HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"count": 1608389,
"next": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=153886",
"previous": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=153884",
"results": [
{
"id": 1557042,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557042/?format=api",
"text_counter": 471,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Martha Wangari",
"speaker_title": "The Temporary Speaker",
"speaker": null,
"content": " Thank you. Let us have Hon. Zamzam."
},
{
"id": 1557043,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557043/?format=api",
"text_counter": 472,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kumuunga mkono kwa haraka Mwenyekiti wangu, Hon. Alice Ng’ang’a. Siku ya Ijumaa tuliweza kuwahoji hawa wawili walioteuliwa, CPA Carren Achieng Ageng’o, ambaye ameteuliwa kusimamia Idara ya Ustawi wa Watoto; na Fikirini Jacobs, aliyependekezwa kama Katibu Mkuu katika Idara ya Masuala ya Vijana na Ustawi wa Uchumi Bunifu."
},
{
"id": 1557044,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557044/?format=api",
"text_counter": 473,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Carren alionyesha weledi wa kuweza kuangalia masuala ya watoto. Kama tunavyofahamu katika taifa hili, masuala ya watoto yameachwa kando na hayajazingatiwa vizuri. Kwa hivyo, tulimpiga msasa kwa kuuliza maswali, na aliweza kuyajibu kwa uweledi. Nina imani kuwa wale maofisa watakaofanya kazi chini yake, pamoja na elimu yake, watamuwezesha kufanya juhudi zaidi ili kusaidia watoto. Ni msomi, mjasiri na nampongeza kwa kuteuliwa katika Idara hii."
},
{
"id": 1557045,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557045/?format=api",
"text_counter": 474,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Kuhusu kijana Fikirini Jacobs, tunajua vijana katika taifa hili wamekua na matatizo mengi, mpaka wengi wao wakatoka kuandamana barabarani. Tuliweza kumuuliza na akatueleza kuwa atahakikisha kuwa ataangalia masuala ya vijana. Alituhakikishia kwamba atafanya ubunifu wa nafasi za kazi, na pia kuwaelekeza vijana wote kwenye sekta ambazo watapata huduma katika Idara yake ya Masuala ya Vijana."
},
{
"id": 1557046,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557046/?format=api",
"text_counter": 475,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Pia, Fikirini amekuwa kijana jasiri. Kama mama yake kutoka Kaunti ya Mombasa, ningependa kusema kuwa ni mtoto ambaye ametuinua kichwa juu. Hatukutegemea kuwa anajua masuala ya vijana kwa uweledi. Lakini alivyokuwa akieleza kwa ukakamavu, alitushika nyoyo zetu, kwa sababu tulijua kwamba vijana katika taifa hili wana mtihani mkubwa. Wengi walitoka na kulaumiwa, lakini vijana wamesoma katika idara mbalimbali na kubobea katika The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
},
{
"id": 1557047,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557047/?format=api",
"text_counter": 476,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "masuala tofauti kama uchumi samawati. Hata hivyo, hawajapata mwanya wa kupata ajira wala mtu wa kuwaelekeza."
},
{
"id": 1557048,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557048/?format=api",
"text_counter": 477,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Huyu kijana amefanya mabadiliko makubwa sana ndani ya Kaunti ya Kilifi. Wale vijana wa bodaboda, ambao siku zote wanachukuliwa kama watu wabaya, amewachukua na kuwaweka kwenye Savings and Credit Cooperative Organisation ( SACCO ). Akawaletea"
},
{
"id": 1557049,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557049/?format=api",
"text_counter": 478,
"type": "scene",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "investors"
},
{
"id": 1557050,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557050/?format=api",
"text_counter": 479,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "waliokuja na kuwapa mbinu za kuwekeza. Kwa sasa, SACCO hiyo ya Kilifi imebobea katika sekta ya bodaboda Kenya nzima kwa sababu ya akili ya kijana mdogo, Fikirini Jacobs. Yale maneno aliyokuwa anazungumza na Chairman wangu aweze kukubali, tulikuwa na raha mpaka tulikuwa twaonelea kumwambia kuwa awache maswali mengine, isipokuwa ni ule mwelekeo ambao tulikuwa nao kuwa lazima tuyamalize maswali yote. Nampongeza sana Bw. Fikirini Jacobs. Nakuombea Mungu akuelekeze katika kazi hii ili uinue vijana wa Kenya. Na si yeye pekee yake, niliona pia yule Bw Makokha, ambaye amepewa State Department for Economic Planning, The National Treasury and EconomicPlanning amesoma na kubobea. Amesema kuwa atahakikisha kuwa ataweka sheria ambazo zitahakikisha madeni ambayo Kenya imekopa yanalipwa kwa wepesi. Nikimalizia, nachukuwa fursa hii kumshukuru Rais wa taifa hili, Dr William Samoei Ruto, kwa kutoa mwanya wa Broad-Based Government ili waweze kuleta akili ambazo zimebobea na zinazoweza kuendeleza hili taifa mbele. Nampongeza sana kwa kuchukua kijana wetu wa Kigiriama. Tulikuwa tumeachwa nyuma, lakini mara hii, Mama Zamzam ninatabasamu na kusema Bw. Fikirini atainua Wagiriama, Pwani na vile vile Kenya nzima. Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Nawatakia kila la heri."
},
{
"id": 1557051,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557051/?format=api",
"text_counter": 480,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Martha Wangari",
"speaker_title": "Spika wa Muda",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Zamzam, haujamalizia."
}
]
}