All parliamentary appearances
Entries 21 to 30 of 98.
-
16 Mar 2016 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda. Kwanza, nawapongeza maafisa wote kutoka kaunti za Nyamira, Kilifi na Vihiga kwa kutembelea Seneti. Ninauhakika watajifunza mengi kutoka kwetu na maofisa wetu. Seneti ni Bunge la viongozi wa wingi wa busara na wakuheshimika sana. Wao hujadili mambo kwa makini sana. Upeo wao ni wa mbali na mpana sana. Ninawapongeza wakaaji wa Malindi. Imedhihirika kuwa wao si watu wa kununuliwa kwa Kshs1,000 na zaidi na hawawezi kamwe kutishwa na mabundiki; hata tukipokonywa bunduki na walinzi wetu wa kibinafsi.
view
-
16 Mar 2016 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda. Kwanza, nawapongeza maafisa wote kutoka kaunti za Nyamira, Kilifi na Vihiga kwa kutembelea Seneti. Ninauhakika watajifunza mengi kutoka kwetu na maofisa wetu. Seneti ni Bunge la viongozi wa wingi wa busara na wakuheshimika sana. Wao hujadili mambo kwa makini sana. Upeo wao ni wa mbali na mpana sana. Ninawapongeza wakaaji wa Malindi. Imedhihirika kuwa wao si watu wa kununuliwa kwa Kshs1,000 na zaidi na hawawezi kamwe kutishwa na mabundiki; hata tukipokonywa bunduki na walinzi wetu wa kibinafsi.
view
-
10 Mar 2016 in Senate:
Bw. Speaker, ningependa kukaribisha Kamati ya Energy iliyotoka Kaunti ya Kilifi. Kama unavyojua, Kaunti ya Kilifi ndiko kuna mji wa Malindi. Sina haja ya kusema sana lakini unajua jinsi mambo ya Malindi yalivyokuwa. Kwa hivyo, nina furaha sana kuwakaribisha hapa. Ningependa kuwaambia watakaporudi huko, waendelee kama walivyofanya.
view
-
3 Mar 2016 in Senate:
Bw. Spika, Nidhamu yangu ni kwamba Sen. Adan hakujibu swali liloulizwa na Sen. (Prof.) Lonyangapuo. Ameulizwa kama rubani huyu ni mgeni. Katika jibu lake alisema, “ndio ana paspoti ya Marekani.” Ni wazi kwamba yeye ni mgeni. Sen. (Prof.) Lonyangapuo aliuliza, kwa nini rubani wa kigeni anapewa kazi ilhali kuna rubani wengi hapa nchini? Lakini amelihepa swali hilo.
view
-
3 Mar 2016 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, naomba Naibu Mwenyekiti atueleze kama anajua kwamba katika Katiba Kifungu 37 kuna haki ya watu kufanya maandamano. Ameeleza vizuri kwamba wakati maandamano ikienedelea, vitoa machozi vilifyatuliwa. Kwa nini askari waliacha kufyatua vitoa machozi? Viliisha ndio wakaamua kupiga risasi mara kadhaa.
view
-
28 Oct 2015 in Senate:
Asante sana Bw. Spika kwa kunipa nafasi niunge mkono Hoja hii. Nimeitazama Hoja yenyewe na kuisikiliza ilipokuwa ikipendekezwa kwetu na nimeridhika na majina ya Maseneta ambao wameteuliwa kuhuduma katika Kamati hii. Kwa maoni yangu, Hoja hii na Kamati hii, ina uwezo kupita maelezo kwa sababu Maseneta wote ambao ni wanachama, hakuna ambaye anaweza kununulika kirahisi. Nikiwatazama vizuri, nina hakika hakuna yule ambaye anaweza kununulika; hayumo! The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
-
28 Oct 2015 in Senate:
Bwana Spika---
view
-
28 Oct 2015 in Senate:
Bw. Spika, nimefurahi kwa sababu inaonekana sasa Kiswahili chafuatiliwa vizuri kwa sababu sasa ndio tunapoenda katika utamu wake na ladha yake. Nilichosema mimi ni kwamba “sifikirii”. Kufikiria ni kwamba jambo hilo haliko katika mawazo yangu. Kwa hivyo, niliposema sifikirii kwamba kuna Seneta anayeweza kununuliwa kiurahisi, ni fikira ambayo haipo wala jambo hilo haliko. Ni fikra ambazo nimezileta. Yaani hata hauwezi kuliwaza jambo kama hilo. Ninawashukuru kwa maana yaonekana kidogo Kiswahili chaanza kufufuka ndani ya Seneti. Bwana Spika, nikiendelea ni kwamba Hoja hii ni ya moja kwa moja---
view
-
28 Oct 2015 in Senate:
Bw. Spika, ninafikiri nimelijibu vizuri. Nimesema ningelieleza kwamba haimo katika mawazo yangu kwamba kuna yeyote anaweza kununulika. Lakini kama amelielewa kimakosa, basi wacha nimuweke katika hali ya usawa kwamba asiwe na taswishi. Naona Kiswahili hapo kimeeleweka. Nimeliondoa tamshi hilo. Kwa hali hiyo, naiunga mkono Kamati hii na ningependa kusisitiza kwamba nimehudumu katika moja ya Kamati hizi; zina kazi nyingi, zina muda mrefu, zina muda ambao wakati mwingine Kamati zinafika mpaka usiku wa manane, kwa hivyo, ni kazi ya kujitolea. Kwa hayo machache, naunga mkono. Asante.
view
-
14 Oct 2015 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda kunipa nafasi hii ili niungane na Maseneta wenzangu kuunga mkono Hoja hii muhimu. Ukiisoma Hoja hii, unafaa kujiuliza inapendekeza nini. Hoja hii inataka mabadiliko katika Katiba ili kuifanya Seneti hii kuwa na nguvu. Inafaa tujiulize ikiwa ni kweli kwamba Seneti haina nguvu. Jibu la swali hili ni kuwa Seneti haina nguvu. Kwanza tunafaa kuwasifu Wanakamati wa Kamati hii. Kamati hii iliwajumuisha mawakili wanne waliokolea katika taaluma ya uwakili. Nilipotazama vizuri, niliona kuwa ilikuwa na akina dada wawili wazuri sana na walio na elimu ya juu. Ukitazama vizuri, utaona kwamba Kamati hiyo iliundwa na watu ...
view