Ali Wario

Parties & Coalitions

Born

5th May 1970

Post

P. O. Box 10 Bura, Tana

Email

warioali@yahoo.com

Telephone

0721398361

Telephone

0725206089

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 612.

  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Zamani kuna mtunzi mmoja wa Shairi aliyesema: view
  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Uhuru sijauona, na tunda silibaini view
  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Ijapo tumepigana, tukang’oa mkoloni view
  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Limebaki kubezana, na utu kutothamini view
  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Tunda la uhuru lipi, Mkenya shamba huna? view
  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, tunapozungumzia uhuru wa mahakama, vifungu vya sheria 48, 49, 50 na 51 vinazungumzia kwa upana uhuru wa mahakama. Uhuru huu utatoka wapi iwapo Jaji Mkuu na majaji wa Mahakama Kuu ni watu wanangoja waajiriwe na Rais, Rais ambaye licha ya kuwa kiongozi wa taifa, ni kiongozi wa utawala? Kwa hivyo, mimi naona kuna chembe kubwa hapa. Uhuru wa mahakama ni ndoto mpaka tuwe na sheria maalum ambayo inawapa rasilimali bila kuomba. Jaji Mkuu anasimama hadharani akiomba apewe rasilimali. Sasa uhuru utatoka wapi wakati Jaji Mkuu hawezi kutekeleza wajibu wake wa kisheria mpaka aombe utawala umpe ... view
  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Kuna dhana potovu kule nje kwamba Bunge la Taifa ndilo linasimamia ugavi wa rasilimali za taifa. Kuna vipengele kadhaa katika sheria yetu vinavyoruhusu utawala kutumia pesa bila kupitia Bunge. Ni tamthilia uwezo wa Bunge kusimamia ugavi wa rasilimali. Ugavi wa rasilimali ni siasa. Ni mchakato wa siasa. Ndiposa kama mahakama inafanya kazi yake vilivyo, mifereji hufungwa ili wahisi kiu, walie na waombe ifunguliwe kidogo kwa mtiririko. Kwa hivyo, uhuru wa mahakama ni ndoto ambayo ni ngumu Wakenya kuifikia kwa sasa. view
  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Demokrasia nyingi duniani zina mipaka baina ya utawala wa Bunge na mahakama. Kenya pia tunaamini kwamba kuna mipaka baina ya utawala, Bunge na mahakama. Lakini utawala ndio unakalia rasilimali. Umewahi kusikia hukumu ikitolewa kwamba ndugu yetu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Miguna Miguna ana uhuru wa kurudi Kenya? Imetokea nini Miguna hawezi kurudi Kenya? Ni kwa sababu utawala hauna masikio ya kusikia hukumu ya haki. Miguna hawezi kurudi Kenya. Vivyo hivyo, utawala wa mahakama ni ndoto. view
  • 11 Mar 2020 in National Assembly: Katika Tana River, kuna Mahakama Kuu moja kule Garsen. Tana River ni kilomita 88,000 mraba. Ili mtu aliye Balambala aweze kufikia Mahakama Kuu iliyoko Garsen, lazima asafiri kilomita 400. Access to justice kama walivyosema wahenga ni nadra. Ni vipi yule mtu aliye kilomita 400 atapata haki kweli? Ni vizuri tuwe na kifungu ambacho kitatoa uhuru wa rasilimali kwa mahakama. Uhuru wa mahakama hauwezi kupatikana hadi hapo watapokuwa na uhuru wa kupata rasilimali bila kutegemea taasisi nyingine. Hivyo basi, zile pesa wanazopata zichunguzwe. Hata zile zitakazoenda kwa utawala pia zichunguzwe lakini kuwe na uhuru. Tusifike kiwango cha kumdhalilisha Jaji Mkuu hadi ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus