Ali Wario

Parties & Coalitions

Born

5th May 1970

Post

P. O. Box 10 Bura, Tana

Email

warioali@yahoo.com

Telephone

0721398361

Telephone

0725206089

All parliamentary appearances

Entries 551 to 560 of 612.

  • 12 Sep 2007 in National Assembly: Ahsante sana Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa fursa hii. Mwenyezi Mungu anatuambia: "Nimewaumba kwa makabila na mataifa ili mpate kujuana. Bora kati yenu ni yule anayemheshimu na kumtii Mwenyezi Mungu zaidi." Ndiposa mtu anapokufa huvuliwa vazi la ukabila. Mtu hafi kama Mjaluo. Unapokufa, unakuwa maiti! Ile dakika roho yako inakatika, wewe si Mjaluo wala Mkikuyu tena. Unapokufa, wewe unaitwa maiti! view
  • 12 Sep 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, rai walizotoa waheshimiwa Bw. Muturi na Bi. Njoki Ndung'u ni nzuri na za ukweli. Hata hivyo, rai zao zinahitaji Hoja nyingine, siyo hii. Hoja hii itakuwa sumu kwa nchi hii. Ni Hoja mbaya inayostahili kupingwa na kila mheshimiwa Mbunge aliye ndani ya Bunge hili. Bw. Naibu Spika wa Muda, yapasa tujiulize ni kwa nini Hoja hii imeletwa Bungeni leo. Hoja hii imeletwa leo kwa sababu miezi michache ijayo, tutaenda kupiga kura. Nia ya Hoja hii ni kuamsha hisia za kikabila na chuki na uhasama baina ya Wakenya! view
  • 12 Sep 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, mwaka huu tutapiga kura. Serikali hii ilichukua uongozi miaka minne iliyopita lakini yeye ameileta Hoja hii hapa leo. Bw. Naibu Spika wa Muda, sitaki kuzungumza juu ya mja, lakini tutakapozungumza juu ya nafasi za kazi huku tukizingatia ni nani amepewa cheo kipi au kile, nafikiri mhe. Ojode hastahili kuileta Hoja hii. Yeye alikuwa Waziri Msaidizi katika Serikali iliyopita na hii iliyoko sasa. Hakuna siku hata moja ambapo yeye alitangaza kuwa atajiuzulu kwa sababu kuna ukabila katika Serikali hii. Yeye alijiuzulu kwa sababu headman alimwambia aondoke kazini! Kwa hivyo, ikiwa Hoja hii itapitishwa--- view
  • 12 Sep 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, tulinyamaza wenzetu kutoka Upinzani walipokuwa wakichangia Hoja hii. Wao pia yafaa watuvumilie sasa kwa sababu ni lazima wasikie rai zetu. Si lazima tuichukue Hoja jinsi inavyoletwa kwetu. Sisi tuko hapa kuchambua. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningewaomba wenzetu waangalie nyuma. Tuliambiwa hapa kwamba Wizara zenye fedha nyingi zimepewa Wakikuyu. Je, kabla Wizara hizo kupewa Wakikuyu, zilikuwa chini ya Mawaziri gani? Kwa mfano, Wizara ya Kawi ilikuwa na Waziri yupi? Je, Wizara ya Barabara na Ujenzi ilikuwa chini ya nani? Swali ambalo ningependa kuwauliza ni hili: Wizara ya Elimu inaongozwa na mhe. Prof. Saitoti. Je, elimu ... view
  • 12 Sep 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, nitapunguza Kiswahili ninachozungumza. Pengine ndicho kinachowasumbua wenzangu! Tena nitazungumza kwa upole ili niweze kueleweka! view
  • 12 Sep 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, nikimalizia mchango wangu, ningependa kusema mambo mawili. Kwanza, tusiwe na mazoea ya kusema eti Kenya ina makabila 40. Kuna makabila mengi ambayo hayajasajiliwa. Kwa hivyo ile hesabu ya kusema kwamba Kenya ina makabila 42 ni ya kikoloni. Leo, hapa Kenya kuna makabila mengi ambayo hayajatambulika. Unaweza kuongeza katika makabila hayo Mmarakwet na Mnyayaya. Kuna makabila zaidi ya 50 humu nchini! Mwisho, Bw. Naibu Spika wa Muda, sharti tuingalie Kenya kama Kenya wala siyo kama nyumba ya ukabila. Tukipitisha hii Hoja kuwa sheria, italeta mizozo, chuki na uhasama katika nchi hii. Tuitupe haraka iwezekanavyo! Ninapinga Hoja ... view
  • 23 Aug 2007 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Spika. Kuna sauti inayokera! view
  • 8 Aug 2007 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii na nampongeza Dkt. Awiti kwa 3042 PARLIAMENTARY DEBATES August 8, 2007 kuileta Hoja hii. Ninasimama kuiunga mkono kama Mbunge. Sitaki kuingia katika masuala ya falsafa ya kibepari na kikomunisti, kwa sababu sioni kama ndio suluhisho la matatizo yanayowakumba wananchi na Wakenya kwa jumla. Lakini kuhusu masuala ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma, kwa sababu kama jina linavyoonyesha, ni mashirika yaliyopatikana kutokana na rasilimali za umma, ni muhimu kuwepo uwazi katika ubinafsishaji huo. Kwa nini nasema haya? Muda mchache uliopita, tuliambiwa kuwa Kenya Meat Commission (KMC) haiwezi kubinafsishwa ... view
  • 17 Jul 2007 in National Assembly: Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii. Mwenyezi Mungu anatuambia--- view
  • 17 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, nashukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu katika Kurani tukufu anatuambia, "Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba mwanadamu kwa pande la damu. Soma, Mola wako ni mtukufu ambaye amemfunza---" view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus