Andrew Mwadime

Parties & Coalitions

Email

achawia@yahoo.com

Telephone

0722867598

All parliamentary appearances

Entries 191 to 200 of 443.

  • 13 Mar 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii. Nimechunguza kwa wenzangu wote ambao wamechangia na nimeona suluhu kwa kweli iko tu na Wabunge hapa hapa. Kwanza, tumetambua kwamba usalama ndio tatizo. Ndio maana Mbunge ambaye amenitangulia amesema kuwa yafaa kuwa na walimu wanajeshi. Mimi naongea kama mwalimu. Nikimnukuu yule Muingereza anayeitwa Maslow alisema kwamba kwanza mahitaji yale madogo madogo lazima yawe sawa ndio mahitaji makubwa makubwa yaje baadaye. Ukimweka mwalimu katika hali ambapo hamna usalama hapo kuna tombojoto. view
  • 13 Mar 2018 in National Assembly: Ninakumbuka nilipotoka chuoni nilienda kufundisha mahali ambapo nilikuwa natofautiana napo kitabia na masuala mengi tu. Baada ya muda mfupi tumbo lilianza kuwa na vidonda. Muda kidogo nilikuta risasi ambayo kwa Kiingereza inaitwa stray bullet ikanigonga na maisha yangu hayakuwa sawa sawa. Mwalimu ambaye maisha yake hayako sawa sawa kufundisha ni uongo. Hapo tunadanganyana. Ni vizuri TSC iangalie suala hili kwa undani. Pia tunafahamu kwamba hapa Kenya ukabila upo. Hivi sasa ukienda kule utakuta kuwa wale wako huko ambao si jamii ya huko ni wale watu wadogo wadogo ndio wamesukumwa huko. Hao ambao wanapitisha sheria hizo watoto wao wako katika shule ... view
  • 13 Mar 2018 in National Assembly: Kwa hivyo, watu wasilichukulie suala hili kwa mzaha. Waliangalie kwa kina na suluhu ipatikane kwa haraka maana wale watoto wakikosa elimu risasi zitazidi upande ule na wale nao wakiwa kule hamna elimu inaendelea maana hawajatulia. Usalama wao upo hatarini. Unajua ukishajisikia usalama hauko sawasawa basi utakuta tumbo lako kila wakati linawaka moto na hamna kazi unaweza kufanya. Tuyaangalie na kuyapina yote hayo na tujaribu kutatua suala hili kisawasawa. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. view
  • 1 Mar 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii. Nimechunguza kwa wenzangu wote ambao wamechangia na nimeona suluhu kwa kweli iko tu na Wabunge hapa hapa. Kwanza, tumetambua kwamba usalama ndio tatizo. Ndio maana Mbunge ambaye amenitangulia amesema kuwa yafaa kuwa na walimu wanajeshi. Mimi naongea kama mwalimu. Nikimnukuu yule Muingereza anayeitwa Maslow alisema kwamba kwanza mahitaji yale madogo madogo lazima yawe sawa ndio mahitaji makubwa makubwa yaje baadaye. Ukimweka mwalimu katika hali ambapo hamna usalama hapo kuna tombojoto. view
  • 1 Mar 2018 in National Assembly: Ninakumbuka nilipotoka chuoni nilienda kufundisha mahali ambapo nilikuwa natofautiana napo kitabia na masuala mengi tu. Baada ya muda mfupi tumbo lilianza kuwa na vidonda. Muda kidogo nilikuta risasi ambayo kwa Kiingereza inaitwa stray bullet ikanigonga na maisha yangu hayakuwa sawa sawa. Mwalimu ambaye maisha yake hayako sawa sawa kufundisha ni uongo. Hapo tunadanganyana. Ni vizuri TSC iangalie suala hili kwa undani. Pia tunafahamu kwamba hapa Kenya ukabila upo. Hivi sasa ukienda kule utakuta kuwa wale wako huko ambao si jamii ya huko ni wale watu wadogo wadogo ndio wamesukumwa huko. Hao ambao wanapitisha sheria hizo watoto wao wako katika shule ... view
  • 1 Mar 2018 in National Assembly: Kwa hivyo, watu wasilichukulie suala hili kwa mzaha. Waliangalie kwa kina na suluhu ipatikane kwa haraka maana wale watoto wakikosa elimu risasi zitazidi upande ule na wale nao wakiwa kule hamna elimu inaendelea maana hawajatulia. Usalama wao upo hatarini. Unajua ukishajisikia usalama hauko sawasawa basi utakuta tumbo lako kila wakati linawaka moto na hamna kazi unaweza kufanya. Tuyaangalie na kuyapina yote hayo na tujaribu kutatua suala hili kisawasawa. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. view
  • 28 Feb 2018 in National Assembly: Asante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia fursa hii. Vile vile, watu wa Taita County, haswa Mwatate, wanaunga mkono malalamishi na kilio kuhusu wanyama pori, haswa vile wanaharibu mimea na kuua watu, lakini hakuna malipo yoyote. Kitu ambacho kimetushangaza zaidi ni kwamba watu wanabebeshwa mizigo juu ya mingine. Ndovu wanatolewa Laikipia na kupelekwa Mbuga ya Wanyama Pori ya Tsavo. Badala ya kumaliza hiyo taabu kule Laikipia, wanatupelekea hiyo taabu kule Taita. Tafadhali, tunaomba wakati mnaanaglia hili suala la malalamishi, jaribuni kuliangalia vyema. Tayari ukiangalia orodha ya malipo ya fidia Kenya nzima, wakazi wa Taita Taveta County ndio wanaodai hela nyingi zaidi. ... view
  • 24 Jan 2017 in National Assembly: Ooh, asante sana, Mhe. Spika. view
  • 24 Jan 2017 in National Assembly: Shukrani kwa kunipa nafasi hii. Mwanzo kabisa, ningependa kuiunga mkono Hoja hii. Nikiangalia walioorodheshwa katika ratiba ya leo, wote wanauzoefu wa kazi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 24 Jan 2017 in National Assembly: hii. Kabla sijaendelea, nawatakia wenzangu mwaka wenye fanaka na vilevile kuomba wafanikiwe kwa shughuli nyingi walizo nazo mbeleni. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus