All parliamentary appearances
Entries 71 to 80 of 1707.
-
14 Nov 2019 in Senate:
In the meantime, please, spare us.
view
-
12 Nov 2019 in Senate:
Ahsante sana, Bwana Spika. Ninataka kumpongeza ndugu yangu, Sen. (Dr.) Ali, wa kaunti ya Wajir, kwa kuleta hii taarifa. Yale maneno ambayo maseneta wenzangu wamezungumza ni ya haki na kweli kwa sababu magavana wamekuwa ni mtindo wa kutumia pesa kiholela wanapojua ya kwamba hawana hizo fedha katika hazina zao. Hao hupeana kandarasi mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wakidhani ya kwamba watawashawishi wananchi kuwapigia kura. Hao pia huajiri watu kiholela wakifikiria ya kwamba watu watawapigia kura. Ukweli ni kwamba, wananchi wanajua mtu ambaye wanafaa kumchagua. Rais alisema ya kwamba, magavana walipe pending bills lakini hakuna dalili ya kwamba hiyo inafanyika. Kuna ...
view
-
12 Nov 2019 in Senate:
yake, inakuwa ni vigumu kwake kuishi. Kwa hivyo, ninapendekeza ya kwamba Committee on Justice, Legal Affairs and
view
-
12 Nov 2019 in Senate:
watengeneze sheria ambayo ita wahold responsible magavana wale ambao watakosa kufanya vile ambavyo sheria inavyosema.
view
-
9 Oct 2019 in Senate:
Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja hii ambayo imependekezwa na Seneta Kasanga kuhusu kuanzishwa kwa vyama vya jamii vya kulinda misitu katika kila kaunti. Kwanza, nampongeza Seneta Kasanga kwa kuleta Hoja hii katika Bunge kwa sababu imekuja kwa wakati mwafaka, wakati tunaona kwamba kuna misukosuko kila mahali kuhusu misitu. Kuna misukosuko katika sehemu za Mau na sehemu zingine ambazo kuna hatari kubwa kwa misitu yetu kupotea. Bi. Spika wa Muda, kule Mombasa, tuna misitu ya mikoko, yaani, Mangroove
view
-
9 Oct 2019 in Senate:
, ambayo inasaidia kusafisha hewa katika miji yetu na vile vile---
view
-
9 Oct 2019 in Senate:
Mhe. Bi Spika wa Muda, ningeomba unilinde kutoka kwa ndugu zetu wawili ambao wanazungumza kwa sauti ya juu.
view
-
9 Oct 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, pia, naona taa nyekundu imewaka hata kabla sijaanza kuzungumza.
view
-
9 Oct 2019 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Nilikuwa nasema kwamba kule Mombasa tuna misitu ya mikoko ambayo inasaidia pakubwa kwa kusafisha hewa na vile vile kusaidia sehemu ambazo samaki wanataga mayai ili waweze kuzaana na kuendela kutoa chakula na kuweka sawa yale mazingira ya baharini. Bi. Spika wa Muda, ukiangalia sehemu kubwa katika eneo la Tudor, kuna sehemu kubwa ya msitu wa mikoko ambao umekatwa ili wananchi waweze kupata makao. Hii inaathiri pakubwa sehemu za samaki kuzaa na kutaga mayai na hivyo, inapunguza idadi ya samaki ambao wako katika Bahari ya Hindi ambao wanatumia mikoko ile ili waweze kuzaaa na kutaga mayai. ...
view
-
9 Oct 2019 in Senate:
Hoja hii itasaidia pakubwa kuwapa watu asili wa sehemu zile - kama alivyotangulia kusema Sen. Cheruiyot - nafasi ya kusimamia ile misitu kwa sababu wanajua vile watatunza misitu ile na kusaidia pakubwa kuleta ajira katika sehemu zile. Ukiangalia katika sehemu ya Mombasa hivi sasa, kuna sehemu kubwa ambapo kuna takataka ambayo ni hatari kwa mazingira kwa mfano zile plastic ambazo zinatupwa katika bahari ili wale waweze kuweka misingi ya nyumba zao. Jambo hili linaharibu mazingira ya bahari. Mara nyingi, bahari inatoa fursa ya kuondoa uchafu wote wakati zile mawimbi zinakuja katika ufuo ili kuondoa takataka na pia kusafisha mazingira. Lakini ...
view