Aisha Jumwa Katana

Parties & Coalitions

Email

skcharo@yahoo.com

Telephone

0712055922

Telephone

0703176492

All parliamentary appearances

Entries 101 to 110 of 131.

  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu wa marekebisho. Ni wajibu wa kila mmoja kuwa katika uongozi. Akina mama wameshindwa kufika kwenye Bunge la kitaifa na kwenye mabunge mengine kule nyanjani kwa sababu ya ukosefu na udhaifu wa kiraslimali. Kwa hayo machache, naunga mkono. view
  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii kwanza nimpongeze Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge hili la Kitaifa kwa sababu ya Mswada huu tunaendelea kuujadili. Nauunga mkono kwa sababu ya marekebisho ya kikatiba ambayo tunaenda kuyahitimisha tutakapofika tarehe 27. view
  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Kenya ni nchi ya kidemokrasia na pia vile vile ina mashirika mengi sana ya kijamii ambayo yamekuwa na mchango mkubwa sana katika Mswada huu kwa kuitekeleza marekebisho haya ya kikatiba. view
  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Bunge la 10 lilikuwa na wakilishi wa jinsia ya kike asilimia 9.8. Bunge la 11 lina asilimia 19.1 ambayo ni asili mia ya chini sana tukiilingasha na majirani wetu katika Afrika Mashariki. Rwanda inajivunia asilimia 63.8 baada ya uchaguzi mwezi wa tisa 2013. Tanzania vile vile vile inajivunia asilimia 36 baada ya uchaguzi uliofanyika mwezi wa kumi 2010. Uganda inajivunia asilimia 35 na Burundi asilimia 30. Hii imetufanya sisi Wakenya kuonekana kurudi nyuma na imefanya nchi ya Kenya kuorodheshwa 78 ulimwengu kwa uakilishi wa Wabunge wa jinsia ya kike kwa Bunge mwaka 2014. view
  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Hata hivyo si jambo ambalo limekuwa rahisi. Nawapongeza vinara wetu wa muungano wa CORD. Tulipokutana kujadili swala hili, waliliunga mkono na kudhirisha ya kwamba wako tayari kuunga kina mama ama jinsia ya kike ndani ya uongozi. view
  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Nataka nizungumzie historia ambayo imetufanya wengine wetu tumepata fursa hii kuingia katika Bunge. Haijakuwa rahisi vile. Nilichaguliwa kama mwakilishi wa Wadi 1998 hadi mwaka wa 2007. Nilijaribu kutafuta kiti cha ubunge lakini haikuwa rahisi katika eneo la Bunge la Bahari ndani ya Kilifi Kaunti. view
  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Nawapongeza sana waliokuwa katika Bunge la 10, wote katika jinsia ya kike na kiume kwa sababu ya kuleta na kuibadilisha Katiba ambayo imetupa fursa hivi sisi tunaongea hapa tukiwa tumeingia viti vile 47 maalum vilikiwa vimetengwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Litakuwa ni jambo la maana katika Bunge hili la 11 tutakapoitekeleza Katiba maanake ni jukumu letu kuhakikisha kwamba imefanyika na tumeitekeleza kwa mujibu wa Katiba inavyotuamurisha. Tayari hii inafanyika. Katika kipengele cha 27(3) cha Katiba yetu ambayo ilipita 2010, inaelezea usawa wa jinsia zote kiuchumi, kisiasa na kijamii. Tayari hii inafanyika katika bunge zetu za kaunti. Kikatiba katika Kitengo cha 177(1)(b) na (c) katika bunge za kaunti tayari hii inafanyika. Hivyo basi ni uhamisho tu ili ifae katika bunge zetu za kitaifa katika kitengo cha 97 na 98. view
  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Kina mama ama jinsia ya kike katika taifa hili na katika ulimwengu mzima si kitu ambacho kinaweza kuangaliwa na jicho moja likiwa limefungwa. Tumeona nchi ambazo zimestawi na zile zimeendela, na Kenya ni moja kati ya zile ziliorodheshwa, zimepata kupiga hatua lakini tunajivuta nyuma kwa sababu ya kukosa uakilishi wa jinsia ya kike. view
  • 21 Apr 2016 in National Assembly: Naunga mkono kina mama kupata nafasi hasa sana katika vyama vya kisiasa. Tuige mfano katika muungano wetu wa CORD kwa sababu naona wengi walipata nafasi bila upendeleo. Kwa hivyo, vyama vya kisiasa vizingatie na kuangalia maadili ya akina mama na kuwapa nafasi. Badala ya kupewa viti maalum tuwe tunang’ang’ana kama vile naelekea Malindi. Nina hakika ya kwamba nitakuwa Mbunge wa kwanza kurudi hapa nikichaguliwa katika eneo moja la bunge la Malindi. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus