All parliamentary appearances
Entries 391 to 400 of 612.
-
16 Dec 2015 in National Assembly:
ilifanywa 2013, hali ya elimu itakuwaje katika sehemu ile? Shule hizo zilijengwa miaka 20 au 30 iliyopita. Hii ni thuluma kwa watu wa Tana River. Ingawaje tunataka kuhifadhi misitu, uhifadhi wa misitu usitumiwe kutunyima sisi fursa ya kuelimisha watoto wetu. Kwa hayo machache, hii ni arifa ninatoa kwa Bunge: Ninaomba siku hiyo itakapofika, niruhusiwe nilete pendekezo la marekebisho ya sheria hiyo. Ahsante, Mhe. Naibu Spika.
view
-
3 Dec 2015 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kusema kongole kwa dada yangu Mhe. Amina na Wizara husika kwa kuleta sera ya kuhifadhi sehemu ya chemichemi. Wakenya wanakumbuka tulipopigana vita na kampuni ya Mumias Sugar walipotaka kuichukua Tana Delta kwa minajili ya kupanda miwa. Wachache tulisimama na tukasema kuwa chemichemi zinastahili kuhifadhiwa wala sikugeuzwa kuwa shamba la miwa. Iwapo tungekuwa na sera hii siku hizo, basi hatungezozana na kampuni ya Mumias Sugar. Kwa hivyo, nitampongeza Mhe. Amina na Wizara husika kwa kuileta sera hii ili chemichemi nchini zipate hifadhi. Chemichemi kubwa zaidi katika nchi ya Kenya iko katika Kaunti ya ...
view
-
12 Nov 2015 in National Assembly:
Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Ninachukua fursa hii kutoa kongole kwa Kiongozi wa Wengi Bungeni kwa kuleta Mswada huu hapa. Mada na maudhui ya Mswada huu ni kulinda mila na desturi yetu kama taifa. Mhe. Kang’ata aliyenitangulia amenisikitisha akisema kuwa mila yetu kama Waafrika haina maana. Ni kwa masikitiko makubwa hayuko na sisi ndani ya hii Bunge. Ningependa kumwambia kwamba watu wamemwaga damu au wamekufa kwa minajili ya kulinda mila ya Mwaafrika hapa Kenya. Anataka kutuambia wale waliopigania Uhuru wa taifa hili walikuwa wajinga? Ningemwambia arudi darasani ajue mila ni nini. Nimebahatika kusoma kitabu kilichoandikwa na ...
view
-
12 Nov 2015 in National Assembly:
Tumepata nini kutoka kwa wazungu? Tumepata bunduki na utumwa. Mila ya Kizungu tuliyonayo leo katika nchi ya Kenya ni mila tumelazimishwa tuifuate kwa kutishiwa na bunduki. Ninasikitika kuwa siwezi kuingia katika Bunge hili bila tai. Ni masikitiko makubwa sana. Bunduki walioleta imeenda lakini sheria zao bado ziko. Sikubaliwi kuzungumza Bungeni mpaka nije na tai. Lini Mwafrika atazinduka na kuwa na uhuru? Angalia tulivyopoteza mila. Mwafrika alikuwepo kwa miaka na miaka. Kwa masikitiko makubwa, angalia vile ambavyo ukahaba kiasi cha umalaya ulivyoenea mijini mwetu. Angalia vijana wetu. Kila mmoja wao anatumia madawa ya kulevya kwa sababu tumepoteza maadili kama jamii. Ninasikitika ...
view
-
20 Aug 2015 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii, kwanza, kumpongeza Mhe. Kaluma kwa kuleta Mswada huu ambao utaleta mwongozo na uuwiano baina ya taasisi tofauti humu nchini. Bunge lina wajibu wa utunzi wa sheria. Mahakama hutafsiri sheria na utawala hutekeleza sheria. Ni lazima kuwe na uwiano baina ya taasisi tatu za Serikali zinazohusika katika utekelezaji wa sheria. Iwapo hakuna heshima, maanake sisi kama Bunge---Katika Kanuni za Bunge ambazo zinatuongoza hazituruhusu kujadili maswala ambayo yako mbele ya mahakama. Kwa bahati nzuri au mbaya, kanuni kama hizo haziko katika upande wa mahakama. Wakati mwingine mahakama huingilia shughuli za utunzi wa ...
view
-
6 Aug 2015 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono sera hii. Ni kwa nini naiunga mkono? Nchi ya Kenya, kama nchi zingine zinazoenedelea katika Bara la Afrika, tulipopata Uhuru, tulizipa kipaumbele sekta za uzalishaji, uwekezaji na biashara kuliko sekta ya haki na sheria. Maswala ya demokrasia na haki za binadamu yamekuwa matukio ya kigeni katika nchi ya Kenya. Ukilinganisha uwekezaji wa rasilimali katika sekta za biashara na uzalishaji na sekta ya sheria, ni kama uwekezaji katika sekta ya sheria umeanza juzi. Kwa sababu hiyo, dhuluma dhidi ya jamii na wananchi wa Kenya imeenda juu sana. Ni ...
view
-
6 Aug 2015 in National Assembly:
aliyefanya makosa. Mtu akishakaa kwa jela miaka 20 na ni mtu amefikisha miaka 80, atafika umri gani ndiyo Serikali iamini atajirekebisha? Kwa hayo machache, naiunga mkono sera hii.
view
-
6 Aug 2015 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Lengo kubwa la mkataba na ratiba hii ni kuboresha hali ya usalama wa ndege ama usafiri wa angani, kwa sababu duniani, kuna watu wanaotumia ndege kama silaha. Wanatumia ndege kulipua watu na makazi yao. Ratiba hii imeletwa ili kuwe na nyanja za kisheria katika ushirikiano wa kimataifa. Mataifa mbali mbali duniani yanafaa kutia sahihi ratiba hii ili kuleta usalama katika safari za angani. Pili, ni vipi tutakuwa na sheria itakayofanya tukomeshe watu kutumia ndege za abiria kama zana za kivita? Mara nyingi, ndege hizo za kivita huleta vifo ...
view
-
5 Aug 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Kifungu cha 94(1) na (3) kinapeana wajibu wa utunzi na urekebishaji wa sheria kwa Bunge la taifa. Wale wenye dhana kwamba Wabunge wana nia ya kujiongezea muda na wanataka kuzua pesa, hii ni dhana isiyokuwa na msingi wa kisheria. Tuna wajibu. Wakitusifu au watutusi, tuna wajibu wa kuirekebisha sheria.
view
-
5 Aug 2015 in National Assembly:
Swala nyeti ni, je, Mswada ulioko mbele yetu, unataka kura ya maoni? Kifungu cha 255 ni wazi kuhusu ni nini kinachofaa kupigiwa kura ya maoni na ni nini hakifai. Kwa hivyo, Kifungu 259 kinatupa sisi fursa ya kutunga sheria kama hii ili kuweka wazi siku ya uchaguzi itakuwa lini ndio Wakenya waweze kujipanga kimbele.
view