29 Apr 2015 in National Assembly:
Nataka kuunga mkono na niseme kwamba ni jukumu letu sisi wote tuhakikishe kwamba Wabunge wenzangu Mswada huu umepita, upite na tuweze kuwa na sheria mwafaka ambayo itatusaidia sisi kama wazazi, na pia kama viongozi kutoka mashinani.
view
29 Apr 2015 in National Assembly:
Asante sana, mhe Naibu Spika wa Muda.
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, mhe. Spika. Nimesimama nikukumbushe tu kwamba ndani ya Bunge hili kuna wabunge akina mama maanake tumeona mtiririko wa wabunge wenzetu; kufikia sasa kama kumi wameongea na akina mama tumebonyeza lakini hatujapata nafasi. Asante.
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, mhe. Spika. Nimesimama nikukumbushe tu kwamba ndani ya Bunge hili kuna wabunge akina mama maanake tumeona mtiririko wa wabunge wenzetu; kufikia sasa kama kumi wameongea na akina mama tumebonyeza lakini hatujapata nafasi. Asante.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kwa jambo la nidhamu. Kwa ajili ya umuhimu wa Hoja hii ambayo inaendelea kuzungumzwa, ningeomba tupunguze muda. Badala ya kuwa dakika kumi, ziwe angalau dakika tano ili kila mmoja aweze kuzungumza. Asante.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kuichukua nafasi hii kwanza nimpongeze Mhe. Lay kwa kuileta Hoja ambayo ni muhimu sana katika taifa letu la Kenya na katika Bunge hili kwa jumla. Wakenya waliandika historia tarehe 27/8/2010 kwa kupitisha Katiba ambayo ni mwongozo katika taifa hili letu la Kenya. Lakini, Wakenya wengi kuhakikisha kwamba Katiba inawalinda, lazima waifahamu. Lugha ambayo inafahamika kwa urahisi na wananchi wengi katika taifa hili ni lugha ya Kiswahili. Hakuna mtu ambaye anaweza kujivunia Kiswahili na kusema ni lugha yake. Ni lugha ambayo imetumika katika taifa hili na 1974, ilitangazwa rasmi kuwa lugha ya kifaifa. Inatumiwa ...
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Mataifa mengi ambayo yameendelea katika dunia ni yale ambayo yameandika sheria zao katika lugha ambazo zinazungumzwa kwa wingi katika mataifa yao. Nasisitiza na kuunga mkono ya kwamba sheria na Katiba katika Jamhuri yetu ya Kenya iandikwe na kutafsiriwa kwa Kiswahili.
view
14 May 2013 in National Assembly:
(Hon. (Ms.) Katana): Mhe. Naibu Spika, mimi ni mheshimiwa Aisha kutoka Kilifi. Kwa vile ni mara yangu ya kwanza, naomba uniruhusu niwapongeze watu wa Kilifi kwa kunichagua ili niwaakilishe katika Bunge hili la Kumi na Moja. Nimesimama kuunga mkono orodha ya majina. Nimeipitia Ripoti hii kwa uchache na nikaona kwamba walioteuliwa wana tajriba na taaluma ya kutosha kuendesha Wizara walizotengewa. Kuhusu suala la ukabila, nafikiri Katiba imeangazia hilo jambo katika Kipengele cha 152 (d); kwamba si chini ya Mawaziri 14 na si zaidi ya 22. Katika taifa letu, tuna makabila 42. Wenzangu waliozungumza awali wametaja kwamba kuna ugumu fulani unaojitokeza. ...
view
14 May 2013 in National Assembly:
(Hon. (Ms.) Katana): Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunitetea. Nikimalizia, uteuzi huu umezingatia kanuni za Katiba zinazoangazia usawa wa jinsia. Mheshimiwa Rais na naibu wake wameangalia sana suala hilo na wamewapa nyadhifa kina mama ambao wana uwezo kama sisi katika utenda-kazi. Kwa hayo---
view
14 May 2013 in National Assembly:
(Hon. (Ms.) Katana):: Hapana,
view
14 May 2013 in National Assembly:
Kwa hayo, naunga mkono orodha hii ya Mawaziri.
view