Abdulswamad Sheriff Nassir

Parties & Coalitions

Post

PO BOX 16735, Mombasa, Kenya

Email

asnassir@radiorahma.co.ke

Link

Facebook

Telephone

0722333109

Telephone

0737333109

Link

@Asnassir on Twitter

All parliamentary appearances

Entries 231 to 240 of 1018.

  • 10 Nov 2020 in National Assembly: Tulisema na tukatoa maoni, na ninashukuru yamekubaliwa, kuwa ile ardhi - hamna shirika lolote la Serikali katika Kenya lenye ardhi zaidi kama Shirika la Reli la Kenya - ichukuliwe na fedha ambazo zinatumiwa kiholela holela zitumike kulipa madeni ambayo yalichukuliwa. view
  • 10 Nov 2020 in National Assembly: Baada ya kuzungumza, mimi binafsi, Wabunge wenzangu, Mwenyekiti na washikadau tulikubaliana ya kwamba ikiwa mtu anataka kutumia reli, badala ya kulipa asilimia 2 kama view
  • 10 Nov 2020 in National Assembly: apunguziwe iwe asilimia 1.5. Na ikiwa ni lazima atumie gari kwa sababu ya hiari yake, basi aongeze kwango cha 0.3. Ukiangazia zile hesabu, wenye biashara walikubaliana na jambo hilo. view
  • 10 Nov 2020 in National Assembly: Tulisema ni sawa ikiwa SGR inaona inatatizo la kupeleka mizigo kutoka yadi yao mpaka katika sehemu za wenyebiashara, ni sawa wazungumze na washikadau ambao ni wasafirishaji wakubaliane nao kuwa mizigo ikiingia, mtu ana hiari ya kutumia njia anayetaka ili mizigo ifike katika yadi yake. Zamani kazi za clearing and forwarding zilikuwa zimejaa Mombasa. Leo kwa sababu ya amri hii, biashara zote za clearing and forwarding zimeenda kwingine. Lakini tunakubaliana na nashukuru kuwa mtu awe na hiari ya kuchagua Container Freight Station anayoitaka na aweze kuwa na hiari ya kuchagua kampuni ambayo anataka. view
  • 10 Nov 2020 in National Assembly: Jambo hili si la Kenya peke yake. Nchi ya Ethiopia ilifanya jambo hili. Napendekeza Serikali iregee chini ianze kuzungumuza na Serikali ya China wakubaliane vile mikopo itakavyolipwa. Tumegundua kuwa gharama kuu zaidi ya kuendesha SGR ni malipo kwa kampuni fulani kila mwezi ya takribani bilioni. Ni lazima waangalie njia kwa sababu Wakenya wanaumia na pesa zinaenda kwa shirika fulani peke yake. view
  • 10 Nov 2020 in National Assembly: Nashukuru Mwenyekiti mwenzangu na nashukuru washikadau. view
  • 10 Nov 2020 in National Assembly: Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nilikuwa namalizia kwa kusema kuwa namshukuru Mwenyekiti na Wanakamati. Tulipoanza jambo hili kulikuwa na mvutano na bugudha sana. Nawasihi ndugu zangu wanaopendelea “ bonga points ” za mitaani kwa kuzungumza tu na kutoa kashfa ambazo hazina ukweli, kuwa leo pengine iwe funzo tunawapa jinsi sheria zinatungwa. Tumefaulu leo na nina imani kila mmoja amekubaliana na kauli yetu kuwa ni lazima SGR isiwe ya kulazimishiwa mtu bali iwe hiari kwa sababu wanaona inafaa. view
  • 10 Nov 2020 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda. view
  • 13 Oct 2020 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. I am glad that the Leader of the Majority Party has said I will be glad to be here. Usually, I am someone who is active and I do not mind being here, but that will be at your discretion. I was not consulted, but I will respect the Standing Orders and the position of the Leader of the Majority Party on this matter. The Chair who is about to move his Motion informs me that his is an issue of replying. I know the international issues in his Report. I plead with the House leadership ... view
  • 13 Oct 2020 in National Assembly: Hon. Speaker I beg to move: view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus