20 Jan 2009 in National Assembly:
Mimi ningependa kusema machache. Sisi kama Wakenya tunajivuna kwa sababu huyu ni mmoja wetu. Babake ni kutoka sehemu hii, na sisi, kama Wakenya, tunafurahia siku hii ambayo imepatia nchi yetu sifa kubwa katika ulimwengu mzima. Hata huko Marekani tunaambiwa kwamba wanaume wetu wana soko nzuri zaidi. Kwa hivyo, sisi tunafurahi sana.
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Jambo ambalo ningependa kusema la muhimu ni kwamba kuna mambo ambayo ni lazima tujifunze. Tunaweza kuchagua rais ambaye hana mambo ya ukabila katika roho yake na akawa kiongozi wa Kenya. Kama vile Obama amechaguliwa na Wamarekani bila kuwa na kabila kubwa. Ukabila si kitu ambacho kilimpeleka juu bali ni mambo ambayo aliamini.
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Jambo la pili ni kwamba si lazima kuchagua wazee kuwa viongozi wa nchi ya Kenya. Kila wakati tukienda kwa kura ni kwamba lazima uwe na nywele nyeupe. Hapa Kenya imekuwa ni kama desturi kwamba watu ni lazima wawe na nywele nyeupe. Ndiyo maana viongozi wetu wanajipaka vichwa vyao rangi. Jambo ambalo tunajifunza ni kwamba si lazima tuchague wazee kuwa viongozi wa nchi ya Kenya. Bw. Obama ameingia akiwa na nywele nyeusi na zinazong'ara kama za Bw. Mungatana.
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Jambo la tatu ambalo tunaweza kujifunza ni kwamba tunaweza kuchagua kiongozi wa nchi, ambaye hajahusika na mambo ya ufisadi. Barack Obama amechaguliwa kuwa kiongozi wa Marekani na hajatajwa katika kashfa za ufisadi. Kwa sasa ni lazima tujifunze kwamba kuna watu ambao tunatarajia kwamba watataka urais, na sasa wanaingizwa katika maneno ambayo hayafai. Katika Kenya hii tumesikia kwamba kuna watu wanaokula mahindi ya maskini. Ni aibu kwamba wakati huu ambapo dunia nzima inaangalia Wakenya, kuna vichwa vya magazeti vinavyosema kwamba kuna ufisadi nchini Kenya. Kuna wengine ambao wanataka ukubwa ilhali wanahusika na kashfa ya mafuta. Tumesikia kashfa ya mahindi hapa Kenya ...
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
4254 PARLIAMENTARY DEBATES January 20, 2009
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Do you want to inform me? Let him inform me on the issue of corruption.
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, kitu ambacho tungependa kusema ni kwamba---
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Tena kuongezea, wanataka kuwa marais. Ni aibu kwamba sisi hapa Kenya tunaona vichwa vya magazeti. Kuna kashfa ya Triton, ambayo ni ya Kshs7 billion. Tuna na kashfa ya mahindi ya karibu Kshs1 billion. Tuna kashfa katika utalii ya Kshs35 million.
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Jambo lingine ambalo tumejifunza leo ni kwamba unaweza kuwa kiongozi hapa Kenya bila kuingia katika kuhusishwa na kashfa za ufisadi. Tunaomba kwamba wakati wa kura ya mwaka 2012, tuangalie swala la tatu ambalo tumejifunza kutokana na ushindi wa Rais Barack Obama. Si lazima uwe mfisadi, ama uwe na kabila ama pesa. Tunaweza kuchagua mtu ambaye atasaidia nchi hii na atupeleka mbele, na si wafisadi wanaotaka ofisi kubwa.
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Kwa hayo machache ninashukuru kwa kunipa nafasi.
view