3 Apr 2025 in Senate:
Bw. Spika, kawaida lazima umtaje mtu jina kama ilivyo kawaida.
view
3 Apr 2025 in Senate:
Bw. Spika, kwanza nataka kuunga mkono hii Hoja ya kuongeza muda kwa ile jopo linalofanya interview kuchagua wale wenzetu ama watu ambao watakuwa makamishina. Jopo hili lina kazi nyingi sana kwa sababu lilikuwa limepewa muda kulingana na Katiba. Hata hivyo, ule muda unaonekana umeyoyoma sana na bado wale watu wanafanyiwa interview wanaendelea kuja. Muda ukifiki hawatakuwa wamekamilisha na ndiyo sababu wameomba muda, waongezewa siku 14. Sababu walizosema ni kuwa hawakutarajia kitendo kama hiki kitaweza kutendeka. Walitumaini watamaliza ili Wakenya wapate tume itakayosimamia mambo ya uchaguzi katika nchi yetu ya Kenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for ...
view
3 Apr 2025 in Senate:
Kitu ambacho ningependa kusisitiza ni kuwa tunataka kama Wakenya tupate kazi safi. Ni matumaini yetu kuwa wale watu watakaochaguliwa watatimiza wajibu wao na kufanya kazi vilivyo. Vile vile, tunajua watu ambao wanakuwa interviewed wanatoka sehemu mbalimbali za Kenya. Hii sio kazi ambayo unaweza kuketi na kuchagua watu. Tunataka kuona katika muda wanaouhitaji ili kumaliza kazi hii, watachukua watu kutoka upande zote za Kenya. Ni jambo kubwa ama jambo lililo na mzigo mkubwa katika muda huu ambao wameuliza. Kwa hivyo, mimi nataka kuunga mkono ya kuwa ni sawa wakiongezewa siku hizi 14 ambazo wameuliza. Ikiwa wamemaliza zile siku zao 90 kulingana ...
view
3 Apr 2025 in Senate:
Sio haki kijana kama Cherarkey kuongea ninapoongea. Bila kuchukua wakati zaidi, naunga mkono Hoja hii kwa dhati.
view
1 Apr 2025 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Ninataka kuchangia hii Kauli ambayo imeletwa na ndugu yangu, Sen. Omogeni. Hili ni jambo ya kusikitisha sana. Katika Kaunti ya Nyamira, kuna watu ambao wamesoma; kuna watu ambao wanaelewa kunaendelea namna gani. Kwa hivi sasa, tunaona aibu tupu ambayo huyu Gavana Amos Nyaribo ameleta ndani ya Kaunti ya Nyamira. Haiwezekani kuwe na County Assembly mbili ikiwa wewe ni gavana mmoja pale. Ni matusi kwa watu wa Kaunti ya Nyamira kufanyiwa namna hii. Juzi, alituambia ya kwamba yeye hajui ni county assembly gani ambayo iko na mamlaka zaidi ya nyingine. Lakini ikifika wakati wa kutambua pale ...
view
1 Apr 2025 in Senate:
Tafadhali, nipe dakika mbili kwa sababu ninataka kumaliza.
view
1 Apr 2025 in Senate:
Ninasema hivi; tafadhali gavana afanye heshima na watu wa Nyamira ili aweze kuleta mwelekeo vile county assembly itaendelea. Hatuwezi kukubali kuwa na Spika wawili, clerks wawili na hata kila mahali watu wawili wawili. Je, hao watu wanalipwa aje? Ninakubaliana na Kiongozi wa Walio Wengi, Sen. Cheruiyot, akisema kwamba makosa haya yanaletwa na mtu mmoja ambaye yuko na interest hapo, ambaye anapaswa kutuambia. Huyo mtu ambaye ni Controller of Budget, ikiwezekana, pia yeye tumuite aje katika Seneti ili tumhoji. Asante.
view
1 Apr 2025 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, naunga mkono yote ambayo ndugu yangu ambaye ni Kiongozi wa Wengi amesema kuhusu Mswada Huu. Hii ni sheria ambayo itatupa nafasi ya kufungua ukurusa mwingine ili watu wasaidike wakati kuna janga. Hii ni mojawapo ya Miswada ambayo si ya kawaida lakini inaweza kutupatia mamlaka. Wahenga walisema kuwa fimbo ya karibu ndio huua nyoka. Hii inamaanisha kuwa kitu ulichonacho ndicho hukusaidia wakati una shida fulani. Sisi tulikuwa katika shida kubwa na ilikuwa lazima tuepukane na shida hiyo. Kwa hivyo, ni lazima tuwe na sheria ambayo itatusaidia kutoka katika janga hilo. Ndio ...
view
1 Apr 2025 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view