17 Feb 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninataka kutoa pongezi kwa Mswada huu ambao umeletwa katika Bunge. Huu ni Mswada ambao unatekeleza masharti ya Katiba ya Kenya kulingana na vipengele 19(2), 48, 50(2)(g) na (h). Katiba ya Kenya inaeleza wazi kuwa kila Mkenya ana haki ya kupatiwa msaada katika masuala ya kisheria. Pia, ni muhimu Serikali iweke jopo litakalosaidia wasiojiweza katika masuala yanayohusiana na mahakama. Historia ya Kenya inaelezea wazi wakenya wamefungwa kwa muda wa miaka, na wote kwa sababu wamekosa uwakilishi katika mahakama. Ukiangalia watoto na akina mama utakuta kwamba wamepata dhuluma za aina tofauti kwa sababu hawana watu ...
view
17 Feb 2016 in National Assembly:
kutoka kwa Serikali. Lakini kuna umuhimu wa kupata uwakilishi wa vijana na akina mama katika bodi hii.
view
17 Feb 2016 in National Assembly:
Yangu yatakua ni hayo. Tutaleta maoni yetu na fikira zetu ili tuweze kubadilisha Mswada huu, ili ukipita uwe ni kwa minajili ya wakenya vile inavyostahili.
view
17 Feb 2016 in National Assembly:
Asante sana kwa nafasi hii, na nina imani kuwa wenzangu vile vile wataweza kuunga mkono.
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Wenzangu wa upande ule wa pili walikuwa wananiita niende upande ule lakini Wakenya wangeona nimewasaliti na ikawa ni bora nikae huku. Ninakubaliana na utaratibu wa mwendo ambao umeletwa, kwa lugha maarufu ya Kiingereza “ Procedural Motion”, ili kuweka muda wa ambao utahakikisha kila mmoja ananafasi ya kujadili na kutoa maoni yake katika maswala haya. Hili ni jambo ambalo halitasaidia Bunge hili peke yake, lakini pia litaweza kusaidia Wabunge wajao watakaokaa katika viti vivi hivi na watakaozingirwa na kuta zizi hizi. Wengi wameyazungumzia mambo haya. Ninaomba unipatie fursa na wenzangu wanipatie fursa nitaje hili ...
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
ambayo uliitoa wakati ule ulikuwa unaomba kura. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
Japo tunazungumza, na ninaskitika kuwa tumelifanya hili jambo likawa ni la kubinafsishwa, kwamba mtu fulani ametolewa katika kamati, wale wengine watakaoingia katika zile kamati, hawawezi kulifanya lile jambo. Kuna tatizo gani ikiwa wataweza kulifanya na waifanye ile kazi kwa njia mwafaka na inayofaa. Ninajua wenzangu hapa hupenda sana kwenda nyuma ya zile kanuni na sharia za Bunge wakiona fikira na akili zimewashinda. Hupenda kuenda nyuma na kuyatumia yale maswala ya nidhamu na mambo mengine kama vile anavyofanya.
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
Inafaa tuwe ni wenye kuhoji kwa akili. Tukiwa tunazungumza kuwa tuna njia na tunataka watu wawe katika kamati waweze kupendekeza matakwa ya wakenya, tuachieni kwa sababu sisi ni sauti ya wakenya. Hatuko hapa kuzungumza sauti ya mtu mmoja, bali ni sauti ya wakenya ndio inazungumzwa hapa.
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninakubaliana, lakini pengine unaweza kutupatia mwelekeo wa lugha mwafaka inayofaa kutumika kwa sababu “huelewanga” ama lugha kama hii sijui kama ni Kiswahili. Tuzungumzeni Kiingereza au Kiswahili.
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view