Ali Wario

Parties & Coalitions

Born

5th May 1970

Post

P. O. Box 10 Bura, Tana

Email

warioali@yahoo.com

Telephone

0721398361

Telephone

0725206089

All parliamentary appearances

Entries 561 to 570 of 612.

  • 17 Jul 2007 in National Assembly: Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Mwenyezi Mungu anatuambia:- "Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba mwanadamu kwa pande la damu. Soma, Mola wako ni mtukufu mno ambaye amemfunza kuandika kwa kalamu. Amemfunza mwanadamu asilolijua." Bw. Naibu Spika wa Muda, hayo si maneno yangu bali ni maneno yake Mwenyezi Mungu katika Kurani tukufu Sura 96, Aya ya kwanza hadi ya tano. Kuhusu umuhimu wa elimu, Mwenyezi Mungu ametoa mfano huu kuthibitisha kufaulu kwa mwanadamu humu duniani na ahera keshoye. Ili mwanadamu apate kutatua matatizo yake, inategemea ni elimu aina gani mwanadamu amefunzwa. Mbali na hayo, ninasimama kuunga mkono Hoja hii. ... view
  • 17 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda nitaliondoa neno hili na badala yake niseme watapotosha Wakenya kwa sababu wanaota ndoto isiyotekelezeka. Leo, elimu ya bure imetolewa kwa watoto. Watoto wafugaji wasiokuwa na tamaa ya kufika Darasa la Nane, leo wameacha kuchunga mifugo na kila mmoja anakimbia kuelekea July 17, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2547 darasani kung'ang'ana kama watoto wengine wa Kenya. Serikali, kupitia tuition, imesema kwamba karo inayotolewa kwa ajili ya masomo itaondolewa mwaka ujao. Huo ni mzigo wa pili wa Mkenya kuondolewa. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni vigumu mtu kuamka siku moja kujenga nyumba na kuikamilisha. Hii elimu ya bure ina ... view
  • 29 May 2007 in National Assembly: Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga Hoja hii mkono. view
  • 29 May 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, swala la kuhesabu vyama si swala la Bunge hili mbali ni la Msajili wa Vyama. Juzi Bunge liliketi na kupitisha sheria kuhusu namna ya kuwachagua waakilishi wa Kenya katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashiriki. Ni matumaini yangu, kuambatana na sheria hiyo, ikiwa mhe. Bunge, alitaka kuikosoa, basi alikuwa na fursa na nafasi ya kutosha kuhakikisha vyama fulani na watu binafsi watapata fursa katika uwakilishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashiriki. Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge hili. Hatuwezi kuibatilisha sheria! Kenya imechelewesha shughuli za Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashiriki kwa sababu ya mvurtano ... view
  • 27 Mar 2007 in National Assembly: Hoja ya nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. view
  • 27 Mar 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, je, ni sawa kwa mzungumzaji kusema kwamba watu wote wanaotoka katika Ofisi ya Rais ni watu kutoka kabila moja, ilhali mimi natoka katika Ofisi ya Rais na sitoki Mkoa wa Kati? Je, ni sawa kupotosha Bunge hili? view
  • 27 Mar 2007 in National Assembly: Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningetaka kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia nafasi hii. March 27, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 137 Nikizungumza kutoka sehemu hii--- view
  • 27 Mar 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, nikizungumza kutoka sehemu hii ya Bunge hili, wengi wanashangaa na wanauliza ni kwa nini ninafanya hivyo, ilhali wao hawashangai wanapotoka sehemu ya kulia na kwenda sehemu ya kushoto. Ni lazima kila Mbunge na chama kipewe haki ya kutekeleza demokrasia itakavyo. Sio kwamba, wengine wana ruhusa ya kwenda sehemu ya kushoto na wengine hawana ruhusa ya kwenda sehemu ya kulia ya Bunge hili. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningetaka kuchukua fursa hii kumpongeza Rais na kuunga mkono Hotuba yake, iliyotoa mwongozo wa sera na sheria, kwa sababu, siasa sio porojo bali ni sera na sheria. view
  • 27 Mar 2007 in National Assembly: Katika Hotuba yake, Rais aligusia swala la uhalifu au sheria zilizoidhinishwa, ikiwemo uhalifu wa kiuchumi, usimamizi wa mali ya umma, maadili mema ya wafanyikazi na ubinafsishaji wa mashirika yasiyo ya Serikali. Haya yameboresha hali ya maisha ya Wakenya na uchumi wa taifa hili. Hali hii imechochea uwekezaji zaidi wa rasilmali za nje katika nchi yetu. Bw. Naibu Spika wa Muda, ama kwa hakika, huu ndio ufanisi na usawa ambao Wakenya kwa mara ya kwanza katika miaka 40 wameanza kusherehekea leo! Ninasema haya kwa sababu kuna mtiririko wa rasilmali ya taifa katika mashinani, zikiwemo pesa za CDF, pesa za barabara, pesa ... view
  • 27 Mar 2007 in National Assembly: 138 PARLIAMENTARY DEBATES March 27, 2007 Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna hazina ya vijana. Maeneo ya Bunge 210 yamepokea Kshs210 milioni. Hivi karibuni, zaidi ya Kshs7 milioni zitapeanwa kwa vikundi vya vijana. Pesa hizi zitawawezesha vijana wetu kujinufaisha na kujiboresha katika nyanja ya kibiashara. Kuna vipofu na viziwi ambao hawawezi kusikia, kuona au kuzungumza juu ya haki zao. Ukizungumza juu ya sera au sheria, unaambiwa kuhusu ufisadi. Kumaliza ufisadi siyo rahisi kama kunywa kahawa ambayo itakuchemsha damu mara moja; kumaliza ufisadi kunahitaji karakana, mikakati, sera, sheria na uwiano. Tukisimama pamoja, tutafaulu kupambana na ufisadi. Tukingojea Rais Kibaki amalize ufisadi ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus