All parliamentary appearances
Entries 281 to 290 of 993.
-
2 Nov 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu wa Spika. Nashukuru kwa nafasi hii kwamba mhusika mkuu katika mchakato wa kubanduliwa nje ya kiti apewe nafasi hii kujieleza wazi, Wakenya wakisikiza. Vile vile, madai ambayo viongozi wa wadi wako nayo, waje wajieleze na stakabadhi zinazoweza kudhibitishwa na Seneti. Halafu, kama ni kunyolewa, watu waandae maji, sabuni na haki itendeke kwa yeyote ambaye atakuwa na makosa. Iwapo hana makosa, atasamehewa. Ninavyofahamu ni lazima kila mtu awajibike katika uongozi. Tutakuwa tunampa nafasi, yeye na Bunge la Kaunti, ili waaajibike kutokana na hoja watakozoleta Seneti. Gavana na wenzake wawe kielelezo kwa magavana wengine Kenya hii watakaojipata katika hali ...
view
-
2 Nov 2023 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Ningependa kuanza na ya kwanza. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu Nambari 53(1) kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Elimu, kuhusu ongezeko la visa vya mimba za mapema kwa wanafunzi wa shule za upili katika Kaunti ya Bungoma. Katika kauli hiyo, Kamati iangazie yafuatayo - (1) Iarifu Seneti kuhusu idadi ya wanafunzi wa shule za upili katika Kaunti ya Bungoma waliopata mimba mwaka huu wa 2023, ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2022. (2) Ibaini sababu zinazopelekea kuongezeka kwa visa hivyo vya mimba za mapema, hususan katika shule ya Upili ya St. Thomas ...

(3) Ieleze hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya wahusika waliowapachika mimba wanafunzi hao, ili kukomesha hali hii ambayo imeathiri viwango vya masomo katika kaunti hiyo.

31 Oct 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa wakati huu kuchangia. Wakati gavana huyu alikuwa hapa kujitetea alipoletwa na kaunti yake husika, aliponea chupuchupu. Utetezi wake ulifanywa katika kikao ambacho hatukuwepo lakini kwa sababu ya uamuzi wa jumla wa Seneti kwamba waliyokubaliana nayo pia sisi tukubali, tukakubali shingo upande. Watu wa kaunti hii wana mambo ambayo wangependa kusikia yakitajwa, yakijadiliwa na yakizungumziwa peupe mchana. Pia wanataka kujua rafiki yao ni nani na asiyekuwa rafiki yao ni nani. Wanataka kujua kama Seneti inajua yanayoendelea katika kaunti yao ama hapana. Wanajua kwamba katika majadiliano ya watu wachache, kuna mazungumzo ya chini kwa chini ambayo hao ...
view
-
31 Oct 2023 in Senate:
Leo, wana nafasi kusikia wazi. Wale wanaoitwa madaktari, maprofesa na walimu wadhihirishe uwezo wao wazi mchana kadamnasi. Ni wapi ama ni shinikizo zipi zinahakikisha kwamba wanapata haki ama nafasi ya kujieleza kwa sababu Seneti ni Bunge la kutetea ugatuzi.
view
-
31 Oct 2023 in Senate:
Iwapo viongozi kama Wabunge wa Kaunti wamekata kauli kwamba lazima Pilato awape nafasi wamsulubishe Barnabas ama Yesu, sisi ni nani tuje hapa tuchukue nafasi yao kana kwamba hawana akili ilihali ni watu timamu kuambiwa hatima yao?
view
-
31 Oct 2023 in Senate:
Naomba msamaha na naomba kuondoa. Lakini kabla sijakaa, watu kwetu husema, fisi aliambia jiwe ‘japo umenyamaza, lakini umesikia.’
view
-
19 Oct 2023 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I rise pursuant to Standing Order No.53(1) to seek a Statement from the Standing Committee on Education concerning the operational viability of the Webuye Campus of the Masinde Muliro University of Science and Technology. In the Statement, the Committee should- (1) Provide a report on the operational status of the Webuye Campus, Masinde Muliro University of Science and Technology, shedding light on reports that the campus is collapsing; (2) State the number of students at the campus and disclose steps and actions that have been initiated to address reported decline of student population at the ...
view