All parliamentary appearances
Entries 91 to 98 of 98.
-
25 Sep 2013 in Senate:
Mtandawazi ndio mwelekeo wa kisasa. Hoja hii ina umuhimu kwa sababu kaunti ndio mwelekeo mkubwa ambapo sasa tunaenda katika Serikali za Ugatuzi. Makao makuu ya ugatuzi sasa yako katika kaunti. Hapa ndipo mahali ambapo huu mtandawazi utakapounganishwa, basi kaunti zitaweza kuunganishwa na Serikali kuu, Seneti, Treasury na ulimwengu kwa ujumla. Hivi sasa ulimwengu umekuwa nyumba moja na hatuwezi kukaa na kusema kwamba kaunti zetu zibaki vile zilivyo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
-
25 Sep 2013 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, namshukuru kwa sababu nilifikiri haelewi kumbe anaelewa. Hivyo alivyo elewa ndio ilikuwa nia yangu na wala si nia yangu kupotosha wananchi. Kuna Serikali ya Kitaifa na serikali ya ugatuzi.
view
-
25 Sep 2013 in Senate:
Kulingana na hali hii, nia na madhumuni ya hoja hii ni kuhakikisha ya kwamba nchi nzima, huu utandawazi ambao ni mwelekeo wa miaka hii, unaendelea. Kwa hivyo, namsifu aliyeleta Hoja hii. Yeye ni mwenyekiti wa kamati yetu. Naona kwamba yeye yuko na maono ya mbele. Nawaomba maseneta wote kuunga mkono Hoja hii kwa sababu inaeleza kinagaubaga nia na madhumuni yake. Pia ameeleza wazi wazi sababu za kuunga mkono Hoja hii na ifuatiliwe kikamilifu. Serikali ya Kitaifa yafaa ihakikishe kuwa jambo hili linakamilika kama ipasavvyo.
view
-
25 Sep 2013 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga mkono.
view
-
19 Sep 2013 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kumshukuru Sen. Anyang’-Nyong’o kwa kuileta Hoja hii. Ningependa kwanza kuichambua Hoja hii. Hoja hii yasema nini? Hoja hii yataka vyama vya kisiasa vipewe ufadhili. Hoja hii haisemi kwamba Chama Cha Jubilee, ODM ama chama kingine kipewe ufadhili. Kinachoonekana katika Hoja hii ambacho ni cha muhimu ni swala la ufadhili ama hela kutoka kwa Serikali. Vyama vinafaa kupewa hela. Je kuna umuhimu wa vyama kupewa hela? Umuhimu upo. Umuhimu huu ni upi? Tunaijua maana ya demokrasia. Tukitaka mambo yafanyike kulingana na Katiba, ni lazima tutumie fedha. Tutaimarisha demokrasia vipi kama ...
view
-
23 Jul 2013 in Senate:
Tell them! Tell them!
view
-
22 May 2013 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza ningependa kutoa shukrani kwa Sen.(Dr) Zani kwa kuleta Hoja hii. Maoni yangu ni kwamba Sen. (Dr) Zani alikuwa anafikiria juu ya Kaunti ya Kwale katika mawazo yake. Hii Hoja ni juu ya Kaunti ya Kwale. Lakini kwa sababu yeye ni Seneta mteule mawazo yake ni ya kitaifa. Mimi nitazungumza juu ya Kaunti ya Kwale. Hii ni moja kati ya kaunti maskini sana. Hata hivyo, ni moja kati ya kaunti zenye utajiri mwingi wa rasilmali. Tuna fuo zakuvutia sana. Mwezi wa Desemba, watu wengi kutoka bara huja kuogelea katika bahari yetu. Lakini watu wetu hawafaidiki ...
view
-
8 May 2013 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ningependa kuungana na wenzangu na Seneta aliyeleta Hoja hii ya Usalama. Usalama ni mojawapo wa haki ambazo Mkenya anatakikana apate anapokuwa katika nchi yake. Sasa imekuwa ni jambo la kawaida kutokuwa na usalama. Utasikia swala hili likizungumziwa kule Mombasa, Kwale, Bungoma na kwingineko nchini. Hata hivyo, katika Serikali kuna vyombo vinavyohusika na kuleta usalama nchini. Tuna polisi wa kawaida na majasusi ambao kazi yao muhimu ni kuchunguza kwa udani. Haya mambo tunayoyazungumzia leo hupangwa katika fikira za wanadamu kabla ya kutekelezwa. Watu hupanga mambo kabla ya kuyatenda. Tuliona katika runinga watu wakigonga madirisha na kuwalazimisha ...
view