11 Apr 2018 in National Assembly:
Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Waruguru. Nampongeza sana kwanza kwa fikira ambayo inaguza kila Mkenya katika taifa letu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
11 Apr 2018 in National Assembly:
Ugonjwa wa saratani ni mmoja katika ya magonjwa sugu ambayo yamehangaisha jamii zetu. Kuna umuhimu ama haja ya ugonjwa huu wa saratani kutangazwa janga la kitaifa. Vile vile kuwe na hazina maalum ambayo itashughulikia maradhi haya ambayo ni mazito sana.
view
11 Apr 2018 in National Assembly:
Wenzangu waliotangulia kuongea ni wataalamu pia katika Jumba hili wametoa sauti zao. Kutokuwa na ufahamu kuhusu vile ugonjwa huu unavyoletwa na nini ama vipi inaanza ni jambo linalochangia pakubwa sana. Wakati ufahamu unapopatikana baada mtu kuzuru vituo vya afya, huwa tayari imeshachelewa. Shirika la Afya Ulimwenguni limetoa takrimu ambazo zinatutia hofu. Ugonjwa huu kujulikana kwa haraka inakuwa ni vigumu. Watu wengi hufaamu kuwa wako na saratani wakati wanatembelea kituo cha afya na kupatikana tayari ugonjwa umeshafika kiasi cha asilimia 70 hadi 80. Kwa hivyo, inakuwa kazi ngumu kuthibithiwa. Yote haya yanatokea kwa sababu ya kutokuwa na ufahamu.
view
11 Apr 2018 in National Assembly:
Kuna sheria ambayo tayari imeshapitishwa kama Cancer Control and Prevention Act,
view
11 Apr 2018 in National Assembly:
ambayo inaangalia masuala ya kuzuia, kuthibithi na matibabu katika taifa letu la Kenya. Lakini sheria kama hizi zimepewa kisogo na Serikali. Hazipewi kipau mbele na hazina ufadhili wa kutosha wa kuziwezesha kulishughulikia suala la kukinga, kuthibithi na hata kutibu saratani. Vipengele vya 4 na 20 vya sheria hii…. Ni vyema sisi kama Wabunge ambao tunaadhiriwa na jambo hili moja kwa moja kwa kuhusika katika michango kusaidia wagonjwa katika maeneo yote kwa njia moja ama nyingine ili wapate matibabu... Majibu tunayoyapata baadaye si ya kuridhisha. Mara vifo vinatokea wakati tumechanga pesa zetu kiasi ili mgonjwa apate matibabu. Ndio maana nataka nimpongeze ...
view
11 Apr 2018 in National Assembly:
Taasisi zilizoko kama Kenya Cancer Registry inatupea tarakimu zinazotusaidia katika mipangilio ya kuhakikisha ya kwamba tunazitengea mgawo wa kutosha ili zihakikishe ya kwamba... Naunga mkono.
view
11 Apr 2018 in National Assembly:
That is my surname.
view
8 Nov 2017 in National Assembly:
On a point of order, Hon. Temporary Deputy Speaker. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
8 Nov 2017 in National Assembly:
Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninaomba nikukumbushe kwamba katika Bunge hili kuna jinsia mbili na sisi sote tuko hapa kama Wabunge. Ninawasihi macho yenu yawe yanaweza kuangazia jinsia ya kike pia.
view