangalia na kusema watatumia shilingi 1.5 bilioni. Mahandisi waliyofanya kazi hii wawekwe wazi hapa pamoja na wahusika wowote waliokuwa na uwezo wa kutengeza kiwanja hicho. Swala langu la pili ni ikiwa hivi sasa imeonekana ya kwamba chini ya hii ardhi haiwezi ... view
  • 9 Apr 2025 in Senate: wameadhibiwa? Swala la tatu ni Bw. Waziri atueleze wao mahandisi walisomea wapi uhandisi wao? view
  • 9 Apr 2025 in Senate: La mwisho, Bw. Spika wa Muda--- view
  • 9 Apr 2025 in Senate: Swali langu la mwisho ambalo ningetaka kumuuliza Bw. Waziri- -- view
  • 9 Apr 2025 in Senate: Ndio Swali ni moja lakini, pole, ningetaka kuongezea. Ni hatua gani ambayo inaweza kuchukuliwa kuona ya kwamba athiri kama hii haitatokea na hawa mainjinia wanatakikana kumsaida Mhe. Rais ili aonekane akisema kitu kitafanyika, kifanyike. Hawa ndio wafisadi kwa sababu wanataka kurudi tena watengeneze pesa, ilhali, pesa ambayo ilikuwa allocated kwa airport hiyo ni zile ambazo walizitumia na sasa wamezweka mara mbili, kutoka shilingi 1.5 bilioni. Sasa wanasema ya kwamba wanaweza kumaliza kiwanja hicho ikiwa watatumia shilingi bilioni nne. Kwa hivyo, ni hatua gani ambayo Waziri amechukua kuona ya kwamba hawa wahandisi waliofanya hii kazi wamechukuliwa hatua? view
  • 8 Apr 2025 in Senate: Thank you, Madam Temporary Speaker. It is not dirty. I just wanted to say that it might not appear to be clean, but that word ‘dirty’ does not exist legally. He can use another language. view
  • 3 Apr 2025 in Senate: Asante, Bw. Spika. Hukuwa umeniita lakini nimechukuwa nafasi hii kwa sababu ulikuwa unaongea na dadangu, nikasema ni sawa, nitatendelea. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus