Abdulswamad Sheriff Nassir

Parties & Coalitions

Post

PO BOX 16735, Mombasa, Kenya

Email

asnassir@radiorahma.co.ke

Link

Facebook

Telephone

0722333109

Telephone

0737333109

Link

@Asnassir on Twitter

All parliamentary appearances

Entries 211 to 220 of 1018.

  • 25 Mar 2021 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika. Kupitia Kanuni za Kudumu za Bunge 218(2), naomba upeane amri kwa Kamati husika ya Nishati alimaarufu Energy na Kamati ya Sheria za Kukabithiwa alimaarufu Delegated Legislation waweke uchungunzi wa Pamoja kuhusu mikakati inayotumiwa na Energy and Petroleum Regulatory Authority (EPRA) kuweka bei za jumla na rejareja za mafuta, ikiwa hawaja fahamu petroli katika nchi hii yetu. view
  • 25 Mar 2021 in National Assembly: Sote tunakubaliana yakuwa hamna uchumi uliostawi katika nchi yoyote, isipokuwa bei ya mafuta iwebei iliyotulia. Bei zimetulia licha ya bidhaa kuzidi ama kupungua na wala sio masoko ya mafuta kuingiliwa na ujanja. Tunawasiwasi kwa sababu petroli na bidhaa zake zimepanda kwa bei haijawahi onekana katika nchi hii kwa muda wa miaka tisa. Leo lita moja ni takriban Ksh122. Ni aibu kwangu. Mwisho wa bei hii ulikuwa November 2011. Hii kupanda bei bila mipangilio imeadhili bei ya chakula, usafiri, utengenezaji wa bidhaa na bei ya kila kitu kwa jumla imepanda. Wakenya wanaumia na hawawezi kujimudu kimaisha. Wengi wanahisi ikiwemo walioko katika ... view
  • 25 Mar 2021 in National Assembly: Bei kupanda zaidi za petroli ni vigezo ama parameters zinazotumiwa na EPRA ambazo hazieleki, hazikosawa na hazina mpangilio. Mpaka bei ya mafuta hapa Kenya iko juu na hailingani na bei za nchi zingeni katika dunia nzima. Ili Wakenya waweze kupunguziwa mizigo ya bei ya mafuta naomba uwelekezo wako kupitia kwa Kanuni za Kudumu za Bunge 218(2): (a) Kwanza, kamati hizi mbili zichunguze na kuingilia kwa undani EPRA kuangalia njia za kubadilisha viegezo vilivyowekwa na Energy (Petroleum Pricing) Regulations 2010 na the Energy, (Petroleum Pricing) (Amendment) Regulations 2012. (b) Ningeomba kwa unyenyekevu kwa niaba ya Wakenya wasizidi siku 30 waweze kurejea ... view
  • 11 Mar 2021 in National Assembly: Actually, Hon. Deputy Speaker, this is something that might interest the petitioners and those supporting the same. After the whole Kenya Medical Supplies Agency (KEMSA) thing, we are planning to table a report regarding Galana- Kulalu. I am aware there is the element of land, and the land from the ADC has since been transferred to the National Irrigation Board (NIB). So, there is quite a lot. Maybe if they wish, they could provide some of this information to us. Land ownership is subject to audit in all our audit reports. view
  • 11 Mar 2021 in National Assembly: Mheshimiwa Naibu Spika, nilipopata jawabu hii jana, niliwasiliana na familia. Nasikitika kuwa dadangu amepewa karatasi asome lakini sivyo ilivyo. Kwanza, majina yaliyo hapa si yale niliulizia. Pili, ikiwa ni wizi, tujaribu kuwaza. Fedha ambazo zinazunguka katika duka lile hazipiti hata Ksh20,000. Watu waliingia na AK-47 kuiba kutoka kwa duka ndogo sana la M-PESA. view
  • 11 Mar 2021 in National Assembly: Tatu, kama ni kweli uchunguzi unafanywa mpaka leo, Statement ya Sadat haijachukuliwa. Viongozi wa Wizara hawajui kile ambacho wanachokizungumza. Wamesema kwamba wale ambao walimiminiwa risasi walipelekwa hospitali ya Coast General ambayo ni uongo. Hawakupelekwa huko, Mhe. Naibu wa Spika. Wale waliathirika walipelekwa katika hospitali ya Memon ambayo iko karibu. Baada ya hapo, walipelekwa katika hospitali ya Aga Khan. Wametaja hapa kuwa kuna namba ya Occurrence Book (O.B). Lakusikitisha ni kuwa hakuna mmoja wa wale wanafanya kazi katika eneo hilo, waliopigwa risasi ama familia zao ambao Statement yao zimechukuliwa. Licha ya hivyo, walijipeleka kusema kuwa wanataka kupiga ripoti ya masuala haya. ... view
  • 11 Mar 2021 in National Assembly: Mwishowe nikimalizia, kuna huu mwenendo wa Katiba 2010 ambao Waziri anaandika ripoti, kisha anampelekea Mjumbe kuisoma. Nasikitika itabidi waregeshe tena suala hili ili wajue ukweli. Mwisho, wamesema post-mortem ilifanywa. Hakuna post-mortem yeyote ilifanywa kwa marehemu. Kwa hivyo, nasikitika kwa sababu itabidi dadangu ambaye yuko katika Kamati ambayo inahusika arejee tena kuambia Serikali kuwa kuna kiwango ambacho watu wanaweza kuhadaiwa. view
  • 18 Feb 2021 in National Assembly: Thank you very much, Hon. Speaker. I will not comment on what you have just talked about because these are my colleagues, but I think we should raise these matters in the Liaison Committee. Back to the Statement. view
  • 18 Feb 2021 in National Assembly: Thank you very much, Hon. Speaker. I will not comment on what you have just talked about because these are my colleagues, but I think we should raise these matters in the Liaison Committee. Back to the Statement. view
  • 16 Feb 2021 in National Assembly: Asante sana Bw. Spika. Kwanza, kwa niaba yangu na ile ya Wanamvita, ningependa kutoa pole kwa familia na jamii ya Mhe. Oroo Oyioka ambaye alikuwa Mbunge wa Bonchari na ile ya Marehemu Mohamed Yusuf Haji ambaye alikuwa Seneta wetu. Kibinafsi, ningependa kutoa pole zangu kwa wanawe Abdul na Noordin. Bw. Spika, mengi yameweza kuzungumzwa katika Jumba hili lakini kuna mafunzo ambayo vifo hivi vinafaa kutufunza sisi. Kwanza, hamna ambaye ana mkataba na Mwenyezi Mungu ni lini ataenda mbele ya haki. Haya mambo ya watu kujigamba kuhusu 2022… Ikiwa kuna lolote mwanasiasa anapaswa kujifunza na vifo hivi ni kuwa yeyote anaweza ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus