All parliamentary appearances
Entries 381 to 390 of 612.
-
16 Mar 2016 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
-
16 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Kongole Mheshimiwa Mwaura. Zamani zile za kuwaficha na kudhulumu walemavu; zamani zile za kuamini walemavu ni laana, zilipita. Hivi sasa, lazima tuje na mikakati mipya, kama hii ilioletwa na Mheshimiwa Mwaura. Katika Mwada huu, tuwe na sera na sheria zitakazowalinda walemavu na kuwawezesha kupata elimu au kuingia kwa nyumba za ghorofa bila matatizo yoyote. Naunga mkono Mheshimiwa Mwaura.
view
-
16 Mar 2016 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Chairlady, I beg to move:- THAT, Clause 76 be amended by inserting the words “and subject to any variations as may be specified in the Third Schedule to this Act” immediately after the words “Forests Act, 2005—”.
view
-
16 Mar 2016 in National Assembly:
I am convinced, Hon. Temporary Deputy Chairlady. That is on my amendment to Clause 76.
view
-
16 Mar 2016 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Chairlady, I withdraw the proposed amendment to Clause 76.
view
-
16 Mar 2016 in National Assembly:
Thank you. My first amendment has been taken care of by Hon. Amina’s amendment. I, therefore, beg to move:- THAT, the third schedule be amended by- (b) deleting the expression ’29.Bangali 39/2/2013”; and (c) deleting the expression “31. Mbalambala 40/2/2013”. The reason as I earlier said is that the proposed gazetted forest area had not been there from Independence time up to 2013. When they gazetted it on 16th December, 2013 they did this from Nairobi without taking the input of the local communities. In the process they ended up closing the social amenities. I have petitioned Hon. Amina and ...
view
-
2 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Kwanza kabisa, ninasimama kuiunga mkono Hoja hii. Pili, Kenya ilipopata Uhuru, kulikuwa na SessionalPaper No.2 . Sera hii iligawanya Kenya katika sehemu mbili; sehemu ya rotuba na sehemu isiyokuwa na rotuba. Huduma katika taifa imegawanywa kwa msingi wa sera hii. Wakenya wengine wanapozungumza kuhusu utoaji wa kitambulisho, mimi nahisi kulia. Kule kwangu, utapata mama amezaa watoto watano na mpaka leo hana kitambulisho na hawezi kutembea barabarani kwa sababu Kenya Defence Forces (KDF) wako katika kila kona. Kitu cha kwanza watamuuliza ni atoe kitambulisho na si makosa ya yule mama kutokuwa na ...
view
-
2 Mar 2016 in National Assembly:
Nikimaliza kuunga mkono, ninatoa kongole kwa Mhe. Wamalwa kwa kuileta Hoja hii. Hii Hoja ingekuja jana, leo vitambulisho vingetolewa katika Kaunti ya Tana River. Ninasema hivyo kwa sababu mtu anatoa nauli kuja Nairobi na kulipa hoteli kutafuta kitambulisho ambacho angeletewa kule aliko. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii. Asante.
view
-
16 Dec 2015 in National Assembly:
Asante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuiunga mkono Mswada ulio mbele yetu kuhusu uhifadhi wa misitu. Duniani nzima, na Kenya kama nchi, ni muhimu tuhifadhi misitu. Lakini huo mchakato wa kuhifadhi misitu ni lazima uwe na utu na uheshimu jamaa ambao wanaishi katika sehemu hizo. Mwezi wa nne mwaka uliopita nilileta teteze Bungeni juu ya kubadilishwa kwa mpaka wa misitu katika kaunti ya Tana River.
view
-
16 Dec 2015 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu wa Spika. Kwanza, ingawaje ninaunga mkono Mswada huu, nina dukuduku kadhaa. Hektea 123,000 za ardhi katika sehemu ninayowakilisha Bungeni zimechukuliwa. Shule za msingi na zile za upili, pamoja na hospitali, sasa ziko katika sehemu ya msitu. Nilileta teteze Bungeni mwezi wa nne mwaka uliopita. Kamati husika ya Bunge hili ilitumwa huko na kujionea ukweli wa mambo. Kamati hiyo imeleta pendekezo kwamba mipaka ya misitu katika kaunti ya Tana River, na haswa katika sehemu ya Bura, ibadilishwe. Kwa bahati mbaya ama nzuri, Ibara ya 28 ya Sheria ya Misitu, ambayo ilipitishwa na Bunge kabla ya Ripoti ya Kamati ...
view