HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"count": 1607048,
"next": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=160698",
"previous": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=160696",
"results": [
{
"id": 1625162,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625162/?format=api",
"text_counter": 377,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kuna mambo ambayo siyo mazuri kufanya katika kaunti zetu, bado sisi wanatuchukulia to kama bwege. Siku inafika wakati watakuja kuingia kumi na nane zetu. Na ndipo wengi wakilia kuwa wanapigwa swaga."
},
{
"id": 1625163,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625163/?format=api",
"text_counter": 378,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Maneno tunayoongea hapa na wakati tunaotumia tunafaa kuwa tunasikizwa. Nilisema hapo kitambo sisi ni kama mashine inayobomoa misitu ikijenga barabara baadaye inasemekana iwekwe juu ya lori isiharibu barabara na tumesema iwe hivyo. Tunafaa jambo kama hili tulizingatie and tulizungumzie. Hata kama ni kupitisha pesa kwanza tuangalie kama kuna matumizi mabaya. Siwapi magavana wosia. Mimi sio mnasimu lakini ninayoongea hapa ninajua wale walionituma hapa pia wanasema vivyo hivyo. Ukiagalia ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha, utapata ya kwamba fedha nyingi zinazopotea ni kwa mabango yanayowekwa picha. Nikiona picha ya gavana imewekwa katika bango huwa inanikumbusha kwamba katika duka unapotaka kuua mbu, utapata kuna dawa inayoitwa Doom amabayo huwa imechorwa mbu. Inaenda kuua mbu bali haina manufaa kwa mbu Haya mabango yanayowekwa na magavana katika mendeleo yanayofanyiwa mwananchi kwa pesa za umma haimaanishi kuna mambo mazuri yanayofanyika katika kaunti zetu. Gavana anapoletwa hapa kwa sababu hafuati tunayosema ashajua kwamba dunia ni gunia tofauti ni herufi moja anaanza kulia eti anaonewa na mengine."
},
{
"id": 1625164,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625164/?format=api",
"text_counter": 379,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mstahiki Spika wa Muda, mimi ni Mlokole. Ninaamini sijafanya mambo mengi kuwa malaika lakini ninajua sijakosea sana kuwa ibilisi. Ndipo wakati mwingi katika maombi yangu huwa ninamwambia Mungu atuepishe na bangi na viroba vya ugoro kwa sababu maneno yanayofanywa wakati mwingine na viongozi hata wewe huwezi kuyafikiria."
},
{
"id": 1625165,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625165/?format=api",
"text_counter": 380,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Unapita katika shedi za boda boda, kitu cha kwanza kuona ni picha kubwa ya gavana. Bila kupoteza wakati, ningependa kuwaambia wananchi walio katika kaunti kwamba ukiona bango limewekwa mahali hiyo ni kumbusho kwamba kuna kitu kimeibiwa."
},
{
"id": 1625166,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625166/?format=api",
"text_counter": 381,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hebu nitoe falsafa moja ya bweha na simba. Wakati mmoja simba alimshika bweha na akamwambia, “nitakukula kama hutaniletea kitu chingine cha kula.” Bweha akasema, “nitakuletea, tena kikubwa utakachokula siku mbili au tatu.” Bweha alienda kwa punda na kumwelezea kwamba simba na wanyama wote walikuwa wamekubaliana kwamba punda ndiye kiongozi na kwa hivyo, alikuwa akiitwa na simba."
},
{
"id": 1625167,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625167/?format=api",
"text_counter": 382,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Alipofika kwa simba, jambo la kwanza ni kumrukia na kumg’ata mkia. Mkia ulikatika na punda akakimbia akipiga mayowe. Alifuatwa na bweha na kuambiwa, “kwani wewe ni baradhuli. Mbona unakimbia? Simba amekukata mkia uli uweze kukalia kiti cha enzi. Huwezi kukalia ukiwa na mkia.”"
},
{
"id": 1625168,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625168/?format=api",
"text_counter": 383,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Punda kwa upumbavu wake alirudi kwa simba aliyemrukia mara ya pili na kumkata masikio. Alitoroka tena akipiga mayowe akifuatwa na bweha. Mbwega akamwuuliza, “wewe mjinga? Hujui simba amekukata masikio ili ile kofia ya enzi iweze kutoshea katika kichwa chako?”Mwishowe, punda aliporudi aliuawa na simba."
},
{
"id": 1625169,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625169/?format=api",
"text_counter": 384,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Simba alimwambia bweha, “sasa kwa sababu umwefanya kazi yako nenda kamchinje halafu uniletee maini, moyo na aliki yake nile.” Bweha alipoenda kuchinja punda alikula akili yote akaleta ini na moyo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
},
{
"id": 1625170,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625170/?format=api",
"text_counter": 385,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Simba alimwuuliza, “mbona hukuleta akili? Bweha alimwuuliza, “wewe mfalme, unaona huyu punda alikuwa na akili yoyote. Angekuwa na akili, angerudi mara mbili baada ya kukatwa mkia na masikio?”"
},
{
"id": 1625171,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625171/?format=api",
"text_counter": 386,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kuna mambo ambayo watu wanaambiwa na wengi wanapiga makofi katika kaunti zetu kwa sababu wanaona kana kwamba kazi imefanyika, lakini huwa wanachukuliwa rahisi kama bei ya chumvi. Bw. Spika wa Muda, hebu niongee kidogo kuhusu sheria ambazo zinatoka mahali kwengine ukiniruhisu kwa sababu zinaambatana. Tunafaa kuwa wangalifu wakati tunapopitisha sheria, iwe ya gavana ama yoyote ile. Ukiangalia sheria zingine saa hii, unaanza kuweweseka na nywele shingoni zinaanza kuamka. Wakati tunapopitisha sheria zinazoenda kutumika, lazima tuwe tumefanya sample. Kwa nini nasema hivyo? Sheria zinapokuja hapa ni kama msumeno. Msumeno hukata mbele na nyuma. Kwa hivyo, wakati tunapopitisha sheria, tunatia makali msumeno. Tunasahau kwamba huenda siku moja ule msumeno ukaja kukata msitu tunaojificha kama viongozi, tuachwe tukionekana uchi na kila mtu. Mwaka 2012, kuna sheria iliyopitishwa inayoitwa kwa kimombo, “Prevention of Terrorism Act (POTA)”. Sikuwa katika Bunge hili wakati huo. Kuna zingine zitaendelea kuja na kuna zingine najua nishafika hapa. Lazima tujue kwamba zile sheria tunazopitisha zitatumika inavyofaa . Leo nimetoka mahali ambapo kuna watoto 11 chini ya miaka 17 na jaji ameamua kwamba wanafaa kuachiliwa, lakini wamewekwa pamoja na watu wazima. Sheria rahisi zinazofaa kufuatwa zinatutia aibu. Unashangaa anayetuma watoto wadogo wawekwe pamoja na watu wazima, hajui kwamba kuna sheria kuhusu watoto? Ni vizuri tuwe makini tunapopitisha sheria hata kama tunasema zichungwe. Nikimalizia, kipofu anapoanza kuona, kitu cha kwanza kutupa ni ule mkongojo alioutumia kwa miaka mingi wakati alikuwa haoni. Tunapofanya kitu cha maana kama kupitisha fedha na kufikia maridhiano, wa kwanza kutemwa ni sisi Maseneta. Kwa nini tunatemwa ilhali tumepewa kila kitu? Kweli tunabweka vilivyo, lakini ni lini tutaanza kuuma? Hilo ndio swali kubwa. Kwa sababu leo tunaongelea hili, tutajadili lile. Ukienda nyumbani, utakutana tu na picha za magavana kila mahali. Nimeuliza swali hapo awali, kama maendeleo ni maendeleo, kwa sababu kuku ni kuku, jogoo ni jina, kwa nini hawaweki picha zao katika makafani, kwa kimombo, “ mortuary” ? Kwa nini hawaweki picha zao huko, wanachagua tu mahali wamejenga daraja na barabara? Barabara inapotengenezwa na kuwekwa hicho kibandiko kikubwa, ikiharibika mwaka ujao, hawaweki picha zao kwa kile kibandiko walichoweka hapo awali. Wanaweka kingine cha pili pale pale. Unaona kuna ubadhirifu na tunapoteza pesa nyingi sana. Ningeomba magavana, kama kuna ulazima wa kuweka picha zao, waweke kwao nyumbani. Huko ndio muhimu. Utendakazi wa Serikali Kuu na ugatuzi si mapenzi. Kama unataka kuweka picha, weka kwa whatsapp ama uende uzitume kwa mtu anayekupenda. Baadhi yao kweli wako na sura nzuri, lakini kuna wengine pia wako na sura nzito na wanalazimisha kuweka picha zao katika miradi ambayo hawafai kuonekana. Kuna mmoja ana sura nzito kama ule uji unaopewa wanawake wa martenity. Unapata alijenga The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}
]
}