Boy Juma Boy

Died

13th February 2017

Telephone

0713 242955

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 98.

  • 14 Sep 2016 in Senate: Bw. Spika, ningependa Msimamizi wa Bajeti anifafanulie--- view
  • 14 Sep 2016 in Senate: Bw. Spika, niokoe kutokana na maneno ya Sen. (Dr.) Khalwale na Sen. Orengo. view
  • 13 Sep 2016 in Senate: Hoja ya nidhamu, Bw. Spika. view
  • 13 Sep 2016 in Senate: Bw. Spika, ulikuwa umeshatoa uamuzi ya kwamba haitakuwa kazi yetu kuwasaidia washtaki. Nidahmu anayorejelea tena Sen. Wako anapinga amri ile ile uliyokwishatoa ya kwamba mshtaki aachwe aendelee na kesi yake na sisi kazi yetu ni kusikia. Baada ya kumpa mwanya sen.wako anarejelea kulekule ambako wewe tayari umeshatoa uamuzi. Je, hii ni sawa? view
  • 28 Jul 2016 in Senate: Asante,Bw. Spika. Nilikuweko ndani ya Jumba hili ulipotoa amri kwamba swali hili lijibiwe leo. Amri yenyewe ilitoka kwako; Spika wa Bunge hili! view
  • 28 Jul 2016 in Senate: Sasa, Bw. Spika leo imefika na jibu hakuna. Ina maana aliyedharauliwa ni Spika ama ni Bunge? Kwa fikira yangu, kuna nyoka anayeuma halafu kuna nyoka wa plastiki. Agutusha tu lakini haumi. Sijui kama hawa wenzetu wanatufanya sisi, Bunge la Seneti, kuwa nyoka wa plastiki ambaye haumi. Naungana na Sen. Sang kwamba itabidi nyoka aume sasa; asiwe nyoka wa plastiki. view
  • 20 Jul 2016 in Senate: Bw. Naibu Spika, Kamati inayo deal na swala la maji ni Kamati ya Ardhi--- view
  • 20 Jul 2016 in Senate: Bw. Naibu Spika, Kamati inayohusika na swala la maji na ardhi ni Kamati ya Ardhi na Mazingira. Mimi ni mwanachama wa Kamati hii na nitalishughulikia swala hili na kuleta jibu kwa muda wa wiki moja. view
  • 9 Jun 2016 in Senate: Bw. Spika, asante kwa kunipa nafasi ya kuunga mkono malalamishi haya. Bw. Spika, kuna kulalamika na kunung’unika. Kunungu’nika ni ile hali ya kupigo domo tu bila kuchukua hatua yoyote. Wakenya wengi tunapenda kununung’unika. Tunayotaka sisi ni kulalamika na kuhakikisha maneno yamewekwa katika maandishi kusudi jambo lile liweze kufuatiliwa. Haya malalamishi ndiyo tunataka kuliko kunung’unika. Bw. Spika, naunga mkono watu wa Bungoma kwa jambo walilotenda na ninahimiza jambo hili lifanyiwe kazi kwa haraka. view
  • 24 Mar 2016 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika. Hapa ninavyoona ni kwamba swali lililoulizwa ni linguine, mbali na lile linalojibiwa. Ameulizwa juu ya “acute food shortage” na anatuambia kwamba kuna chakula kimepatikana “kuna nini, lele mama, hehe, hoho wala hasemi ukweli. Je, kuna upungufu wa chakula au la? Jambo la pili ambalo ameulizwa kama wanafunzi hawaendi shuleni kwa sababu ya ukosefu wa chakula. Jibu ambalo amesema ni kwamba hana habari hiyo. Sen. (Prof.) Lonyangapuo na Sen. Munyes wamesema hayo mambo. Je, nani muongo? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus