21 Apr 2016 in National Assembly:
Nawapa changamoto wenzangu ambao tumechaguliwa katika viti hivi maalum ya kwamba tumestawi ya kutosha. Tunaweza kuingia katika nyanja hii kung’ang’ana na wanaume. Nataka niwapongeze akina Millie Odhiambo, Cecily Mbarire, Dr. Laboso na Shebesh waliokuja hapa kama wateuliwa. Lakini waliporudi kila mtu aliingia katika eneo bunge na tumeona wamerudi hapa. Kwa hivyo wale mama 47, badala ya kungoja na kuzizuilia zile nafasi kwa wanawake wengine katika jamii na katika taifa hili, tujitoe na tutafute kwa sababu vile anafanya mwanaume hapa Bungeni sisi tunaweza kufanya zaidi. Tumewashinda sana. Si Mary Wambui peke yake vile, Mhe. Chris amesema. Wako wengi ambao wamewashinda hawa ...
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Naona tuna uwezo na tunawezafanya. Naomba siku ya Jumatano tujititokeze kwa wingi Wabunge wa kike na kiume tupitishe kwa sababu ni suala ambalo ni la maana.
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Asante sana. Naunga mkono.
view
16 Dec 2015 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika. Nachukua nafasi hii kuunga mkono mjadala huu ambao tunaujadili sasa kuhusu uteuzi wa mawaziri. Kwanza, namshukuru sana Rais wa Jamuhuri yetu ya Kenya kwa kuwachagua Wakenya ambao Ripoti ya Kamati ya Uteuzi hapa Bungeni inaonyesha kuwa wana tajriba nzuri na elimu ya kutosha ya kuweza kuongoza katika nyadhifa hizo ambazo Raisi amewatunuku. Mimi binafsi, namshukuru sana Rais kwa sababu ya kumteua ndugu yetu Mhe. Dan Kazungu ambaye alikuwa Mbunge wa Malindi. Tunafurahi sana kama watu wa Kilifi na Wakenya na, hususan, wakaazi wa Malindi. Nimemjua Mhe. Dan Kazungu kama kiongozi. Ni mtu ambaye ana tajriba na ...
view
16 Dec 2015 in National Assembly:
ngazi ya kuwa na wadhifa wa kitaifa. Nampa kongole. Kama alivyosema kakangu Mhe. Midiwo, inaonekana kwamba upande wa kulia wa Spika kidogo una upungufu lakini upande huu wa Upinzani inaonekana kuna watu wenye uwezo wa kusaidia. Wanapotuhitaji sisi bado tuko. Kila la heri Mhe. Dan Kazungu. Sisi tunafurahia na tunakupatia kongole. Nataka niseme kwamba kwa vile tunaenda kwa kinyang’anyiro, tutakuwa pale na mwaka wa 2017, nipo ndani nitachukua mwenyewe. Ahsanteni.
view
1 Jul 2015 in National Assembly:
Asante sana Mhe. Dawood, ama Mhe. Naibu Spika wa Muda ndiye amenipa nafasi. Nataka nichukue nafasi hii kwanza nimpongeze sana Mhe. Dawood pia kwa kunipatia dakika yake moja ili nipaze sauti yangu kuhusu Hoja hii. Nimesimama kuiunga mkono. Nataka kwanza nipongeze pia lile jopo la wataalam ambalo lilikuja na mabadiliko ijapokuwa yameangushwa; niliomba sana wenzangu tuyazingatie kwa sababu maswala ambayo yamezungumzwa ni ya ukweli ili kuhakikisha swala hili limepata uhakika wa kufanyika, na ni lazima tulizungumze kwa upana. Kupata ICU katika kila eneo la uwakilishi Bungeni una ugumu kama vile wenzangu waliotangulia kusema. Pia kuna umuhimu sana watu kuzingatia huduma ...
view
29 Apr 2015 in National Assembly:
Asante sana mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza sana mhe Wangwe kwa kuleta Mswada huu. Tunajua sisi wote kwamba elimu ni mwangaza na ni muhimu sana kwa watoto wetu katika taifa hili. Mhe Wangwe amefikiria si eneo Bunge lake tu, lakini watoto wote katika taifa letu la Kenya.
view
29 Apr 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, nataka kusema kwamba nimesimama kuunga mkono kabisa Mswada huu ambao utakuwa muhimu kwa sababu tumeona Rais wa Jamhuri ya Kenya akitoa amri kwamba malipo ya mitihani yetu ya kitaifa ya Darasa la Nane na Kidato cha Nne yote yaondolewe. Serikali imejitolea kabisa tukipitisha Mswada huu itakuwa ni sheria, na itakuwa ikifanyika bila pingamizi. Hii ni kwa sababu Rais akiongea, ama wakuu wetu wakiongea, ni kwamba bado kuna waalimu ambao ni wakuu wa shule wanaosembea. Kwa mfano, mwaka jana tulimwona Rais wetu pamoja na makamu wetu wakiongea kuhusu vyeti vya watoto wa Kidato cha Nne, kwamba ...
view
29 Apr 2015 in National Assembly:
sana watoto wetu kuhakikisha kwamba wamefanya mitihani bila matatizo na wanapata vyeti bila shida.
view
29 Apr 2015 in National Assembly:
Wabunge wetu wanafanya bidii sana kutumia Hazina za Maeneo Bunge kujenga shule na kupeana bursary . Lakini haya hayana msingi iwapo vyeti havitapeanwa kutoka katika shule mbalimbali katika Jamhuri yetu ya Kenya.
view