Vincent Kipkurui Tuwei

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 181 to 185 of 185.

  • 13 Sep 2017 in National Assembly: ambapo ameona ni vyema na haki niwakilishe wananchi wa Mosop. Nawashukuru sana wananchi wa Mosop kwa sababu baada ya kuomba kura kwa miaka mingi wameona ni vyema na haki wakati huu mimi niwe kiongozi wao. view
  • 13 Sep 2017 in National Assembly: Pili, nina shukrani kwa sababu ya kuchaguliwa kwako kama Naibu Spika kwa kura nyingi sana. Tatu, ningependa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa yale yote ambayo amesimamia kama kiongozi wa nchi hii. Tukitafakari yaliyotokea hapo nyuma tunakumbuka kwamba kuna watu wengi ambao walipigania haki ya nchi hii ili tujitawale. Walipigania haki hiyo kwa machungu na maisha yao. Katiba ambayo tunayo hivi sasa imetokana na matukio ya miaka ishirini iliyopita ikiwa ni mchakato wa wale ambao walikuwa na nia nzuri kwa nchi hii. Sisi sote ambao tumepata nafasi ya kuchaguliwa hapa ni kwa sababu ya demokrasia ambayo iko nchini. view
  • 13 Sep 2017 in National Assembly: Nampongeza Rais kwa yale yote ambayo alisema katika Hotuba yake. Alisema kwamba sisi sote lazima tuwajibike kulinda na kudumisha Katiba. Sisi sote kama Wabunge, wao kama viongozi wakuu na idara ya mahakama sharti tuwajibike. Katiba yetu inahitaji kwamba mtu yeyote ambaye ana wajibu lazima azingatie mawazo na nia ya mwananchi. Madaraka haya yote ambayo tumevishwa ni kwa sababu ya mwanachi. Ukiwa Jaji Mkuu, Jaji, Rais, Mbunge, Seneta ama mwakilishi wa kaunti, wajibu na haki ni kwa mwananchi mwenyewe. Huyu ndiye amepewa haki zote kikatiba kwa sababu ni msingi wa nchi hii. view
  • 13 Sep 2017 in National Assembly: Nashukuru kwamba sisi sote ambao tumechaguliwa hapa kama Wabunge ni viongozi tuliyochanganyika wazee, vijana, akina mama na walio na usumbufu fulani wa kimaumbile. Hii inamaanisha kwamba tuko hapa sote kisawa. Tuko hapa kwa sababu ya mwananchi na nchi yetu ya Kenya. Uchanguzi wa Rais ndiyo tatizo kwetu sasa. Suala litakuja mbele yetu Wabunge ili tujadili sheria ambayo inahusiana na uchaguzi. Mwananchi atakapo piga kura, basi uamuzi wake uheshimike. Isiwe kwamba mtu binafsi aliye na madaraka anatumia nafasi yake kuiletea nchi hii hasara. Pesa zote ambazo zitatumika katika uchaguzi wa tarehe 17 Oktoba ni za Wakenya. view
  • 13 Sep 2017 in National Assembly: Uchumi wetu hivi sasa unapitia pagumu. Nimesikia Wabunge wenzangu wakisema kwamba kwao kuna shida ya ukame. Kule kwetu Rift Valley tunamshukuru Mwenyezi Mungu Maulana kwa sababu tunayo mvua kochokocho. Hivyo, mahindi na mazao mengine mengi yatakuwepo na nchi hii itakuwa pazuri. Tunachoomba Serikali ni kwamba bei ya mazao hayo iangaliwe ili kukidhi maisha ya wananchi ambao wanategemea sana kilimo. Sisi sote tunao wajibu. Nashukuru Mwenyezi Mungu kwamba tarehe 17 Oktoba tutakaporudia uchaguzi wa Rais, tutahakikisha kwamba Rais Kenyatta anashinda kwa kura nyingi zaidi ili kutoa aibu ambayo tumepewa na wenzetu. Ahsanteni. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus