30 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa familia, jamii na marafiki wote wa hizi familia ambazo zimeathirika kwa wapendwa wao kuuwawa katika hali ya kinyama na sintofahamu. Pia, ninatoa heko kwa ndugu yangu na mdogo wangu, Eddy, kwa kuwasilisha Hoja hii ambayo imeleta msisimko mpya ndani ya Bunge letu la Seneti. Tumeona Wakenya wanauwawa kiholelaholela na bila sheria na bila hatua yeyote kuchukuliwa na polisi. Kitu cha kwanza ningependa kutafakari vizuri ni kwamba, kuua watoto wadogo, tena watoto wa kike; watu ambao hawezi hata kupigana ama kujiregeshea ngumi au kusukuma mtu. Wewe unaenda unapata watoto ...
view
30 Oct 2024 in Senate:
Tunawaona tu wakati wanataka kututupia teargas, mimi nikiwa na Sen. Sifuna. Tunawaona tu wakati wanataka kuonyesha sehemu zetu za siri kwa magazeti
view
30 Oct 2024 in Senate:
Hawana maana. Washindwe kabisa! Bi. Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha. Si jambo la kucheka. Mtu kama Willies Ayieko, alikuwa anafanya kazi kwa Wells Fargo.
view
30 Oct 2024 in Senate:
Sen. Sifuna anasema amebeba. Sikuona mimi. Nasema tu ya kwamba ni jambo la kusikitisha hivi leo ikiwa mtu mzima kama yule, aliyekuwa hana ubaya na mtu anaweza kupoteza maisha yake kiholela namna ile halafu anatolewa macho. Hata kama ni uhalifu, umefikaje kiwango hiki? Mwisho, huyu Inspector-General wa Polisi, Bw. Kanja, tuliyemchagua hivi majuzi, ninataka kumwambia aamke kutoka kwa huo usingizi; aamrishe askari wake wafike kila mahali. Vile vile, vitengo vingine vya uchunguzi kama vile Kitengo cha Ujasusi wawape wananchi ripoti za ujasusi na hatua zilizochukuliwa. Tunakemea sana. Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya wahalifu hao. Hoja hii ambayo imeletwa na ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ndugu yangu anayetoa maoni yake kuhusu ripoti yetu ya Kamati ya Usuluhishi amesema kwamba pengine mwenzetu haelewi lugha ya Kiingereza anayoitumia. Namuuliza, je, ni haki kwamba hasemi kwa uwazi? Sen. Munyi Mundigi hujiita daktari. Kama daktari anafahamu lugha ya Kiingereza sana. Nishamsikia akiongea lugha ya Kiingereza. Je, ni haki ndugu yangu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara na Usafiri kusema kwamba Sen. Mundigi ana upungufu wa kufahamu lugha ya Kiingereza? Asante, Bw. Spika wa Muda.
view
27 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ninataka kuwapa kongole wale Maseneta wetu hususan katika Seneti. Haya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
27 Oct 2024 in Senate:
yalikuwa ni majadiliano kulingana na vile ambavyo hatukuwa tumeelewana katika ugavi wa pesa zinazoenda kwenye serikali zetu za mashinani. Majabali wetu waliokuwa katika hii Kamati wakiongozwa na Sen. Ali Roba, walikuwa Sen. Sifuna, Sen. Murgor, Sen. Faki, Sen. Veronica Maina, Sen. Onyonka, Sen. Wamatinga, Sen. (Prof.) Tom Ojienda Odhiambo, SC, Sen. Mungatana, na Sen. Oketch Gicheru. Tuliwapeleka majabali hawa ambao walifanya bidii walivyoweza kujadiliana na kupitisha pesa zile. Kulingana na matokeo ya awali tulikuwa tumesema tupeleke Shilingi 400 bilioni kwenye serikali za kaunti 47 zote. Wagawanye taratibu ili kila kaunti ifaidike na zile pesa. Lakini kwa sababu ya sintofahamu tofauti ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
kuhudumia mtu aliyepata ajali ama mtu anayetaka kulazwa katika vile vyumba ambavyo vinaitwa Intensive Care Unit (ICU) au chumba cha wagongwa mahututi; chumba ambacho mtu anaweza kupata madawa na hatimaye akatoka katika ile hali yake ya kimahututi na akaja akiwa mzima tena na akarudi kwa jamii yake akiwa na afya njema. Tunasema hiyo ndiyo sababu tunasisitiza sana kwamba pesa nyingi zipelekwe kwa hospitali ili wakenya wawe na afya nzuri, nchi itakuwa na maendeleo zaidi. Bw. Spika wa Muda, vile vile kuna hali za mawasiliano. Pesa hizi si za kutumia vile mtu anavyotaka, ila tuone hali za mawasiliano. Barabara zile za ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
Tunaona simanzi zinatandaa katika familia tofauti tofauti kwa sababu ukiulizwa unasema mimi sina pesa za kulipa mishahara. Lakini sasa hakutakuwa na sababu ya wafanyikazi wetu wanaofanya kazi katika serikali za mashinani kukosa mishahara yao. Nasema kwamba kipaumbele iwe ni wafanyikazi wenu wanaofanya kazi katika kaunti zote 47 katika Kenya. Hivi sasa pesa ziko. Walipeni mishahara yao. Bw. Spika wa Muda, nataka kumalizia kwa kusema hii Ripoti yetu tuliiandika na kukubaliana nayo. Hii ni kwa sababu ni ripoti ambayo imepeana mwelekeo na imeeleza ni sababu gani tumeweza kukubaliana kuchukua hizi Shilingi 387 bilioni. Tukakubali zile zingine kama shilingi 13 bilioni zipotee ...
view
17 Oct 2024 in Senate:
Bw. Spika, naunga mkono Hoja hii ili tuwe na nafasi ya kumsikiliza Naibu wa Rais siku ya Jumamosi. Tunaelewa kwamba hii ni kesi muhimu sana na macho yote nchini yanaangalia Seneti. Napeana pole zangu kupitia Senior Counsel, Mhe. Paul Muite, kwa sababu client wake ni mgonjwa. Ugonjwa ni jambo la Mwenyezi Mungu. Hatuwezi kusema kwamba mtu hawezi kuwa mgonjwa. Mtu yeyote anaweza kuwa mgonjwa. Kwa hivyo, ningependa afikishe pole za Seneti. Tunamtakia kila la heri. Mwenyezi Mungu ampe nafuu ili tupatane hapa. Bw. Spika, tuko katika njia panda; ni mgonjwa. Je, tuendelee ama tusiendelee? Tumpe nafasi. Kama binadamu, hii ni ...
view