Zuleikha is grateful that her father’s postings abroad exposed her to a myriad of opportunities, which impacted on her life positively. While studying in South Africa, she recalls that she went through the stages of anger over apartheid. The realization of Zuleikha that one needed to be in politics to influence policy formulation prompted her to join politics. Initially, Zuleikha sought the Kaloleni parliamentary seat but was dissuaded. In parliament she has pushed the government to fund the National Youth Council.
9 Feb 2017 in National Assembly:
Kwa hayo machache, asante.
view
31 Jan 2017 in National Assembly:
Ahsante sama Mhe. Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nichangie Hoja hii. Naunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa mara nyingi humu Bungeni. Hoja hii imejadiliwa katika Kamati mbali mbali za Bunge na katika mikutano tofauti tofauti kwa miaka mingi hapa nchini. Hili jambo linaudhi kwa sababu viongozi ambao wamepewa nafasi kuwasaidia wananchi hawaonyeshi wana kusudia kuwasaidia wananchi. Mbinu zote ziko. Ripoti zimeandikwa. Pesa ziko katika nchi ya Kenya. Haya yote yanatuwezesha kuwa na chakula cha kutosha na maji ya kutumika hata pakiwepo ukame lakini viongozi ambao wamepewa mamlaka wamekataa kufanya hivyo. Kuna ukame katika Kaunti ninayotoka. Inasikitisha. ...
view
31 Jan 2017 in National Assembly:
Lakini kwa ukweli, hiyo haiwezi kusaidia kwa sababu Serikali peke yake ndiyo iko na pesa nyingi za kusaidia. Wakati mwingine ninashangaa nikiona wananchi wanakunywa maji ambayo rangi yake ni kama ya kahawa. Kuna watu hawajaoga miezi mitatu imepita. Watoto wadogo wa miaka miwili na mitatu wanakaa njaa na hukula mara moja tu kwa siku. Wanakunywa uji peke yake bila sukari ama maziwa kuanzia saa tisa mpaka kesho yake saa tisa ndiyo wanakula tena. Hatuwezi kuamini watoto wetu wakipitia shida kama hiyo.
view
31 Jan 2017 in National Assembly:
Pia, kuna ripoti kwamba kuna watu katika hizi sehemu za ukame ambao wanaenda kwenye sehemu ambazo ni nafuu ama zina maji ya mifereji na kupeana watoto wao waangaliwe kwa sababu hawana chakula na wanaweza kuaga dunia. Pia, kuna habari za wasichana wadogo ambao wanauziwa wanaume kwa shillingi mia tano, elfu moja au mbili kwa sababu familia zao zimeshindwa kuwalisha na pia kuna hatari ya hao wasichana kuaga dunia. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Hebu fikiria sisi hapa tukiwa na msichana wetu na hatuwezi kumlisha na inabidi tumuuze kwa mwanaume. Kuna wale ambao wanafurahia jambo kama hilo.
view
31 Jan 2017 in National Assembly:
Ni jambo la kusitikisha na haya yote si kwa sababu ya wananchi kuwa wajinga ama Kenya kuwa nchi maskini sana. Kenya ni nchi tajiri yenye mali ya kutosha kuhakikisha kwamba wananchi hawafikii hali kama hii. Kitu kingine cha kuudhi ni kuwa viongozi hawa ambao wanapewa majukumu ya kuhakikisha kuna maji na chakula kwa wananchi wanatumia njaa kama kitega kura. Wanaenda kwa wananchi wakijisifu sana na kugawanya kilo moja au mbili za maharagwe na mahindi ama maji kidogo na kuwaambia wananchi wawapigie kura. Unashangaa sana kama hii ni nchi ambayo tumemweka Mwenyezi Mungu mbele. Hapa Bungeni, kabla tuanze kuzungumza tunaomba Mwenyezi ...
view
31 Jan 2017 in National Assembly:
tukipitisha mambo ya Bajeti na vile pesa zinavyofuatiliwa kuhakikisha kuwa pesa zinaenda kule zinastahili. Asante, Naibu Spika.
view
19 Oct 2016 in National Assembly:
Shukrani sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia Hoja hii muhimu sana. Nataka kumshukuru Mheshimiwa Nooru kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Hili jambo limenitamausha sasa kwa kiasi cha wiki nzima. Nimehuzunika kusikia na kuona jinsi watu wanavyoteseka katika kaunti yangu ya Kwale. Hili jambo halijaanza jana, juzi wala wiki jana. Hii mvua ilipoanza miezi kadhaa iliyopita ilikuwa chache sana na kulikuwepo na dalili ya ukame. Kuna akina nyanya ambao hawajawahi kuenda shule lakini walitabiri kwamba mwaka huu kutakuwepo njaa. Itakuwaje wataalamu ambao wameandikwa kazi na Serikali hawawezi kujua kama huu mwaka kungekuwa na ukame? Hivyo, ...
view
19 Oct 2016 in National Assembly:
Shukrani Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nafikiri sikosei kwa sababu kama Mheshimiwa angekuwa anaelewa Kiswahili vizuri angejua kuwa nimesema chama cha ODM na wala si chama cha ODM pekee ndicho kilitetea ugatuzi. Tulikuwa katika msitari wa mbele katika kutetea ugatuzi. Naomba pia niongezee dakika moja kwa sababu nimekatizwa na haya mambo ni muhimu
view
19 Oct 2016 in National Assembly:
Asante sana. Jambo lingine ni kwamba kaunti wamesema watachimba yale madimbwi ya maji lakini mpaka sasa kuna madimbwi mengi kama huko Kaunti ya Kwale ambayo hayajachimbwa. Unajua mchanga huo unarudi ndani na hawajakuja kuutoa katika miaka minne na wala hawajachimba lile dimbwi likawa linaweza kubeba maji mengi kusaidia watu. Jambo lingine, nataka kutumia hii nafasi kuwaeleza wananchi kuwa huu ndio wakati wa kujua kiongozi anayekujali, maanake hakuna kiongozi mzuri ambaye atakubali watu wake wafe, rasilmali zao zife ama ziharibike na watu waishi kwa dhiki kama hiyo ya kuwa hakuna chakula na hivi sasa pia hakuna maji ya kunywa. Nataka kuomba ...
view
10 Aug 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuchangia Mswada wa kusitisha hongo. Tunapopitisha sheria hapa Bungeni, tunaomba kuwa viungo vya Serikali vinavyohusika vitahakikisha kuwa sheria hizi zinafuatwa. Serikali inafaa kufanya kazi yake hususan vitengo vya polisi na usalama na kile kinachokabiliana na ufisadi kuhakikisha kuwa sheria hizi zinafuatwa. Sheria hizi zikifuatwa, ufisadi utaisha. Mwananchi wa kawaida hawezi pata huduma za afya, ambazo ni haki yake, ilhali analipa ushuru. Kule hospitalini, inabidi mtu atoe hongo ili aweze kuona daktari. Ni jambo la kusikitisha sana. Tatizo haliko hapo peke yake lakini liko katika sehemu tofauti tofauti mpaka barabarani ...
view