Andrew Mwadime

Parties & Coalitions

Email

achawia@yahoo.com

Telephone

0722867598

All parliamentary appearances

Entries 181 to 190 of 443.

  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, mazingira yameharibika. Ile mvua tulikuwa tunapata zamani haipo tena. Mtu anapoongea juu ya unyunyizaji maji wa mashamba, huo ni mwelekeo mwema. Mwenyezi Mungu, kabla hajatuumba sisi binadamu, alitupatia maji, hewa na chakula. Vitu vingine kama vile nguo na usalama yalikuja baadaye. Ukimpa binadamu chakula, utakuwa umempa maendeleo. Ukifananisha nchi yetu ya Kenya na nchi zingine, utakuta kwamba Mwenyezi Mungu alitupa ardhi nzuri ambayo ina rotuba nyingi. Shida ni kwamba mipangilio yetu haiko sawa sawa. Yule aliyeleta huu Mswada kuhusu unyunyizaji maji sharti tumpe kongole. Kule kwangu katika Kaunti ya Taita, Eneo Bunge la Mwatate, kuna ... view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Makazi yamekuwa ni taabu. Hapa nchini Kenya wananchi wengi ni wakulima. Kwa kweli, Serikali yetu inapaswa kutenga pesa za kutosha ili kujenga mabawa. Tunapaswa kuwa na mpangilio sawasawa ndio tuzidi kuenda mbele. Wahenga walisema kwamba, ‘panapo hela basi hapo hela zitaongezeka.’ Pia vile vile, panapo maji pia maji yataongezeka. Hii ni kumaanisha haya mabawa yakijengwa basi watu wataanza kupanda miti ambayo italeta mvua. Pia mzingara yatakuwa kama yalivyokuwa hapo awali. view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Mbunge ambaye ameleta Mswada huu amefikiria wakati mwafaka. Basi tunapaswa kuunga mkono na kuhakikisha kwamba umetekelezwa. Wenzangu wameongea mengi na singependa kurejelea yale wameongea. Nashukuru kwa kupatiwa fursa hii. view
  • 10 Apr 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii. Asante sana. Umenitambua kwa sababu nilikuwa nimekuja mbele kabisa. Bahati mbaya mwenzangu kwa ile view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: ukapitiwa ukashika kadi yangu kwa bega lake basi ikabanduka. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Kabla hata sijaongea, kwa kweli na dhati kabisa, naunga mkono hii Hoja. Kabla sijasahau, najua wenzangu hapa wameongea kuhusa masuala ya maji. Nadhani katika awamu ya Bunge la 11, nilipitisha Hoja ya maji na Wabunge hapa waliunga mkono kwa wingi kabisa kuwa kila taasisi ya umma ipate maji. Hiyo Hoja ilipita vizuri lakini kwa sasa hivi mpaka dakika hii hatujui imefiki wapi. Nimejaribu kuifuatilia kila mahali lakini ninatupwa huku na kule. Kwa hivyo, Kamati Tekelezi ni vyema ifuatilie hiyo Hoja. Ikiwezekana maji ipatikane kila mahali ndiyo magonjwa mengi yapungue. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Kwa sasa hivi, mimi kama mwakilishaji wa Eneo Bunge la Mwatate naona saratani inatumaliza. Na ni kweli watu wengi sana wana saratani. Juzi tu, nilikuwa na Mbunge wa kwanza ambaye alikuwa anawakilisha Eneo Bunge la Mwatate. Alikuwa anateta na kuuliza kwa nini Bunge isifanye bidii ili kila kaunti angalau ipate mashine ya kuangalia saratani. Mwenzangu wa Nyali, Mhe. Ali, kwa kweli hii Hoja ameitunga na ikatungika. Tunasema tutaifuatilia ili itekelezwe. Kama vile Mbunge wa Jomvu alivyosema, tusikuwe na mambo ya mchezo maanake magonjwa kwa kweli hayataki siasa. Wakenya tutakuwa tumesaidika. Mwanzo tuanze na ile mikoa ya zamani nane. Kila mkoa ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Mhe. Spika, nadhani kila Mbunge amesikia. Hii Hoja itasaidia Wakenya kwa ujumla maanake watu husafiri kutoka maeneo mbalimbali. Tukiangalia hali ya mfuko kwa kila mtu, kwa kweli haiendi sambamba. Kifungu 43 cha Katiba kinaambatana pia na kile cha ugatuzi. Kinasema kwamba ikiwezekana, hela izidi kusukumwa kwa wingi kule mashinani. Najua kuna changamoto maanake ugatuzi ulianza juzi. Wakipelekewa pesa kwa wingi, nafahamu kaunti zetu zitatatua hili tatizo la magonjwa. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Vile vile, kupata dawa limekuwa tatizo katika hospitali ya Serikali. Hii Hoja ikitekelezwa, najua itapunguza taabu kwa wingi. Kwa sababu wenzangu wameongea sana na nikiongea nitakuwa narejelea yale, natoa shukrani kwa kunipa hii fursa. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus